Plate namba za magari zinavyokimbia hivi ni kweli vyuma vimekaza ?

Mkuu aidha Ww ni mgeni kwenye magari au huna utafiti,namba A na B zilikimbia haraka kutokana na pikipiki na Bajaji zilikuwa zinatumia usajili mmoja na gari.
Kwamba namba D imekimbia sio kweli,ina zaidi ya miaka 7 ipo tu

Achana nae....ni mwana Lumumba huyo!
 
Mimi nina maoni tofauti kidogo naona gari hazinunuliwi namna hiyo!!

Namba D tangu mwanzoni mwa 2015 mpaka leo bado ipo jamani!?? Bado tunasema watu wananunua magari kwa wingi! ?

Hebu wenye nazo muongeze Spid ya kununua magari tumtokomeze huyu Namba D ameshaanza kuwa Mugabe sasa!!!
 
Watanzania walio wengi tunanunua magari used,Sasa hapo lazima namba zikimbie maana ndani ya miaka 3 gari imeshaanza kuchakaa.......
Ushaona dampo la magari yaliyochakaa eneo lako?
Mpaka sasa namba A zipo barabarani
 
Unajua Alferbet moja mpaka iishe yanakuwa yamesajiliwa magari mangapi ya aina moja?
Plus magari yote?
 
Dk ni Plate number za mwaka 2017 miezi ya 8 mpaka 10 hvi mkuu.
Hakuna ukweli kuhusu hili, awamu hii kasi ya ununuzi magari imepungua. Namba inayoanzia D imekaa muda mrefu sana. Kama sikosei JK aliacha DK..
 
nadhani kukaaza au kutokokaza,matokeo yake yapo kwa mtu mmoja mmoja.kuna wanafurai na mambo yao yanaenda ila kuna wanaoteseka mambo yamegoma.binafsi naona maisha yangu niyale yale,ila labda nimeongeza saving zaidi ya spending.
 
Hakuna ukweli kuhusu hili, awamu hii kasi ya ununuzi magari imepungua. Namba inayoanzia D imekaa muda mrefu sana. Kama sikosei JK aliacha DK..
Hii hali imetokea baada ya kutenganisha usajili wa pikipiki na magar tofauti na kipindi cha jk mkuu
 
Mikopo nayo ni source ya kipato kwa mtu.
 
Pikipiki bada ya kuondolewa kwenye mfumo wa number za magari imesababisha number zisikimbie sana. Sasa hivi ungekuta tupo G. Pikipiki zilikimbiza sana number.
Hakuna ukweli kuhusu hili, awamu hii kasi ya ununuzi magari imepungua. Namba inayoanzia D imekaa muda mrefu sana. Kama sikosei JK aliacha DK..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…