Elections 2010 Pingamizi la CHADEMA latupwa

kinacho mshinda mnyika kutoa hadharani hayo maamuzi na kusema ni siri
kama mnaona mtaadhirika kaeni kimya milele

Si ushaambiwa ni CONFIDENTIAL?

Na kama ushajua "akisema tutaadhirika" why the hell unauliza kinachomshinda Mnyika kusema?
 
Huu uamuzi imebidi uchukuliwe kutokana na dharura wanayoiona mbele yao, but this is going down into the books of history for generations to see. Ni moja kati ya vitu ambavyo vitamfanya Kikwete aonekane ni one of the worst performing president Tanzania has ever seen.

Hongera CHADEMA, your smartness inaendelea kuwaforce CCM kufanya makosa ambayo wasingependa kuyafanya. Kwanza mlianza na kumpata mgombea ambae amesababisha Kikwete avunje sheria aliyoisaini mwenyewe mbele ya mabalozi kwa kuongeza mshahara kinyemela. Lakini pia mmeifanya tume ya uchaguzi wafanye kosa lingine la kupindisha maamuzi baada ya kukata rufaa. That shows how clever you guys are, haya ni mapambano dhidi ya MAFIA soon nchi nzima itajua kuwa kumbe tumelipa nchi kundi la watu ambao wanatumia chama cha siasa kama kichaka cha kutumaliza. Hii vita haitaisha, believe me and well done CHADEMA!!!
 
Asante Tendwa nilikuwa naiwazia hiyo nyongeza mpaka basi, na bajeti nilishaipangia, now am very happy kumbe mwanangu anaweza kusoma english medium mwakani, yalah.... but my kura i reserve to no body.
Wewe unawazia english medium wengine hata hilo darasa la chini ya mti hawana, kama Kikwete kaiba kwenye bajeti ya elimu kulipa mishahara, sasa huyu mtoto wako akifika na kukosa dawati na vitabu na mwalimu atafanyaje au utampeleka tuiton jaribuni kuwa na upeo mrefu wa fikra usiishie kwenye urefu wa pua.
 
Well said, watu wanafikiri ni kitu kidogo kinachoendelea lakini ni kikubwa sana mambo ya Kenya yalianza hivi hivi kwa msajili kuchezea katiba. Kwa wanaoona mbele hii move ni ya ukombozi hata kama sio leo lakini historia imeandikwa haitafutika milele lakini kwa wanaoona kesho watafurahia eti wameongezwa mishahara hawajui kesho na kesho kutwa rais anaweza kuitumia hiyo hiyo sheria kufuta nyongeza bila idhini ya bunge.
 
Tendwa angemsukuma nje mgombea wa ccm angejuta kuzaliwa.
Sisi wooote tumeonekana maamuma wa sheria.
Katiba imevunjwa dhidi ya mgombea binafsi... tukaambiwa na mahakama ya juu kwamba ni suala la kisiasa zaidi
sheria mpya imevunjwa kabla haijapoa kabatini.... tunaambiwa hakuna hoja na haijavunjwa.
Kumbe mwenye mpira akigoma na mechi inaisha!!! haya kaka Tendwa, tegemea mwanao aliyeko pale ikulu kupata ubunge wa kuteuliwa.

Sasa msitegemee eti NEC wataendesha uchaguzi wa haki bin sawa. Lazima kura zitachakachuliwa ili wenye kulazimisha kushinda watashinda kwa kishindo cha kushinda.
Yangu ni hayo tu
 
Bilioni 1 kwa fisadi kiwembe? Natumai atalipa kabla ya kuburuzwa mahakamani!
 
Nilitegemea jambo kama hili, hata asiyejua undani wa sheria ilovunjwa angeweza kuona kosa lilipo. Ndo mambo ya bongo bwana nyie acheni tu!
 
Mi huwa najiuliza hivi watu kama Tendwa huwa dhamira zao haziwasuti kweli,wanapokuwa chumbani peke yao huwa hawafikirii kuwa wanayoyafanya ni makosa ambayo hayatafutika vizazi na vizazi,ni kweli hawana ujasiri wa kuifuata sheria bila kujali nini kitawatokea wao na familia zao?Au ndo hivyo wana madudu ambayo waliyafanya na utawala uliop unawalinda?
 


Wazee walishajua kuwa wanaelekea kupotea hivyo wanafanya kila aina ya miujiza ili kumaliza maisha yao kwa style hiyo. Hawana uchungu na nchi wala hakuna cha masikini wa Tanzania au kuendeleza nchi. Tendwa katishwa au ndo kaahidiwa mambo kibao ili watu watoke.
 

yaani uwezo wangu, kufikiri ni mkubwa kushinda hao viongozi wenu wa chadema waliopeleka pingamizi :becky:! unazungumzia bajeti we unajuwa bajeti ni nini..?
 
Tendwa ni mbumbumbu wa sheria ya garama za uchaguzi. off course no one expected that kikwete angeenguliwa ila hili pingamizi nileacha kumbukumbu (precedent) that CHADEMA responsibly raised eyes brows when the election expense laws is being violated by CCM!!!!!
 

Nahisi tendwa siye aliyefanya hayo maamuzi. Bila shaka hiyo barua ameandikiwa na CCM yeye alitakiwa kusaini na kutuma. Ndio mana alikosa ujasiri wa kuweka hadharani maamuzi, na hata hakuwa na uchangamfu wake wa kila siku alipoongea na waandishi wa habari!
 
Leo kutakuwa na press conference Makao Makuu ya CHADEMA. Pamoja na mambo mengine wanasheria wetu watatoa reaction ya CHADEMA juu ya maamuzi ya Tendwa. Cha kuchekesha kuliko vyote katika 'hukumu' ya Tendwa ni kukana kwamba serikali, kufuatia matamshi ya JK, haijaongeza mshahara katika kipindi hiki cha kampeni na baada ya bunge kumaliza kikao chake. Haya ni maelezo ambayo CCM watayajutia kisiasa kwa sababu inamaanisha kwamba walikuwa wanawadanganya wafanyakazi kwamba mshahara umeongezwa kutoka Sh 135,000 hadi 265,000! Tunaunganisha data kamili na tutawaletea wananchi waamue wenyewe. Lakini kilicho wazi mwaka huu ni kwamba hatimaye uongo utajitenga na ukweli!
 
Yaani wewe post ya kwanza unaanza na kuomba updates kuna mtu humu ulimtuma be serious mpigie simu Tendwa atakuwa nazo
Ringmaster
Join Date Mon Sep 2010
Posts 1
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power 0

Hawa ni wale walioingia baada ya kipindi kilichorushwa redioni juzi jumamosi kuhusu JAMIIFORUM.Wako wengi humu.
 

Asante Kitila;

Tunahitaji kusikia balanced news.

Sasa hivi more than 80% ya Media imebakwa na haizungumzii kwa uhakika habari za upinzani (I like to call "Ushindani")

Stay focused badala ya kusiliza propaganda nyingi.
 

Safi sana kamanda. Sasa inabidi hawa jamaa wajipange upya kukanusha kuwa mishahara haikupanda. Lakini la kushangaza zaidi ni pale watu wameshachukua mshahara ukiwa na hilo ongezeko, je, hiyo ni hongo au posho ya kuhudhuria mikutano ya CCM?
 
Simple logic kama Tendwa ni mteule wa Raisi then hawezi amua ndivyo sivyo kibarua kitaota nyasi.
Inasemekana amelitupilia mbali ilo shauri na katoa very okward answers.
Ila nimesikia akina Tundu Lissu wanalifanyia kazi jibu lake.
 

Mr. Mkumbo
Mimi nina wasiwasi sana kuwa barua iliyowafikia kueleza matokeo ya pingamizi lenu itakuwa imeandikwa na CCM, na kumpa Tendwa asaini tu kama hawajafoji saini yake. Ndio mana Tendwa hakuwa na confidence kama tulivyomzoea, kusema maamuzi hayo. Na kwa jinsi Viongozi wa CCM walivyoishabikia hasa point ya kuwa "Imeleta usumbufu" ambayo haina uhusuano na maamuzi ya rufaa, inaonyesha wao ndio walio draft hiyo barua. Habu Unganisheni data mtujuze!!
 

Nafikiri badala ya kumlaumu Tendwa, kunachotakiwa ni kuthibitisha kama hiyo nyongeza ya kufikia 265,000 inatolewa na kuna watu wanaipata (au nyaraka zozote) na si kutegemea magazeti ambayo yanakosea kila siku. waziri wa utumishi na waziri wa fedha wanasemaje?. nyaraka za mishahara zilizopo ni zile za kufikia 135,000/= tu, huenda suala hili ni uvumi tu kama uvumi wa kuwa ukipokea simu sijui namba gani unakufa.
suala la kutoa ahadi halina msingi kwani mbona na Dr. Slaa anatoa ahadi hizo hizo hatuwezi kusema ni rushwa. mf. kutoa elimu bure ni ahadi tu kama kununua meli.
otherwise CHADEMA msipoteze muda kwenye hili, na msiweke resources nyingi kwenye hili mtakuja kugundua ikiwa too late, au ndiyo njia ya kutafuta visingizio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…