Pishi la mchanganyiko wa Dagaa wa nazi, nyanya chungu na bamia

Pishi la mchanganyiko wa Dagaa wa nazi, nyanya chungu na bamia

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Mahitaji


  • Dagaa waliokaushwa ( 2 kikombe cha chai)
  • Bamia ( 5)
  • Nyanya chungu ( 5)
  • Tui la nazi ( 1 kikombe cha chai)
  • Nyanya (kubwa 2)
  • Kitunguu (onion 1)
  • Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai
  • Limao ( 1/2)
  • Chumvi ( kiasi)
  • Pilipili mbuzi ( 1)
  • Mafuta (veg oil)

Matayarisho

Safisha dagaa na uwaweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia dagaa wakaange kidogo kisha tia chumvi, pilipili, curry powder, bamia na nyanya chungu, koroga vizuri mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri kisha tia nyanya na ufunike.

Pika mpaka nyanya iive kisha kamulia limao,na pia hakikisha nyanya chungu na bamia zimeiva kidogo(usiache mpaka ziive sana manake zitavurugika pindi utakapotia tui la nazi) kisha malizia kwa kutia tui la nazi na uache lichemke mpaka rojo ibakie kidogo. Hakikisha nyanya chungu na bamia zimeiva ndo uipue. Na hapo dagaa wako watakuwa tayari kwa kuliwa na wali au ugali.
 

Attachments

  • DAGAA.JPG
    DAGAA.JPG
    8.2 KB · Views: 1,008
Duh. Ukishaweka dagaa basi tena. Nakimbia mlo
 
Back
Top Bottom