Platform ya kuuza na kununua muziki wasafidotcom tayari kwa matumizi

Unazunguka alafu unarudi pale pale nilipoanzia.Yaani Universal wakubali kumlipia mtu bilioni 2 alafu wamuache kirahisi rahisi aendelee kuingiza hela kwenye kitu ambacho wao wamekilipia?!

East Africa ndio soko kuu la Diamond unadhani Universal wasipopata faida huku watauza wapi tena kazi za Dimond kwa faida?!

Alisema kuwa kazi za Wcb zitasambazwa na Universal music au hakusema?!

Hakusema kuwa walilipwa bilioni mbili kwa ajili hiyo au hakusema?!

Unakumbuka kuwa Marry you ilivyotoka ilisambazwa vipi?!

Nini kilichobadilika sasa hivi?!
 
Umesema kitu kikubwa mno mkuu.

Hiyo ni sawa kwa mchezaji kusajiliwa man u kwa mabilioni alafu aachwe akacheze ndondo.

Iko wazi hapa kuna ujanja ujanja Dimond akishirikiana na Universal unataka kufanyika.
 
Yule jamaa wa kuitwa Beka Boy Youtube wamemfungia account yake, pale ilikuwa unadowload nyimbo zote bure.
 
Mbona wazaramo wengine waelewa,Yaani mambo madogo kama aya unataka kila muda uambiwe buana.Chunguza kwanza system nzima ya uuzaji wa muziki.Elewa wasafidotcom sio platform ya kuuza kazi za mondi tu bali msanii yoyote kwa ivo universal wanaeza kuitumia wasafidotcom kusambaza kazi za WCB.Kama hujaelewa kaangalie NgazkwaNgaz au kakojoe ulae tunaoelewa tujadili.
 
Umekuja kwenye point kuu.

Kwa hiyo Universal music wanafanya kazi pamoja na Wasafi.com au Haya ni mawazo yako binafsi tu?!

Hilo
 
Mbona unahangaika sana ndugu..!?
 
Yaaani Diamond bado anaendelea kuonesha Kuwa yeye ni msanii wa kimataifa! Hiki kitu ni amebuni kitu kikubwa sanaaa na wasanii wengine hawana Budi kumuunga mkono! Kwasababu kwa Afrik ameshatoboa Means wasanii wengi wataweka nyimbo zao huko! Kama wimbo mmoj ni sh 300 assume watu millioni 1 wakanunua huo wimbo 1 means ni 300×1000000=30,000,0000 Hapo msanii lazima Atajirike!! Hii ni akili kubwa sanaaa na Msurur wa watu wanao enda OFISI ZA WCB ni ishara tosha kuwa mwitikio ni mkubwaaa hi nzuro sanaaa

Kuwa chini ya Label fulani haimanishi wewe utashindwa kufanya kitu kinginee!!! Diamond yupo chini ya Universal Music Group lakini haimanishi yeye ashindwe kufanya menginee hii tunaita akili kubwa

Ushauri wangu kwa Diamond ni kuwa Hiyo website yake iwe ya Kimataifa kweli ya Iwe updated sio wimbo unatoka leo hadi masaa 3 haupatiki kwenyw hyo website hapanaaa wimbo unaachiwa wakato tayari upo KWA WEBSITE....

Pili asije akawacheweleshea malipo wasanii wenye kazi zao huko au akawazungusha au wakashindwana katika malipo yaani iwe kizunguz kweli mtu apewe haki yake anayostahili na kwa wakatii mtu kama hana uwezo wa kuelewa mkataba ni bor asimpokeee hapo Uswahili aweke pembeni asije letewa shida na aibu bure hapo ni anacheza na nguvu za watu na hela za watu awe makini sanaaaa katika Malipooo ya kazi za watuuu asiwe mnyonyaji wala mnyonywaji!!!

Nampenda Diamond ila awe makini sanaa kwenye Suala la malipo ya kazi za watuuu

Chonde chonde Diamond my Brother Usichezee na Malipo ya kazi za watuu TENDA HAKII vinginevyooo issue iko poa sanaaa
 
Umekuja kwenye point kuu.

Kwa hiyo Universal music wanafanya kazi pamoja na Wasafi.com au Haya ni mawazo yako binafsi tu?!

Hilo
Ndio ivo.Jamaa anapiga ela twice,Kama mmiliki wa platform lakini pia muuzaji yaani msanii.
 
Ndio ivo.Jamaa anapiga ela twice,Kama mmiliki wa platform lakini pia muuzaji yaani msanii.
Diamond mjanja sana mf ata darasa akitoa ngoma kali akaweka pale wasafi diamond anakula zake na darasa zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…