PISHI: Keki Ya Zabibu

PISHI: Keki Ya Zabibu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Keki_Ya_Zabibu.jpg

AINA YA KWANZA
Vipimo

1. Siagi - 200g
2. Unga - 2 Vikombe
3. Sukari - 1 Kikombe
4. Vanilla - ½ Kijiko
5. Arki rose ukipenda - 2 matone
6. Mayai - 6
7. Zabibu - ¼ Kikombe
8. Baking powder - 2 Vijiko vya chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni 350°c.
  2. Saga siagi na sukari kwa mashine mpaka mchanganyiko ulainike.
  3. Ongeza yai moja baada ya moja na huku ukiendelea kusaga mpaka yaishe.
  4. Tia unga uliochanganwa na baking powder.
  5. Endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri, halafu arki rose, vanilla na zabibu halafu koroga kidogo ilizichanganyike vizuri.
  6. Mimina mchanganyiko katika chombo cha kuchomea.
  7. Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 20 mpaka 25.
  8. Ikisha poa kata kata vipande na tayari kuliwa kwa kahawa au chai.

AINA YA PILI
Vipimo

Unga wa ngano - 2 Vikombe
Siagi - 1 Kikombe
Sukari - 1 Kikombe
Mayai - 6
Vanilla - 1 Kijiko
Baking powder - 1 Kijiko cha supu
Zabibu kavu - 1/2 Kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni moto wa 350°F.
  2. Kwenye bakuli la kuchanganyia keki la machine, saga sukari na siagi hadi ilainike.
  3. Kisha tia yai moja moja huku unaendelea kuchanganya.
  4. Halafu mimina unga uliochungwa pamoja na baking powder na uchanganye vizuri.
  5. Kisha tia vanilla na mwagia zabibu na ukoroge.
  6. Kisha umimine katika sufuria ya kiasi ya kupikia keki iliyopakwa siagi.
  7. Vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 35 au hadi iwe tayari.
  8. Iache ipowe na itakuwa tayari kuliwa.
 
Kwa anayefahamu,je ulain wa keki unaletwa na wingi wa mayai au hamira?
 
Kwa anayefahamu,je ulain wa keki unaletwa na wingi wa mayai au hamira?
Keki haiwekwi hamira dear! Hutakiwi kuzidisha mayai!

Hapo sijaona maziwa /maji ya kufanya unga uwe laini na si ugali
 
Kwenye hamira namaanisha baking powder

Maji/maziwa sijayataja sababu kiwango chake kinaeleweka. Shida yangu ni mayai na hamira(baking powder)

baking powder inafanya keki ijae
ulaini wa keki ni jinsi utakavyochanganya mchanganyiko wako vizuri au ukitaka urahisi zaidi tenganisha kiini cha yai na ute, visage tofauti then baadae changanya kwa pamoja hapo ndio utapata keki laini zaidi na hiyo ndo wazungu wanaita sponge cake
 
Asante mkuu

Back
Top Bottom