Pinda: Tuhukumuni sisi, kiacheni chama, Serikali

Pinda: Tuhukumuni sisi, kiacheni chama, Serikali

Tungeacha kukihukumu chama iwapo chama chenyewe hicho kingechukua hatua dhidi ya mafisadi walioko ndani yake. Lakini kwa kuwa chama hichohicho kinaendelea kuwabeba watuhumiwa hao na kuwapongeza kwa "ushujaa wao" wa kujiuzulu, tunashindwa kutenganisha kati ya CCM na mafisadi walioko ndani yake.

Na jambo la pili waungwana, hivi yale matawi ya vyama vya siasa kwenye maeneo ya kazi na taasisi yaliruhusiwa tena upya lini? Kwa kumbukumbu yangu ni kuwa matawi ya aina hiyo yaliondolewa rasmi baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kumbe yamerudi tena? Na je kina TLP, CUF, CHADEMA, DP et al nao wanaruhusiwa kwenda kuanzisha matawi yao huko kwenye vyuo vikuu, au wao pia wakifanya hivyo itaitwa fujo?
 

Na jambo la pili waungwana, hivi yale matawi ya vyama vya siasa kwenye maeneo ya kazi na taasisi yaliruhusiwa tena upya lini? Kwa kumbukumbu yangu ni kuwa matawi ya aina hiyo yaliondolewa rasmi baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kumbe yamerudi tena? Na je kina TLP, CUF, CHADEMA, DP et al nao wanaruhusiwa kwenda kuanzisha matawi yao huko kwenye vyuo vikuu, au wao pia wakifanya hivyo itaitwa fujo?

kuna bwana mdogo alikua kama wakala wa CHADEMA St August pale mwanza (2005) alipewa kazi ya kugawa Card za chama tu lakini alisumbuliwa sana na usalama wa taifa na walim wake,, ntamtafuta nimkaribishe ili aje atoe ushuhuda kitu kilichompata
 
Unajua kuna siku moja member mmoja hapa JF alisema huyu mkulu naye anaongea sana matendo hakuna, somehow ninaanza kuamini!

Damn!
 
Bwana Pinda asitake kusahau kuwa wao ndio chama na serikali. Hii kauli naamini kuwa hajaitoa kwa bahati mbaya, ni katika ule mkakati wao mahsusi wa kuwalinda mafisadi.Huyu huyu Pinda ndiye katuambia serikali haina uwezo wa kuwafikisha mahakamani!
Kiujumla ni kuwa Pinda keshafundishwa sarakasi za CCM na serikali yake.
 
Pinda tumechoka na usanii. Fisadi Mkapa kama kiongozi wa CCM alijihusisha na ufisadi, Sumaye naye kama waziri mkuu alikuwamo kwenye ufisadi, Lowassa naye, Karamagi, Msabaha, Chenge, Mramba, Meghji, Rostam Aziz, Mkono, Mzindakaya wote hawa wamehusishwa na ufisadi kwa namna moja au nyingine. Na wote hakuna hata aliyeguswa na mkono wa sheria. Halafu unataka kuwaambia Watanzania wasiihusishe CCM na sirikali na ufisadi uliofanywa na hawa mafisadi wa CCM! 😕
If you have nothing important to say it is better to keep quiet rather that issuing unintelligent statements

Pinda aikingia kifua CCM, Serikali

2008-05-03 09:15:09
Na Mwandishi Maalum

Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, amesema CCM na serikali yake visilaumiwe moja kwa moja kwa mapungufu ya mtu mmoja mmoja kwa sababu vyombo vyote hivyo viwili ni safi.

Alikuwa akizungumza eneo la Kihesa mjini Iringa jana wakati wa uzinduzi wa tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini na kutoa kadi kwa wanachama wapya 700.

Alisema tuhuma kuhusu rushwa na wizi ni kwa mtu mmoja mmoja ambaye atakuwa na mapungufu yake, lakini siyo kwamba ni sera ya Chama chao na Serikali yake.

``Chonde chonde, nihukumuni mimi Pinda kwa yale ninayokosea muondoeni Pinda kama ni tatizo lakini chama kiendelee na Serikali yake kwa vile ni utaratibu wa kujisafisha tu.

``Chama hiki (CCM) ni kizuri na serikali yake nzuri, kama kuna mapungufu basi yatashughulikiwa na hatua zitachukuliwa.``

Akijibu hoja katika risala ya tawi hilo kuhusu ajira kwa
wahitimu wapya na kupanua wigo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, alisema serikali itajitahidi kuhakikisha wahitimu hao wanatumika vizuri.

Alisema pia utaratibu wa mikopo haujapangika vizuri kwa kuwa lazima kwanza kuwajua wote wale wasiokuwa na uwezo wanaohitaji hasa mikopo hiyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alipinga hoja kwamba Serikali imeharakisha kuanzisha vyuo vikuu kadhaa bila ya maandalizi ya kutosha ya uwezo wa kuviendesha.

Alisema nafasi za vyuo vikuu lazima ziongezeke kwa vile usipofanya hivyo basi utakuwa na vijana wengi waliomaliza sekondari tu na hilo litakuwa tatizo kubwa zaidi.

Waziri Mkuu alizindua tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini katika shughuli iliyopangwa kutekelezwa muda mfupi kabla ya kurejea Dar es Salaam kutoka Iringa ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi kitaifa juzi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.

SOURCE: Nipashe
Hapo ana maana kwamba Chama kikifanya vyema then ni utekelezaji wa sera na ilani za chama wakati huo huo kama kikifanya ufisadi the ni individuals are to blame!
Kwamba sasa sio sera mbovu tena!
Kwamba chama ni safi na hakihitaji mabadiliko wala hakihitaji kupigana vita dhidi ya ufisadi!
Ama kweli viini macho! Mhn!
Najua pia kuna watakao uliza..Fisadi aone ufisadi?Is that possible?
Kwamba kama unakula nyama ya mtu na mwenzako akiila utaona ni mbaya?
Ooops is it too hard to figure out!?
 
Bwana Pinda asitake kusahau kuwa wao ndio chama na serikali. Hii kauli naamini kuwa hajaitoa kwa bahati mbaya, ni katika ule mkakati wao mahsusi wa kuwalinda mafisadi.Huyu huyu Pinda ndiye katuambia serikali haina uwezo wa kuwafikisha mahakamani!
Kiujumla ni kuwa Pinda keshafundishwa sarakasi za CCM na serikali yake.

Peter Pinda anapindisha ukweli tu si kwamba kesha fundishwa na CCM.Pinda maisha yake yote ni mwana CCM hadi akawa waziri na kashika nyadhifa kibao bado tu hawezi kujua longo longo zao ?
 
wahenga wanasema "uozo wa baba huigharimu familia".
sasa uozo wao ndo unaigharimu CCM...huyu naye hana jipya
 
Malezi aliyoyapata Pinda kutoka kwa Lowassa (kama alivyokiri mwenyewe siku alipoteuliwa) ndiyo yanayomuharibu. Hata Lowassa alisema Pinda anafanana nae sana, na haikukanushwa! Tulidhani tumekung'uta tandiko letu kumbe tumelipinda tu, na kunguni wamejisetiri ndani ya pindo hilo, na wanaendelea kujitokeza na kutuuma na kurudi kwenye pindo! Pengine badala ya kupinda tu ingefaa kuifua kwa maji ya moto na kuinyoosha kwa pasi yenye joto kali, au labda kuichoma moto kabisa iungue na kunguni wake tutafute mpya!
 
Peter Pinda anapindisha ukweli tu si kwamba kesha fundishwa na CCM.Pinda maisha yake yote ni mwana CCM hadi akawa waziri na kashika nyadhifa kibao bado tu hawezi kujua longo longo zao ?

hapo nimekusoma lunyungu.
na tokea yupo ngazi za chini alikuwa anaona jinsi mambo yanavyokwenda, na ni lazma aende kwa njia wanazotaka wenzake na ni wazi kuwa akipindisha atakuwa amekiuka maadili ya CCM so wabongo wasitegemee kipya kutoka kwa huyu mzee ni uongo tu uliowajaa hawa jamaa
 
hivi mbona sijasikia akifanya mabadiliko katika ofisi yake,,maana najua Lowasa alikua na ka-network ka kwake pale,,au ndio kubebeshwa mzigo
 
na watu wa vyuoni acheni kujipendekeza kwa wakubwa bwana mkisikia anakuja mnabuni vitu vya ajabu ili muonekane kwa mkuu,,,Na nyie wasomi wazima mmeshindwa kumwambia palepale kuhusu maswala ambayo waTanzania wanayatolea macho??!1 wasaliti nyie
 
Pinda anajaribu kurudisha imani kwa watanzania, ila bado wanashindwa kutekeleza hata moja kati hayo wanayoyasema, sisi tutaendelea kutega masikio, Pinda just do any thing watanzania waamini usemacho.

Kama kweli ana nia ya kurudisha imani kwa Watanzania, basi cha kufanya ni kuiacha sheria ichukue mkondo wake dhidi ya wafisadi wote akiwemo fisadi Mkapa na kama wakionekana wana hatia basi wafilisiwe. Hili likifanyika litarudisha credibility ya serikali kwa wananchi kwa kiasi kikubwa sana.
 
nyerererist pole kwa kuchelewa kumjua.
huyu jamaa ni bure kabisa, yaani JK aliwadanganya watanzania kwa kuchagua mtu mwenye sura ngumu ili wajua kuwa sasa dawa imepatikana ila hamna lolote...
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu tafadhali mweke ktk kitimoto maanake yawezekana hafahamu uzito wa kauli yake.

Inashangaza sana viongozi wetu kila siku huja na hadithi za kukitetea chama ambacho chini ya maazimio yake wameweza pimdisha sheria za nchi Kitaifa - Ufisadi ni Haramu yet, kwa muda wa miaka isiyopungua 7 wamefumbia macho Ufisadi na kuuhalalisha.
Haiwezekani kabisa kama kweli ana akili timamu kutetea hoja ya uchafu huu wa CCM kusema ni uchafu wa baadhi ya watu ambao hadi leo hii watu hawa hawa ni viongozi ndani ya chama. Kama kweli chama hakina makosa basi hiki chama kingechukua hatua mapema kabla hata viongozi hawa kujiuzuru ama kuachishwa kazi (wadhifa) na rais ktk mabadiliko ya mawaziri ambayo bado hatujasikia wakiwajibishwa..
Makosa ya chama ni kuendelea kutumia timu ya wachezaji wachafu ambao ktk ligi hii ya maendeleo tunagigwa mabao kila siku. Sasa tunapotoka uwanjani tumeshindwa tusiseme kuwa ni m,akosa ya timu nzima isipokuwa baadhi ya wachezaji ambao bado wanacheza!...

Binafsi siafiki swala la kufukuzwa Uanachama kwani kila Mtazania ana haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote kile akipendacho hata yule Jambazi kizimbani anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama chochote bila masharti yanayohusiana na CV ama kazi yake isipokuwa kuendelea kuwepo kwa viongozi hawa kama viongozi ndani ya chama hili li kosa kubwa la chama kizima.
Nina hakika kabisa kama CCM ikija ondoa mwavuli (protection) wa chama juu ya watu hawa basi sheria itachukua nafasi yake kirahisi zaidi.
Chama CCM kinahusika kwa kila Ufisadi ulofanywa na watu hawwa wakitumia jina la chama as a fact waliyafanya yote haya kwa mhuri wa jina la chama...
 
Back
Top Bottom