Pitia hapa huenda utanikumbuka

Mkuu mm nataka niwe msomi mwenye hela, nimeaza kujenga nyumba bila mkopo kwa mwaka mmoja sikuwa hata na kiwanja
 
Ili twende sawa lazima tudefine mafanikio tunayapimaje,kwa parameter zipi, Pili tudefine msomi ni nani,Je ni graduate wa primary,secondary, high school, diploma, degree,master au PhD?
Alafu tunasahau kwamba Mifumo yote ya kibiashara na kisiasa inawategemea wasomi.Huwezi kujua maana ya kuwa msomi ukiwa Tz,mahali ambapo hata compensation siyo commensurate na qualifications!Nenda kwa wenzetu,pata MBA ya prestigious college,utajua maana ya kuwa msomi.Kwa ufupi wanaondoka Dunia ni wasomi,hata uwe na Fedha utawatafuta.By the way,fikiria wamiliki wa makampuni makubwa duniani,tunawaita investors au Wenye Hisa,hata kama Kampuni ina hasara,wale managers lazima utawalipa.Waulize hao unaowaita matajiri pesa yao inakwenda wapi,hata kama una majumba mengi, at most unalala room 1!!Nawashauri wasomi wawe pia investors,wasitegemee chanzo kimoja tu cha mapato kama wameajiriwa.Pia waepuke kuingia mtego wa Kupata mapato ya Ufisadi!
 
Ni fact na mwisho ulivocoment kama pastor kurya wa Churchill anaesema waumini wanataka kwenda mbinguni wakati hata yeye hana haraka ya kwenda
Mkuu unahiyo clip? Nimeimiss sana
 
Umesema kweli. Walioelimika wakiamua kujiajiri huwa wanafanya wonders
 
Nilikiwa nafikiria kuendelea na M.A sasa hapo mmeniogopesha
 
Daaah! kila nikimuangalia MD wangu sijui kama hata form four alimaliza but he run the big company east and southern Africa,ameajiri hizo Phd,masters,degree kibao anazituma kama mbuzi na kunyenyekewa juu.huwa nawaza sana elimu kubwa kugeuka kuwa mtumwa wa elimu ndogo
 
Ni kama umetusimamnga vile!!!!!......lakini kuna ukweli mchungu kwenye maneno yako.Kusoma siyo vibaya lakini elimu isiyoweza kutukomboa kwenye umaskini ,elimu hiyo inakosa maana.

Kuwa na maarifa yanayotukomboa katika hali duni hiyo ndo elimu inayohitajika na sisi sote.

Sent from my TECNO R7 using JamiiForums mobile app
 
Tunasoma sababu Jamii inahitaji huduma za kitaaluma zaidi,ila km unasoma uwe tajiri haitotokea.

Jamii inamuhitaji mwalim,muuguzi,askari,mwanasiasa n.k hv vyote ni lazma usome,na sio kwa lengo la kuwa tajiri,ni wito mtu anakuwa nao hvo husomea ili akahudumu jamiii.

Wote tukihitajj pesa sidhani kama jamii itasimama,Mwenye uwezo wa kuihangaikia pesa na afanye hvo na wenye wito wa kuwahudumia wanajamii katika maisha yao ya kila siku nao pia wafanye hvo...

Ila shule hakuna pesa na primary goal ya shule sio kukufanya tajiri...SOMENI JAMII INAWAHITAJI.
 

Wote tunahitaji pesa, awe mwalimu, daktari, polisi, mkulima, Mfanyabiashara. Kila mtu aliyepo kwenye nafasi flani katika jamii anahitaji pesa. Kama hana uhitaji mwambie atoe huduma hiyo bure. Tusijidanganye, each person needs goodlife; and having money is a way to goodlife.
 
Money is power....

Rich people have money,
Poor people have faith,

The goals is to live rich,
Not to be a rich.
 
Shikamooni mlio maliza chuo.
Sisi tulioishia form 4.
Washatubangaize mtaani
Na serikali ya jpm.
 
Uko sahihi lakini hata achambuzi huu wa njia ya mafanikio umeletwa na msomi.
 
Kwa kuongezea pia watu waliosoma wengi wana tendency ya kutaka kulinda status, wanataka waonekane wao zinazowafaa ni kazi sa ofisini tu.
Nitauzaje juice watu watanicheka, ntakuwaje mkulima na hii degree yangu n.k n.k
Siku mtu akiacha hii mentality ndipo anatoka kimaisha. Mimi imenichukua miaka zaidi ya minne kuondoa hii kitu kichwani mwangu.
 
Hapa ndipo tatizo la Waafrika lilipo. Elimu hii tumeletewa na wazungu na hata lengo lake hatulijui. Hata hivyo nijuavyo mimi lengo la elimu hii siyo KUMTAJIRISHA aipataye. Nitatoa mfano.

Siku ya kwanza nimeingia darasani Marekani nilikuwa na kiherehere cha kumuona profesa angalau kwa sura kwani alikuwa ni profesa anayejulikana kimataifa na vitabu na nadharia zake ndizo tulifundishwa pale Mlimani. Kuja kumuona profesa mwenyewe simple sana. Baadaye akaandaa dinner ya Idara na International students wote tukaalikwa. Kwenda nyumbani kwake loh! Prof. anaishi kwenye nyumba ya kawaida tu na anakuja chuoni kwa baiskeli na wakati mwingine pikipiki.

Baadaye ndipo nikagundua kuhusu siri ya hawa wenzetu. They take their jobs seriously na profesa kazi yake hasa ni kufanya utafiti, kunoa akili za kizazi kipya na kuchapisha mawazo yake katika vitabu na majarida. Na jamii inamheshimu na kumuenzi kwa kazi hiyo. Japo hawalipwi mishahara mikubwa lakini wana hadhi na wanaheshimika sana. Yaani unakuta profesa anaongoza kitengo kinachosimamia Optics kwenye Hubble telescope au Mars Lander huko NASA lakini anaendesha baiskeli.

Kutokana na kumakinikia kazi hizi za kitaaluma ndiyo unakuta ugunduzi mwingi wa kinadharia na kivitendo unafanyikia huko. Hata Nobel prize winner utamkuta yupo ofisini mpaka usiku anahenya. Akitoka hapo anaingia kwenye Corolla yake na kwenda home saa nne usiku.

Sasa sisi elimu hii tumeivika jukumu ambalo silo lake. Matokeo yake ni vurugu tupu. Wasomi wetu, badala ya kukomaa kuandaa kizazi kijacho na kuchapisha mawazo yao, wanaogopa kuchekwa na jamii na matokeo yake kila mmoja yuko bize kusaka utajiri ndiyo maana wote wanakimbilia kwenye siasa au vyeo vingine huko serikalini wakaibe. Hata biashara wanaona watachelewa. Hata huko kwenye siasa nako mchango wao hatuuoni kwa sababu lengo lao ni kutajirika ili wasichekwe na jamii. Matokeo yake wasomi wetu wengi hawana mchango wote wa maana katika jamii. Sijui hata ni nani wa kulaumiwa.

Ukifuatilia ugunduzi mwingi utakuta watu walihenya miaka na miaka laboratory na kwingineko na mara nyingi ni life long process. Kama una mawazo ya kutajirika aisee huwezi kugundua cho chote. Ndiyo maana tuna wasomi wazuri sana lakini hata kimashine kidogo cha kumsaidia mkulima shambani hawawezi kutengeneza. Hawana muda na kila mtu anawaza kutajirika.

Mpaka pale tutakapoiheshimu elimu na kuiacha ifanye kazi yake inayotakiwa, Waafrika tutaendelea kuzalisha wasomi wasio na faida kwetu leo, kesho na kesho kutwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…