Pingamizi lingine lawasilishwa dhidi ya ushindi wa Uhuru Kenyatta

Pingamizi lingine lawasilishwa dhidi ya ushindi wa Uhuru Kenyatta

eliakeem

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Posts
17,214
Reaction score
15,853
Muda mfupi kabla ya kufungwa kwa nafasi ya kuwasilisha pingamizi dhidi ya ushindi wa Uhuru Kenyatta, wapinzani wamewasilisha pingamizi hilo mahakamani.
yanayojitokeza:

1. Uchaguzi huu ulikuwa na mapungufu ya wazi, je si dhahiri kuwa utafutwa na Kenya kuingia kwenye uchaguzi mwingine?

2. Gharama za uchaguzi hazitaelemea nchi?

3. Je kipengele cha kuruhusu kuhoji ushindi wa urais kinapaswa kifikiriwe upya?
Wajumbe maswali ni mengi mno. Karibuni kutoa maoni.
 
huu mchezo utaisha mpaka wakati gani??
 
Mmoja afe tu aongeze samadi nchi iendelee
 
muda mfupi kabla ya kufungwa kwa nafasi ya kuwasilisha pingamizi dhidi ya ushindi wa Uhuru Kenyatta, wapinzani wamewasilisha pingamizi hilo mahakamani.
yanayojitokeza:
1. uchaguzi huu ulikuwa na mapungufu ya wazi, je si dhahiri kuwa utafutwa na Kenya kuingia kwenye uchaguzi mwingine?
2. gharama za uchaguzi hazitaelemea nchi?
3. je kipengele cha kuruhusu kuhoji ushindi wa urais kinapaswa kifikiriwe upya?
Wajumbe maswali ni mengi mno. karibuni kutoa maoni.
Tulia usituchafulie our best constitution in Africa
 
Hakuna mtu kufa bali ni mtu mmoja kuzuiliwa na mahakama basi ndiyo dawa
 
  • Thanks
Reactions: MCB
Hakuna mtu kufa bali ni mtu mmoja kuzuiliwa na mahakama basi ndiyo dawa
kuuana hawata uana. lkn issue ni kile kitendo cha kuwa na uchaguzi zaidi ya miezi mitatu. hiyo ni shida sana.
 
Nina swali moja tu kwa watz wote kwenye jukwaa hili. Hivi zile fedha za road fund zilikuwa shilingi ngapi? Dah, Jembe lenu la kweli linatrend kule twitter. Tingatinga kiboko yao! Nimekubali.
hilo ni gumu kulijua. lkn Yeye huyo mkurugenzi ana wajibu wa kujua kama afisa maduhuri (accounting officer).

btw tuendelee na hoja iliyopo mbele yetu. haya mambo ya kupinga uchaguzi mahakamani yataisha lini?
 
Tunaambiwa Tanzania katiba yetu ni mbovu kisa haina kipengele cha kuhoji matokeo ya uchaguzi wa rais. Ila nadhani endapo uchaguzi wa Kenya utarudiwa tena watu watajitafakari kuhusu kelele zao za kupigania hicho kipengele. Haiwezekani nchi ikawa inapeleka tu pesa kwenye uchaguzi eti kisa watu fulani hawajaridhika na matokeo.
 
hilo ni gumu kulijua. lkn Yeye huyo mkurugenzi ana wajibu wa kujua kama afisa maduhuri (accounting officer).

btw tuendelee na hoja iliyopo mbele yetu. haya mambo ya kupinga uchaguzi mahakamani yataisha lini?
Ningekuambia lakini naogopa kusema uongo. 😀😀😀Classic Tanzanian reply. Huyo mkurugenzi hakuwa serious. Nimependa style ya Magufuli, kila mtu ashike adabu zake.
 
Nina swali moja tu kwa watz wote kwenye jukwaa hili. Hivi zile fedha za road fund zilikuwa shilingi ngapi? Dah, Jembe lenu la kweli linatrend kule twitter. Tingatinga kiboko yao! Nimekubali.
Hiyo ni dalili kwamba no nonsense sasa hivi huku Tanzania, hao akina Macharia, Charles Kater, Najib Balala na wengine wengi viongozi wa Kenya, wangekuwa chini ya Magufuli wasingefikisha vigezo vya kubaki kuwa katika nyadhifa zao, wengi hawana uwezo, hawajui mambo, wanadanganya wananchi hadharani na bado watu wanasherehekia, our leardership standard is set very high.

Sent from my MediaPad T1 8.0 using JamiiForums mobile app
 
Ningekuambia lakini naogopa kusema uongo. 😀😀😀Classic Tanzanian reply. Huyo mkurugenzi hakuwa serious. Nimependa style ya Magufuli, kila mtu ashike adabu zake.

mngemchagua Raila saa hii mngekuwa mnaongea lugha ya no nonsense. maana ange replicate system ya Tanzania.
 
Wote wafe...

Maana hawana maana tena.

Ukabila ni Sumu.

suluhisho si kuwaua bali ni kutafuta chanzo cha hali hiyo. huo ukabila wa Kenya unarithishwa. mfano yanayotokea hapo Kenya kwa SASA kizazi kipya young generation inaona na mbaya zaidi inafundishwa ubaya huo. hivyo hata Uhuru na Raila wakifa leo. bado ukabila utakuwepo tu.
 
Sinema za rahila oding'o. Wenzake wanaangaika yeye ashavuta mpungawake anakula Bata tuu.wananchi wenzangu tuwaogope wanasiasa kama ukoma.
 
Sinema za rahila oding'o. Wenzake wanaangaika yeye ashavuta mpungawake anakula Bata tuu.wananchi wenzangu tuwaogope wanasiasa kama ukoma.

Sijakuelwa Mkulu, kavuta wapi huo mpunga wake?
 
We unauliza jibu, hujaona picha last sunday za kanisani wakiwa na uhuru? Wale WanaJuana ila
 
Back
Top Bottom