Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu unahiyo clip? Nimeimiss sanaNi fact na mwisho ulivocoment kama pastor kurya wa Churchill anaesema waumini wanataka kwenda mbinguni wakati hata yeye hana haraka ya kwenda
Umesema kweli. Walioelimika wakiamua kujiajiri huwa wanafanya wondersmachache ya kweli; kuna tofauti ya utajiri na mafanikio. Wasomi wamefanikiwa japo si matajiri lakini pia wengine wao hupata utajiri. Huwezi linganisha msomi na asiyesoma kwa mafaniko hasa ukijua maana ya shule. Unajua mwenye cheti ni msomi? Lakini eaomi wanatofautiana kuna wale wa diploma, bachelor, masters na PhD lskini wote wasomi hao
Tunasoma sababu Jamii inahitaji huduma za kitaaluma zaidi,ila km unasoma uwe tajiri haitotokea.
Jamii inamuhitaji mwalim,muuguzi,askari,mwanasiasa n.k hv vyote ni lazma usome,na sio kwa lengo la kuwa tajiri,ni wito mtu anakuwa nao hvo husomea ili akahudumu jamiii.
Wote tukihitajj pesa sidhani kama jamii itasimama,Mwenye uwezo wa kuihangaikia pesa na afanye hvo na wenye wito wa kuwahudumia wanajamii katika maisha yao ya kila siku nao pia wafanye hvo...
Ila shule hakuna pesa na primary goal ya shule sio kukufanya tajiri...SOMENI JAMII INAWAHITAJI.
Uko sahihi lakini hata achambuzi huu wa njia ya mafanikio umeletwa na msomi.MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI
✍Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.
[emoji117]Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa
[emoji144][emoji432] Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi [emoji537] na [emoji594] [emoji592]magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)
[emoji117]Wapo [emoji144][emoji432]wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana
[emoji117]Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga
Hii inachangiwa na mambo mawili:-
[emoji116]
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli
[emoji117]Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio
[emoji117]Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!
[emoji144][emoji432]Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
[emoji116]
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!
[emoji117]Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.
[emoji113]Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!
Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani
Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti
[emoji41]Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze
[emoji3][emoji120] Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze
....hata mimi sijawa tajiri bado[emoji12][emoji3][emoji3][emoji3][emoji115]