Pishi la boga, nakosea wapi?

Pishi la boga, nakosea wapi?

Wapishi wa humu nawasalimu.

Napenda sana kula boga, ila upishi wangu unanikatisha tamaa, nikinunua boga kwenye migahawa huwa nakula linakua zuri linakua na unga unga kama kiazi kitamu.

Ishu sasa nije nilipike mimi, linakua lina maji maji, yani linanyonya maji sijui likiiva nikiliweka kwenye sahani linavuja maji tu (mchuzi maji)... hata halivutii tena kula linakata stimu. Nakosea wapi?

Huwa naandaa hivi: nalikata vipande namenya maganda, naweka kwa sufuria, chumvi kidogo na maji kidogo nachemsha.

Ila matokeo ndio hayo mimaji, kuna upishi mwingine? Au nakosea kuchagua boga? ( Siku zote sijui tu kuchagua mmh).
Niliwahi kusikia linatakiwa kuanikwa kabla ya kupika, ni kweli?
Naombeni ujuzi.
Mimi napenda maboga pia.Ila pia haya maboga ya bongo ni ya kama kamali vile,unaweza bahatisha .Sema namna nyingine ya kujua boga zuri ni lile lenye uzito mkubwa,yaan linakuwa dogo kwa size ila zito sana.
otherwise unavyopika ndiyo hivyo hivyo yanapikwaga.
 
Unazungumzia pitiku wewe.

hiyo unatakiwa ukaange.

mboga ya mabogo maji maji huwa ni libaya kwangu
Pitiku linoga lya chupuchupu, la ngali mahuta, afu livya la chihuku mweeh livya la kijani mukumuku, ukateleka na ugali wa sembe la kuloweka, ooooh ujiruma minu. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwangu mie.
Nikishakata vipande, naosha naweka kwenye sufuria inayowiana, naweka chumvi na maji kidogo nafunika na mfuniko sawia.
Ndan ya dk 20, napunguza maji ili boga litoe unga unga, baada ya dk 10 naipua linatoka safi, hapo. Linafaa kwa kuliwa.
Utamu tyuuuh,
 
Pitiku linoga lya chupuchupu, la ngali mahuta, afu livya la chihuku mweeh livya la kijani mukumuku, ukateleka na ugali wa sembe la kuloweka, ooooh ujiruma minu. [emoji23][emoji23][emoji23]
Pitiku ni chakula gani tena hicho...
 
Back
Top Bottom