Pishi la boga, nakosea wapi?

Zama hizo, tulimpata msaidizi kutokea Kigoma. Baada ya siku mbili au tatu, binti akawa ameshazoea mazingira. Siku moja jioni, akamtambia wife kwamba amepika msosi heavy. Basi wife akawa na shauku ya kujua menu ya kumaliza siku. Mdada akapika boga kwa kujiamini ila hakujua hakuna wapenzi wa boga. Baada ya msosi kuwekwa mezani, tuliona aibu sisi kutokula, ikabidi tulimeze boga vivyo hivyo, japo alishtukia ameingia msikitini na viatu.

Chakula ni kama sigara. Mpaka utambulishwe na mtu ukiwa hujapevuka ndiyo ukipende.
 
Ni aina ya boga ulilonunua, tafuta lenye ganda laini lakini ndani kama kiazi, ukiweza muulize hapo ulipokula akutafutie
 
Unapata boga baya ambalo sio la unga. Halina ujuzi zaidi ya huo. Hata viazi vingine vina unga vingine vya maji maji.
 
Lazima likate stimu Sasa unamix na nyanya halafu unaweka na pilipili hoho Sasa hilo boga au mboga!! Anyway ngoja wataalum waje wakuelekeze maana bora wewe binafsi chai tu inakuwaga na mabuja..😎
 
Kuna mambo mawili unakosea kwanza kipimo cha maji. Inaekekea unaweka maji mengi kama unapika kande (joke). Punguza kiasi cha maji. Pili boga linatakiwa lipikwe kwenye chombo ambacho kikifunikwa hakiruhusu hewa kuingia ikiwa na kuepuka kufunua funua sufuria yako. Huku kijijini tunafunika na majani ya maboga kabla ya kufunika na mfuniko unaobana.Utajua kama limeiva kwa kusikiliza tu mlio wa kuchemka. Ni vizuri ukaipua wakati maji yote yamekauka ndani ya sufuria.

Jaribu lete mrejesho
 
Lazima likate stimu Sasa unamix na nyanya halafu unaweka na pilipili hoho Sasa hilo boga au mboga!! Anyway ngoja wataalum waje wakuelekeze maana bora wewe binafsi chai tu inakuwaga na mabuja..😎
Mmmh hili pishi...kiboko
 
Update:

Nimefata ushauri hapo juu, nimeshapika mara mbili naweka maji kidogo sana nafunika vizuri mvuke haupiti....linaiva kwa mvuke.
Utamu umeongezeka na halipati maji tena next time nikinunua zuri mambo yatakua bam bam...πŸ˜‹πŸ˜‹
 
Mwenyekiti sijui nikutumie haya ya huku kwetu + magimbi; mbona utajinomaaa
Update:

Nimefata ushauri hapo juu, nimeshapika mara mbili naweka maji kidogo sana nafunika vizuri mvuke haupiti....linaiva kwa mvuke.
Utamu umeongezeka na halipati maji tena next time nikinunua zuri mambo yatakua bam bam...[emoji39][emoji39]
 
Mi spendi la kuchemsha
Napenda kupika hivi
Nakata kata vipande vya kawaida naweka kwa sfuria na maji kiasi kisha natia sukari kiasi na chumvi kidogo,na hiriki
Ikitokota imekaribia kuiva natia nazi
Sikorogi maana sipendi iwe uji nakuwa natingisha sufuria
Ni tamu balaaaa
La kumchesha tu mpaka wanaojua shoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…