Pitia hapa huenda utanikumbuka

ni kweli lakini pia utajiri ni siri ya mtu mbona hakuna rais wa darasa la saba? pia hii hali ya kutokusoma na kufanikiwa inafanya kazi zaidi kwa nchi zilizoendelea
 
tanzania matajiri wengi ni viongozi pamoja na watoto wao mnaosema hawakusoma sana pia na watu wanaofanya biashara haramu vinginevyo utapotosha watu wasisiome
 
Ni kweli na pia watu wanapaswa kufahamu kuwa kuna AKILI inayotokana na elimu na kuna akili inayotokana na KIPAWA yaani TALENT sasa katika uhalisia mara nyingi mafanikio na hata utajiri huwaendea watu wenye Vipawa,na kipawa ni namna ya karama "GIFT" na mtu huzaliwa nacho kama majaaliwa . Sasa hata kama mtu ana elimu ya kiwango gani ikiwa hana kipawa ni vigumu kwake kufanikisha majukumu kwa ufanisi ili kuleta maendeleo. Mtu anaweza akawa na shahada (elimu) ya business administration lakini akawa hana hata uwezo wa kubuni au kuendesha biashara ya kiosk cha kuuza voucher za simu tu, lakini mwingine akawa hana elimu yoyote ya shule na bado akaweza kufanya biashara kubwa kupitia kipawa. Mafanikio ya hali ya juu huja pale mtu anapokua na vyote viwili mfano unakuta katika kundi la madaktari wasomi wa ngazi inayofanana kati yao mwenye kipawa atakuwa daktari bingwa au katikati ya majaji miongoni mwao mwenye kipawa lazima atakuwa kiongozi nk. Katika msahafu (Bible) kuna nukuu inayosema "...kipawa alichonacho mtu kitamfanyia nafasi" hii ikiwa na maana kuwa kipawa alichonacho mtu kitamtengenezea fursa, na pia nukuu nyingine inasema " kipawa cha mtu kitamketisha na wakuu" ndio maana unakuta Mrisho Mpoto ameishaonja MEALS za ikulu ukilinganisha na maelfu ya maprofesa ambao hata mlango wa Ikulu hawaujui rangi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…