Pitia hapa huenda utanikumbuka

Pitia hapa huenda utanikumbuka

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

[emoji117]Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

[emoji144][emoji432] Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi [emoji537] na [emoji594] [emoji592]magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

[emoji117]Wapo [emoji144][emoji432]wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

[emoji117]Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
[emoji116]
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

[emoji117]Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

[emoji117]Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

[emoji144][emoji432]Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
[emoji116]
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

[emoji117]Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

[emoji113]Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

[emoji41]Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

[emoji3][emoji120] Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze
....hata mimi sijawa tajiri bado[emoji12][emoji3][emoji3][emoji3][emoji115]
Hahahahah siri ya pesa anaijua mwenye nayo , km unabishi mbona wewe na hata huyo tajiri mnahangaika kuwapeleka watoto wenu elimu za juu , do you know who owns the world money?? Kuna mambo wanafanya wasio na elimu ambayo educated can't do
 
Mkuu huu ndo ukweli unaotutesa. Binafsi nimeamua mwaka huu wa 2017 kuanzia January ya leo naingia mtaani kwa asilimia 100. Nimekuwa muajiriwa kwa miaka 3 sasa ila nimeona huko niendako ni giza zaidi. Nitakuja hapa December kwa neema ya Mungu kushuhudia yale nitakayokuwa nimekutana nayo.
utupe mrejesho
 
Mkuu huu ndo ukweli unaotutesa. Binafsi nimeamua mwaka huu wa 2017 kuanzia January ya leo naingia mtaani kwa asilimia 100. Nimekuwa muajiriwa kwa miaka 3 sasa ila nimeona huko niendako ni giza zaidi. Nitakuja hapa December kwa neema ya Mungu kushuhudia yale nitakayokuwa nimekutana nayo.
Kila la heri mkuu, mi hayo nilishayafanya miaka 4 iliyopita, ukifanikiwa utajilaumu siku zote kwanini ulipoteza muda wako, mi inafika time huwa nalaumu kwanini nilisoma miaka mingi sana.
 
Hii ni kweli wasomi wengi wakitaka kuanzisha biashara huwaza kwanza hasara na baadae faida kubwa kwa muda mfupi. Na wengi sana wanakosa kitu uthubuti kwa kuhofia hasara. Mchana mwema wajasilia mali
 
Asante mwaka huu nitapiga hatua kwa lazima kwakua nina imani na nimepanga hivyo na Mungu yupo upande wangu. Kitu ambacho hutuangusha wasomi wengi ni kutaka kujifunza kuogelea Darasani. "Njia sahihi ya kujifunza kuogelea ni kuingoi kwenye maji kwanza" Na njia nzuri ya kutoka kimaisha ni kufanya Biashara either kulima au kufanya biashara yoyote ile.
 
Utakuta msomi anajivuna kumiliki kitabu cha :-
HOW TO BE REACH MAN
HOW TO GET MONEY EASY
HOW TO BE SUCCESFULL
HOW TO ESCAPE POVERTY
Na majitabu mengine kibao....!!!!! Wakati ki uchumi anamiliki house girl tu nyumbani alikopanga.
[emoji16][emoji16][emoji16] mbavu zangu
 
Utakuta msomi anajivuna kumiliki kitabu cha :-
HOW TO BE REACH MAN
HOW TO GET MONEY EASY
HOW TO BE SUCCESFULL
HOW TO ESCAPE POVERTY
Na majitabu mengine kibao....!!!!! Wakati ki uchumi anamiliki house girl tu nyumbani alikopanga.
Hahahaha mkuu umeua.

Umesema ukweli kabisa
 
machache ya kweli; kuna tofauti ya utajiri na mafanikio. Wasomi wamefanikiwa japo si matajiri lakini pia wengine wao hupata utajiri. Huwezi linganisha msomi na asiyesoma kwa mafaniko hasa ukijua maana ya shule. Unajua mwenye cheti ni msomi? Lakini eaomi wanatofautiana kuna wale wa diploma, bachelor, masters na PhD lskini wote wasomi hao
 
machache ya kweli; kuna tofauti ya utajiri na mafanikio. Wasomi wamefanikiwa japo si matajiri lakini pia wengine wao hupata utajiri. Huwezi linganisha msomi na asiyesoma kwa mafaniko hasa ukijua maana ya shule. Unajua mwenye cheti ni msomi? Lakini eaomi wanatofautiana kuna wale wa diploma, bachelor, masters na PhD lskini wote wasomi hao
Piga ua garagaza swala zima huku duniani ni PESA tantalila za kusoma ni kupoteza muda,ingewezekana mtu anaejiongeza kichwani ni bola akaishia kidato cha sita au cha nne then akaja mtaa kwa mtaa kusaka pesa,ndivyo navyowajenga hata watoto wangu
 
Back
Top Bottom