Pita, achia msemo maarufu wa kishule unaoukumbuka (mwanafunzi/mwalimu/mzazi)

Pita, achia msemo maarufu wa kishule unaoukumbuka (mwanafunzi/mwalimu/mzazi)

Colabo- chombo Fulani hivi asubuhi hutumuka kunywea uji na kbebea vitafunwa,mchana na jioni kinatumika kumix mazagazag yote Kwa wakati mmoja ugari,maharage,kachumbari na mbogamboga.

Kupuliza- unakunywa uji pasipo vitafunwa inakuwa unaupuliza tu uji
 
Wakuu...

Habari ya jumamosi tulivu hapo ulipo??

Umeshapata chai????

Sasa sikiliza nikuambie,

Najua ulishapita shule, iwe chekechea, vidudu, msingi, sekondari hata chuoni.

Kama utakua unakumbuka vizuri, tulikua na:
1. Majina ya utani ambayo iwe mwalimu au mwanafunzi kutaniwa

2. Misemo ya kiutani au ya kiukweli ambayo ni maarufu tulikua tukiitumia katika mambo ya ufaulu, ulipaji ada na kadhalika

3. Au hata sehemu yoyote ambayo inajihusisha na elimu kwa ujumla..


Sasa kwanini nimeandika hivi??

Ni hivi, leo nilipo amka asubuhi, nikawa nimekumbuka sana enzi nasomesha.

Ilikuwa ikifika kipindi cha ulipaji ada mambo yanakua moto sana utasikia

"January hii bwana hakuna hela"

Sasa naomba wakati tukiendelea kuvinjari mapumziko

Dondosha utani wako unaoukumbuka kwenye kada ya mambo ya kishule ...

Niko hapa nasubiri kusoma unachokikumbuka

1.. 2.. 3... twende kazi
Tulianzisha neno
Kisanga....yaani mtu kuwa na tuhuma...neno hili limetumika nchi nzima...nakumbuka hii ilitokana na mwanafunzi mmoja kwa jina la........Kisanga kila school baraza alikuwa na tuhuma🙃
 
Back
Top Bottom