Playing with FIRE. . . .

Playing with FIRE. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Cheating is like playing with fire, yani someone is bound to.get burnt at some point or another.

Waweza jikuta unapoteza ndoa yako, watoto, heshima kama uliwahi kuwa nayo,mali, kiungo/viungo au hata maisha.

Wale/nyie vinara wakutoka nje ya ndoa na mahusiano yenu hivi hua mnafikiria na kujiandaa na haya??! Mmewahi kufikiria kua siku moja unaweza ukajikuta umepewa sumu, umepigwa mpaka kuvunjwa kiungo au hata kuchomwa kisu kisa kutembeza mwili wako kwa mtu/watu ambao wako nje ya mkataba/makubaliano ya mahusiano yako na mwenzi wako au kwa kuingilia mahusiano ya mtu mwingine?

Utajisikiaje ikitokea siku unajiona unakufa hivi hivi au unapoteza chochote kile ambacho umehangaika sana kukipata kisa tu ulishindwa kutulia na mwanaume/mwanamke wako?

Tulieni jamani, hivyo viungo vya mwili vitawaponza!!!!
 
Naona zile picha za tindikali zimekuogopesha kweli! Lol....meseji senti.
 
Watu wengi huwa hawatathmini madhara ya kile wanachokitenda. Ndio maana majuto huwa ni mjukuu badala ya mtoto!
 
Lolz. . . Leo sijui kama ntalala. . .
Sijui nimuombe desh desh tusijuane kabisa. . . ?
Mambo ya kuharibiwa kauso kangu au kupunguziwa siku za kuishi sitaki kabisa.
 
Watu wengi huwa hawatathmini madhara ya kile wanachokitenda. Ndio maana majuto huwa ni mjukuu badala ya mtoto!

Inabidi waanze kufikiria, sio wasubirie mpaka wakatwe hivyo viungo wanavyogawa hovyo ndo waanze kulia.
 
Lizzy wakishawaka tamaa huwa wanasahau kushirikisha ubongo juu ya impact yake, matokeo ndo majuto mjukuu...
 
Watu wana ujasiriamwili wa hali ya juu..Kuna jirani yangu nilimwambia mimi sio mtu wa kuchafua hekalu langu akanijibu:''forget about fidelity and all that ****,the motto is do not get caught''.Ana mke na watoto watano.
 
ya nini ujope tatizo la kuwaza hayo yote wakati siku hizi wanawake wanakupa utamu...wee ni hela yako tuu....dada poa!!!
 
Kikweli watu huwa hatuliifikirii hilo, kuna best yangu alikuwa anatembea na mume wa mtu wapo nyumba moja ya kupanga, kuna sku mke alifuma meseji,akaiba namba usiku akatoka nje kupiga ile namba na yule shost yangu pia alikuwa uko uko nje akapokea..... loooh kilichofuata best akutoka ndani wiki.
 
Watu wana ujasiriamwili wa hali ya juu..Kuna jirani yangu nilimwambia mimi sio mtu wa kuchafua hekalu langu akanijibu:''forget about fidelity and all that ****,the motto is do not get caught''.Ana mke na watoto watano.
Kaazi kweli kweli.

Watu wana hatari kweli. . .alitembezewa kichapo ehhhh?
 
Lizzy wakishawaka tamaa huwa wanasahau kushirikisha ubongo juu ya impact yake, matokeo ndo majuto mjukuu...
Too bad wengine hata huyo mjukuu wao Majuto hua hawapati muda wa kumuona.
 
Watu wana ujasiriamwili wa hali ya juu..Kuna jirani yangu nilimwambia mimi sio mtu wa kuchafua hekalu langu akanijibu:''forget about fidelity and all that ****,the motto is do not get caught''.Ana mke na watoto watano.
hmwatu wengine wamebanga....khaaa
 
kwa kweli sasa hivi cheating imepamba moto.
Mke wa mtu anacheat hadi anapata ujauzito, si ufa.la huu??
 
Wanafanya mchezo na maisha hao. . .ngoja waume zao na hao wanaowachukulia waume waanze kuwachana matumbo ndo watajua akili zao zilipo.
 
...lakini sio wakati wote CHEATING ni mbaya...unaweza ukashangaa imeimarisha mahusiano yenu.
lakini pia ni lazima tujiulize kwa nini CHEATING inakuwepo?
mm kwa ujumla naweza sema cheating ni matokeo ya kutokuridhika FULLY na partner ulie nae...kama kweli mnapendana na mnafurahia uhusiano wenu,kwa nn niende pembeni kutafta raha ingine ya dk 5?
nitacheat maana nahisi kuna kitu extra nje ya partner wangu!
so kiukweli watu hawaogopi matokeo ya kudanganya...wanachotaka ni kuridhisha nafsi zao japo kwa muda mfupi!
 
Basi wawe wanafikiria na kujiandaa kuridhisha nafsi za wenzao pale watakapokamatwa na kushikiwa kisu au panga.

Na wewe usieridhika na mwenzi wako siuhamie huko unakoridhishwa?
 
preparedness muhimu!..
home sweet home...siwezi kuhamia!...
 
Back
Top Bottom