PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Rebecca Nsemwa wameibuka kidedea katika kura ya maoni ya kumtafuta mwakilishi wa Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Njombe kwa nafasi ya ubunge wa viti maalum CCM.
Wawili hao wamepata kura 700 na 588 mtawalia, katika uchaguzi uliohusisha wajumbe 841. Msimamizi wa Uchaguzi, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (MNEC) wa Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwanselela, amesema wajumbe waliopaswa kuwepo ni 861 na waliohudhuria na kupiga kura ni 841 na kura moja imeharibika.
Amewataja wagombea wengine na kura zao kuwa ni Neema Mgaya (kura 263), Anna Mwalongo (53), Dk. Scholastika Kevela (47), Tegemea Mbogela (22), Magreth Kyando (5), na Tulalumba Mloge kura 3.
Amewataja wagombea wengine na kura zao kuwa ni Neema Mgaya (kura 263), Anna Mwalongo (53), Dk. Scholastika Kevela (47), Tegemea Mbogela (22), Magreth Kyando (5), na Tulalumba Mloge kura 3.