Pita hapa uone jinsi AI inavyotumika kutimiza ule unabii unaohusu mwisho wa dunia!

Pita hapa uone jinsi AI inavyotumika kutimiza ule unabii unaohusu mwisho wa dunia!

Ooh good. Sasa mbona unaomba CCM iwe na mwisho? Hujui kwamba ndani ya CCM kuna wapendwa walio katika Kristo kama wewe, waishio nuruni? Unataka hao nao wawe na mwisho?!!
Dada mbona unazungumza kwa usahiihi sana? Yaani kama roboti Hivi.
 
Aliyelala ni wewe usiyejua kuwa dunia imekaribia mwisho. Zinduka haraka
Swala la kunyakuliwa kwenda mbinguni hapana halipo hivyo!

Mwisho wa dunia ni mwisho wa uovu ,kisha Dunia itaumbwa upya .Watu wema wataebdelea kuishi humu humu duniani
 
Mbingu na nchi zikipita, hakuna kitakachobaki isipokuwa maneno ya Yesu tu.
Mathayo 24:35
"Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe."
Ubarikiwe mtumishi kwa NENO la Uzima....🤝🤝
 
Dada huyo kwenye picha ya profile yako ni wewe halisi au avatar?
Chonde chonde jicho lako lisikukoseshe
 
Yesu Kristo alipokuwa akizungumzia dalili za kuja kwake na za mwisho wa dunia, alisema maneno haya yenye uzito mkubwa: “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” (Mathayo 24:14)

Kwa karne nyingi, wainjilisti wamekuwa wakipeleka Injili katika maeneo mbalimbali ya dunia, kwa miguu, kwa baiskeli, au kwa redio na magazeti. Hata hivyo, njia hizo hazijaweza kuyafikia mataifa yote. Lakini leo, tunashuhudia jambo la ajabu: AI (Artificial Intelligence) imekuwa chombo kipya kinachofanya unabii huo wa Yesu utimie kwa kasi isiyokuwa ya kawaida.

Kwa kutumia AI, injili sasa inatafsiriwa kwa mamia ya lugha ndani ya muda mfupi. Video, maandiko, na mafundisho ya Biblia yanayotolewa kwa lugha moja, yanatafsiriwa papo hapo na kufikia makabila na mataifa ambayo zamani ilikuwa vigumu kuyafikia.

AI inatumika kueneza injili kupitia YouTube, WhatsApp, Facebook, TikTok na mitandao mingine. Algorithm za AI zinasaidia kusambaza ujumbe wa Neno la Mungu kwa watu wengi zaidi na kwa muda mfupi mno. Wale ambao hawajawahi kwenda kanisani, leo wanapata mahubiri kwenye simu zao.

Wahubiri wengi sasa wanatumia AI kuandaa mafundisho, kurahisisha tafsiri za maandiko, na hata kusambaza nyimbo tam tam za Injili zenye ubora wa hali ya juu. Kwa njia hii, kazi ya injili imekuwa nyepesi, yenye kasi, na yenye matokeo makubwa.

Leo hakuna taifa linaloweza kusema halijasikia habari njema. Kwa AI, ujumbe wa Kristo umepelekwa hadi katika vijiji vya mbali kupitia simu janja na redio za mtandaoni, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, kwamba Yesu ndiye njia, kweli, na uzima.

Utabiri wa Yesu katika Mathayo 24:14 kwamba injili itahubiriwa katika ulimwenguni wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, sasa unaonekana kwa macho yetu ukitimia kupitia teknolojia ya AI. Ulimwengu mzima unashuhudia kasi ya upelekaji wa Neno la Mungu kwa njia ambayo haijawahi kutokea katika historia ya mwanadamu.

Hii ni ishara tosha kwamba mwisho wa dunia umekaribia. Karibu Yesu atakuja kuwanyakua wote wanaomwamini. Je, umejiandaa kumpokea Bwana Yesu Kristo atakaporudi?
View attachment 3446647
An AI-generated gospel song☝️ Tazama pia jinsi AI inavyoeneza Injili katika posts #22 na #25
Kila teknolojia ikivumbuliwa mnasema hii ndio ile iliyosemwa kwenye Biblia. Huyu ndiye namba 666, hii ndiyo mpinga Kristo miaka inapita, kinavumbuliwa kingine same story zinaibuka.
Dunia inaendelea tu aluta continua
 
Haleluya, nimezinduka na asante sana
Chukua hatua nyingine muhimu: Tubu dhambi zako, mwamini Yesu, na umpokee moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako.
 
Swala la kunyakuliwa kwenda mbinguni hapana halipo hivyo!

Mwisho wa dunia ni mwisho wa uovu ,kisha Dunia itaumbwa upya .Watu wema wataebdelea kuishi humu humu duniani
Acha mzaha. Yesu yuaja upesi( Ufu 22:10-12)
 
Usipokwenda kanisani utawezaje kushiriki chakula cha Bwana? Utawezaje kujengwa na wenye karama za Roho Mtakatifu usipokwenda kanisani? Faida za kwenda kanisani ni nyingi sana, nashangaa huzijui.

Huu uzi niliuandika zamani labda utakusaidia kuelewa faida nyingine za kwenda kanisani. Ila ni wa kimombo!👇
Soma soma soma . Chakula cha Bwana siyo kwenda kanisani. Chakula cha Bwana ni tofauti na mambo ya kwenda kanisani ndiyo maana hata wakati wa Yesu mwenyewe hakuna mkristo akiye kula chakula cha Bwana hekaluni wala sinagogini ...bali wslilia nyumbani tu
 
 
Back
Top Bottom