Pitia hapa huenda utanikumbuka

Pitia hapa huenda utanikumbuka

Ni kweli wasomi wengi sio matajiri ila mfumo wa elimu yetu nao unachangia asilimia kubwa ya mitaala ya kibongo inakuandaa kuja kuajiriwa na sio kijiajiri.
Mfumo wetu unatoa elimu ...
Mtaani kinachohitajika ni maarifa ... sio elimu.
 
Ni kweli wasomi wengi sio matajiri ila mfumo wa elimu yetu nao unachangia asilimia kubwa ya mitaala ya kibongo inakuandaa kuja kuajiriwa na sio kijiajiri.

Tatizo siyo bongo,dunia nzima wanaokariri badala ya kufikiri wenyewe huwa kama maelezo ya mtoa mada.
 
Ni kweli wasomi wengi sio matajiri ila mfumo wa elimu yetu nao unachangia asilimia kubwa ya mitaala ya kibongo inakuandaa kuja kuajiriwa na sio kijiajiri.
SI MFUMO WA ELIMU TU! NA WAO HAWAJIONGEZI MKUU
 
Asante mwaka huu nitapiga hatua kwa lazima kwakua nina imani na nimepanga hivyo na Mungu yupo upande wangu. Kitu ambacho hutuangusha wasomi wengi ni kutaka kujifunza kuogelea Darasani. "Njia sahihi ya kujifunza kuogelea ni kuingoi kwenye maji kwanza" Na njia nzuri ya kutoka kimaisha ni kufanya Biashara either kulima au kufanya biashara yoyote ile.

Nimekuelewa.
 
MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

[emoji117]Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

[emoji144][emoji432] Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi [emoji537] na [emoji594] [emoji592]magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

[emoji117]Wapo [emoji144][emoji432]wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

[emoji117]Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
[emoji116]
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

[emoji117]Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

[emoji117]Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

[emoji144][emoji432]Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
[emoji116]
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

[emoji117]Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

[emoji113]Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

[emoji41]Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

[emoji3][emoji120] Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze
....hata mimi sijawa tajiri bado[emoji12][emoji3][emoji3][emoji3][emoji115]

Hasa Tanzania hakuna wasomi wote ni wakremishaji bora maisha yaende
 
Nimekuelewa sana
Tusiogope kukosea & ni vizuri kukosea kwa sababu utakachojifunza kwenye hilo kosa ndicho kitakacho kupigisha hatua zingine mbele, na tusiwe waoga wa kuthubutu kufanya mambo ambayo tunahisi yataleta alama chanya kwenye maisha yetu
 
Si wanasemaga ukitaka kumficha kitu mbongo weka kwenye maandishi
Ni jambo linalosikitisha sana. Imagine analalamikia page mbili kuwa ni ndefu. Je, huyo ataweza kujisomea mwenyewe kitabu kidogo cha 200pp? Je, huyo anaweza kujinunulia kitabu ajisomee? Je, huyo ataweza kununua magazeti yenye makala ndefu? No wonder reasoning ya wasomi walio wengi hapa Bongo iko chini!!! Very sad kwa wasomi wa jinsi hii
 
Hoja yako nini sasa? Kwani unatafsiri gani kuhusu MAFANIKIO?

Nijuavyo ni kwamba maisha yanakuwa na maana pale unaporimiza malengo yako uliyojiwekea na hayo ndio mafanikio yenyewe, pesa inaweza kuwa ni sehemu ya mafanikio na sio mafanikio yenyewe wala haimaanishi kwamba wenye pesa ndio wenye furaha na amani. Jitambue.
 
Ni jambo linalosikitisha sana. Imagine analalamikia page mbili kuwa ni ndefu. Je, huyo ataweza kujisomea mwenyewe kitabu kidogo cha 200pp? Je, huyo anaweza kujinunulia kitabu ajisomee? Je, huyo ataweza kununua magazeti yenye makala ndefu? No wonder reasoning ya wasomi walio wengi hapa Bongo iko chini!!! Very sad kwa wasomi wa jinsi hii
Kweli mkuu kusoma kunahitaji kipaji. Mi mwenyewe nilikuwa sipendi kusoma vitabu. Ila kama muujiza hivi nilivyoanza kusoma Rich Dad Poor Dad, nikakiprint kabisa nikawa nakisoma kwenye basi. Nikakimaliza na nikadownload vingine vya Kiyosaki kama 7 nikavisoma. Kiukweli it was my turning point. Nilipenda kusoma vitabu tangia hapo.
 
Kweli mkuu kusoma kunahitaji kipaji. Mi mwenyewe nilikuwa sipendi kusoma vitabu. Ila kama muujiza hivi nilivyoanza kusoma Rich Dad Poor Dad, nikakiprint kabisa nikawa nakisoma kwenye basi. Nikakimaliza na nikadownload vingine vya Kiyosaki kama 7 nikavisoma. Kiukweli it was my turning point. Nilipenda kusoma vitabu tangia hapo.
Asante na hongera sana kwa kuchukua hatua. Wavuvi wa kusoma vitabu wako wengi. Binafsi kusoma vitabu ni utamaduni nilioujenga nikiwa na miaka 15, katika umri huo ndipo niliponunua gazeti langu kwa hela yangu niliyotafuta mwenyewe. Nafurahia kusoma, imagine mtu anacomplain 2pp kuwa ni ndefu. Mwaka huu nimepanga nisome walau vitabu 12 kila mwezi kitabu 1.
 
Kujisomea kwetu tukuambatanishe na malengo tunayotaka kuyafikia. Tusome kupata maarifa na mbinu za kuyafikia malengo yetu. Mambo ya copy na paste yametugharimu sana. Mwaka huu tufanye mambo mapya yenye manufaa kwa familia, Jamii na taifa
 
Back
Top Bottom