Pleasa msaada mke wangu amezimia ghafla ni mjamzito

Pleasa msaada mke wangu amezimia ghafla ni mjamzito

Mpigie bodaboda aje mwende hospitali hapa jf wenzio wengi wanaokupa ilani wako jijini dar hawafahamu shida ya usafiri na usalama nyakati za usiku huko vijinini
 
Jamani wacha kuniona kama siko siriasi niko siriasi tena sana nimesema tatizo ni huduma za afya ziko mbali sana kwa wanajua niko bukoba sehemu ya rwanga kijijini usafiri hakuna kabla ya kesho kwenda hosptal kuna njia ya uduma ya kwanza nzuri nichukue kabla ya matibabu na vipimo?

Mshushie dua mkuu, hilo ndilo jambo la wepesi na linalowezekana kam utakuwa muumini na imani thabiti
 
Jamani wacha kuniona kama siko siriasi niko siriasi tena sana nimesema tatizo ni huduma za afya ziko mbali sana kwa wanajua niko bukoba sehemu ya rwanga kijijini usafiri hakuna kabla ya kesho kwenda hosptal kuna njia ya uduma ya kwanza nzuri nichukue kabla ya matibabu na vipimo?

Ndg. hukusema ni mjamzito wa miezi mingapi, ila naomba nikusaidie hivi:
Kama ni changa yaani kuanzia mwezi 1 hadi 4, anaweza kupatwa na hali hiyo haswa akisimama saana na haswa kama ni mimba ya kwanza.
Pili kama hujawahi kuona hivyo tena, achana na hayo maneno ya watu kuwa ni kifafa cha mimba. Haiko hivyo. Wamama wengi sana wana dalili za ajab ajab wakiwa na mimba haswa ya kwanza. Kama hana dalili za kuchoka sana, hajavimba miguu, hasikii kichwa kuuma, ngojea tu mpaka asubuhi umpeleke kliniki akapimwe.
Walio kwenye miundo mbinu mizuri ndo hao wanaokutukana na kukuita majina. Usiogope, sema na mkeo maneno mazuri wala usiogope na kufadhaika. Weye mtoto wa kiume, onesha pendo tu kwa mkeo na mwahidi kuwa kesho kukicha weye na yeye ni kiguu na njia mpaka mumwone dakitari.
Pole kwa mipasho ya humu jf. jikaze kiume usipanic kwa maneno ya watu
 
Mpigie bodaboda aje mwende hospitali hapa jf wenzio wengi wanaokupa ilani wako jijini dar hawafahamu shida ya usafiri na usalama nyakati za usiku huko vijinini

Ni kweli ndugu yangu ndo maana wananidhiaki sana ila nia yangu ni kuomba msaada na kuelimika ili muda mwingine nitawasaidia maana ni tatizo hapa kijijini. mazingra magumu sana miundo mbinu ni shida sana.
 
Umepata wapi nguvu za kuingia JF ?

Hebu changamka ufike hospital uokoe hao watu!
 
wewe ni dr wa mifugo?

ndiyo wewe huyu?..dah!

avatar18888_28.gif
 
Umepata wapi nguvu za kuingia JF ?

Hebu changamka ufike hospital uokoe hao watu!

he is not serious and he is not married as well.hivi mke anaumwa utakumbuka hata simu au laptop ilipo?na utume ujumbe uanze kusubiri replies?very nasty mind ni ----- hawa watoto
 
by Dr Shekilango;
Hapana siyo hivyo mkuu wala mie siyo mnafiki coz sasa ametulia kidogo alfu niko kijijini sana hakuna huduma za karibu no usafiri ndiyo sababu.

wewe Dr Shekilango sio Doktari???

Au Udokta wa mataputapu!
 
Last edited by a moderator:
Ndg. hukusema ni mjamzito wa miezi mingapi, ila naomba nikusaidie hivi:
Kama ni changa yaani kuanzia mwezi 1 hadi 4, anaweza kupatwa na hali hiyo haswa akisimama saana na haswa kama ni mimba ya kwanza.
Pili kama hujawahi kuona hivyo tena, achana na hayo maneno ya watu kuwa ni kifafa cha mimba. Haiko hivyo. Wamama wengi sana wana dalili za ajab ajab wakiwa na mimba haswa ya kwanza. Kama hana dalili za kuchoka sana, hajavimba miguu, hasikii kichwa kuuma, ngojea tu mpaka asubuhi umpeleke kliniki akapimwe.
Walio kwenye miundo mbinu mizuri ndo hao wanaokutukana na kukuita majina. Usiogope, sema na mkeo maneno mazuri wala usiogope na kufadhaika. Weye mtoto wa kiume, onesha pendo tu kwa mkeo na mwahidi kuwa kesho kukicha weye na yeye ni kiguu na njia mpaka mumwone dakitari.
Pole kwa mipasho ya humu jf. jikaze kiume usipanic kwa maneno ya watu

Kweli niseme Mumgu akujalie hekma na maarifa kwa msaada wako na kunipa mawazo ambayo yamenijenga sana, popote ulipo ulale salama sana.
 
Kweli niseme Mumgu akujalie hekma na maarifa kwa msaada wako na kunipa mawazo ambayo yamenijenga sana, popote ulipo ulale salama sana.

Aksante kama nimeweza hata kuurudisha moyo wako. Najua unaposema tatizo la kijijini. Ni rahisi kwa wanazi kutokukuelewa na kukuona huna mapenzi kwa mkeo.
Ila, asubuhi angalia hali yake ndo umkimbize kliniki. Kama akikuambia anajisikia vyema, na ni mara ya kwanza, shughuli alizofanya leo asiziendeleze. Akae akiwa amenyoosha miguu, alale akijisikia na umpe mapenzi zaidi yaani maneno mazuri ya kumtia moyo. Utashangaa atakavyo badilika. Usiogope. Usiku huu mkumbatie, shikashika na kumpapasa tumbo na uoneshe huna hofu yeyote. Hofu yako itammaliza
 
Wakati tukipata chakula cha jioni ghafla mke wangu niliona anaishiwa nguvu na kunilalia nikajiuliza sina cha kufanya. Kutoka na kuzimia niliamua kuanza kumpepea na baadaye amepata nafuu japo si sana, so kama wajamaa naomba mawazo, ushauri na hatua za kuchukua.

Pole na jitahidi uende hospitali muone daktari haraka iwezekanavyo,Nimewahi pata tatizo nikiwa na hali km hiyo,kw upande Wangu sukari na pressure ilikuwa chini ingawa sina kawaida ya kuwa na shida hizo.
 
Hii inanikumbusha katuni moja, mtu anazama badala watu wamuokoe wao wanapiga picha za kuweka facebook na instagram..
 
aisee, unatakiwa usim'banebane, mpe hewa ya kutosha, kama chumbani padogo kalaleni ata uwani......
 
Wakati tukipata chakula cha jioni ghafla mke wangu niliona anaishiwa nguvu na kunilalia nikajiuliza sina cha kufanya. Kutoka na kuzimia niliamua kuanza kumpepea na baadaye amepata nafuu japo si sana, so kama wajamaa naomba mawazo, ushauri na hatua za kuchukua.
Wewe Doctor Mzima unashindwa kumfanyia huduma ya kwanza mke wako? Au jina hilo la (Dr Shekilango)Doctor ni jina feki? Mkuu Dr Shekilango Muweke sehemu yenye upepo na mpe maji ya uvuguvugu glasi 1na kama unayo Asali weka kijiko 1 ndani ya hayo maji ya uvuguvugu na ikiwezekana asubuhi kukicha salama muwahishe Hospitali haraka iwezekanavyo huenda ana maradhi ya Presha.
 
Kupoteza fahamu kwa mjamzito kunatokana na sababu zaidi ya moja.

Na wakati mwingine Ukipuuzia Inaweza kumletea madhara makubwa sana mtoto alioko tumboni pamoja na Mama mwenyewe.

Nenda hospitali haraka sana akapimwe.

Na suala km hili unalipeleka kule JF DOCTOR sio humu kwa wahuni wanaojadili Ngono masaa 24.
teh teh teh maalim naona unautafuta ugomvi jamvini.
 
Umeniacha hoi hiyo time ya kuingia JF umeitoa wapi?? Yaani badala ya kumuwahisha mkeo kituo cha afya wewe unaingia JF sitaki kuamini kuwa hakuna transport huko kama network inashika Im sure Bodaboda zipo kabisa acha ujinga wewe nenda hosipital
 
Back
Top Bottom