Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala, ameeleza kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, uliotupilia mbali mapingamizi ya chama hicho katika shauri la mgawanyo wa mali.
Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatano, Februari 11, 2026, na Jaji Hamidu Mwanga. Shauri hilo la madai lilifunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed na wenzake wawili, wakidai usawa katika mgawanyo wa rasilimali na mali za chama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Dkt. Nshala amebainisha kuwa ingawa wameupokea uamuzi huo wa mahakama, chama hakikubaliani na misingi ya kisheria iliyotumika kutupilia mbali mapingamizi yao.
Uamuzi huu unafungua milango kwa kesi ya msingi kuanza kusikilizwa baada ya mapingamizi ya awali (preliminary objections) yaliyowekwa na CHADEMA kugonga mwamba.