Platinum Credit ni kampuni yenye huduma mbovu na zisizofaa. Walimu tunakopa kwa sababu ya shida tu.

Chama chenu Cha waalimu sijui kipo kwa ajili ya nini! Naona wanufaika ni viongozi tu ndio maana hata teuzi wanazigomea,akiwasaidii chochote kuwalinda.
 
Ukimuona mtu anaenda kukopa kwenye hizo taasisi za kifedha zenye riba kubwa kupitiliza, badala ya benki! Tambua fika huyo mtu ana upungufu wa akili kichwani.

Kwanza siku hizi watumishi wamerahisishiwa sana njia ya kukopa kupitia E Loan! Na benki zote zinajitokeza ukiingia kwenye huo mfumo, na pia riba zimewekwa! Sasa huko Platinum, Bayport, Maboto, sijui Fanikiwa, nk. Mnafuta nini tena, kama siyo uwendawazimu huu!!
 
Walimu wengi hawana elimu juu ya matumizi ya fedha, mikopo na masuala yote ya fedha ndio maana wanaishia kukopa sehemu kama Platnum credit.

Unakopa laki 1 unalipa laki 4 ninishara kwamba huna ufahamu wowote juu ya elimu ya fedha.
 
Shida zimetuzidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…