Plasduce Mbossa atakuwa kaliona kosa la Eric Hamissi

Plasduce Mbossa atakuwa kaliona kosa la Eric Hamissi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Ukipewa madaraka tegemea siku inakuja utatenguliwa, Ukifurahia picha ya pamoja pale ikulu ukiwa na familia yako pembeni ya Rais jua kuna siku hao hao watakuliwaza jioni baada ya barua yako kusambazwa mtandaoni.

Hiyo ni tamu na shubiri ya madaraka kukasimiwa kwa mtu. Eric Hamis ni kama hakujua kuwa yupo katika probation period ya miezi sita, japokuwa imeongezeka kidogo. Ni kama alisahau kuwa yupo katika muda wa uangalizi wa Rais SSH.

Akaanza ule ukaribu na wanasiasa. Kila mbunge akisimama anamtaja na kumsifia, nini siri ya sifa hizi za waheshimiwa wabunge?. Hii ni mada ndefu sana inayojitegemea.

Sasa kaka Plasduce kapewa koti lile lile lililomshinda Kaka Eric. Labda atakuwa kajifunza maana ya kufanya kazi zaidi na kuepuka sifa za kutajwatajwa na vyombo va habari.

CEO mzuri ni yule anayesifiwa na kiongozi wake baada ya kuonyesha ubunifu wake, Sio yule anayezitafuta sifa kwa nguvu za chini ya kapeti. Kaka Eric atakuwa kajifunza mengi sana pale TPA.

Wapo wenye hoja ya CEO wa bandari kuwa ni mchumi mwenye shule pana ya uchumi na uzoefu mpana wa kibiashara. Sioni kama ni kosa iwapo SSH ataamua kuwaamini hawa mabilionea tulionao wakamshauri ni nani akawa CEO wa bandari katika dunia ya sasa ambayo afrika ni kimbilio la mabepari, katika dunia ambayo reli za kisasa zinajengwa na zinategemewa kuanza kurudisha pesa ya mkopo iliyotumika kuzijenga.

Hakuna ubaya kama SSH akavunja taratibu zilizozoeleka serikalini akaja na team ya watu wenye uzoefu wa uendeshaji na wasiojiona kama vile wanalo deni kwa wanasiasa maslahi kama tulionao kwa sasa.

Ni maoni tu.
 
Back
Top Bottom