Please Could You Be Honesty to Us?


Dah babu aksante

Hapo kwenye namba tatu hapo?? Babu hapooooo................. asiwe mpelelezi yaani dah kusema ukweli huwa ni pagumu sana kutekelezeka. Yaani we utoke kazini uende sehemu kushikana mkono na washkaji .....ukichelewa bibi asikupigie simu??

Lakini tuweni wakweli jamani hivi mnadhanigi wanawake wanawapigiaga simu au kuwasumbua bure?? kuna sababu zinazowafanya wafanye hiyo na moja wapo ni upendo.
1. Ukichelewa kurudi nitakupigia na kukusumbua kwa kuwa -nakumiss
2. Nitakusumbua kwa kuwa - Nina wivu na mpenzi wangu (Nahofia asijedakwa na mapapa mji)
3. nitakusumbua kwa kuwa ninataka kujua usalama wako.............
4. Nitakusumbua kwa sababu tu nina hamu na wewe na sauti yako na kila kitu chako jamani!!

kwanza tunapowasumbua ni njia mojawapo ya kuwaonyesha kuwa tunawajali!
 
big baza odm, yaani mimi babu wa wajukuu naamini katika zaburi: Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, binadamu ni nani hata umwangalie? Wewe mungu bwana wetu, jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

amen!!!!!!!!!!
 
Big Baza ODM, yaani mimi Babu wa wajukuu naamini katika zaburi: Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, binadamu ni nani hata umwangalie? Wewe Mungu Bwana wetu, jinsi lilivyo tukufu Jina lako Duniani kote!

ha ha ha ha!.....

ASEMA BWANA MUNGU WA MAJESHI......!
 



Binafsi nakubaliana sana na huu usumbufu,
na hasa kutokana na sababu za kimsingi ulizozibainisha,
Tatizo ni namna gani mnavyo excute huo usumbufu,
kwakweli kuna usumbufu mwingine hauna uvumIlivu kabisa ila ni kero tu!!!!!!!
Kila dakika, kila sekunde kama vile mmetongozana juzi tu!!!!!!NO................
 

Konakali dah...kusema ukweli umenigusa kwa ainisho lako. Aksante kwa kunibariki na hii post yako

Hapo kwenye RED hapo........dah wanawake wengine huwa tunamtazamo tofauti na huo wako...... kanitongoza rafikio nikwambie live!! duh huwa tunahofia mengi kusema ukweli na badala yake utaona tu unaonyeshwa kwa vitendo na viashiria kuwa wifey haafiki mahusiano yenu tena. utasikia tu ah flani simpendi bwana hana tabia nzuri.....mpaka umbane ndo anakwambia alishanitongoza .......kumbe ni bora tuwe tunakuja straight!!

Halafu kuna wanaume wengine wanachukulia mwanamke wake akitongozwa ni ishara ya udhaifu....utasikia "kwa nini akutongoze ulimlegezea nini?" au " huyu kakutongoza hukumpenda ndo mana umenambia, wangapi wanakutongoza mbona huwashtaki" .. Sasa ukisha kuwa na mtu mwenye mtazamo huu lazima uta-mute- hata kama umetongozwa na jirani.
 
dah,kweli "Hodi" ya chooni haiitikiwi "karibu"................

Kweli kabisa kaka mdogo.... yaani: Kama unadhani aibu ni gharama jaribu fedheha

Kweli kabisa kiongozi, ndio maana NYUKI hapigwi BUSU........................

na ndio maana mimi teamo TI-Mfalme Wa Amani NAJUA kwamba mimi ni mwerevu na mwenye akili,kwa sababu nafahamu kwamba HAKUNA NINACHOFAHAMU"

Big Baza ODM, yaani mimi Babu wa wajukuu naamini katika zaburi: Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, binadamu ni nani hata umwangalie? Wewe Mungu Bwana wetu, jinsi lilivyo tukufu Jina lako Duniani kote!

amen!!!!!!!!!!

ha ha ha ha!.....

ASEMA BWANA MUNGU WA MAJESHI......!


.............. Mnaweza mkafafanua haya katika context ya hii thread??
 
ha ha ha ha!.....

ASEMA BWANA MUNGU WA MAJESHI......!

Hahahaha:

Nikiziangalia mbingu, kazi ya vidole vyako
Mwezi pia na nyota ulizoziratibisha wewe
Kondoo pia ng'ombe wote,
Na wanyama wa kondeni,
Ndege wa angani na samaki wote baharini:

MTU NI KITU GANI, HATA UMKUMBUKE?
BINADAMU NI NANI HATA UMWANGALIE?
 

Okay so issue hapa si upelelezi ................bali namna tunavyoexecute upelelezi wetu eh?! but bacha wengine huwa hamueleweki! na hasa ukimkuta ambaye yeye skirt haikatishi mbele ya macho yake ikasalimika..........mwenye mume wa hivi ni lazima atakuwa na shaka kila ukichelewa yeye atahisi unashughulisha na kusigina haki yake.

nilishawahimshuhudia dada mmoja wamekwenda kazini asubuhi na mumewe, dada yeye ndie anayeanza kufika ofcn kisha mume anaendelea na safari ya mjini. Kufika ofcn kwa mdada, mume anamwambia wife niachie gari (alikuwa anaendesha dada) nitakupitia jioni kwa kuwa leo nitawahi kurudi, mdada likamtoka nikuachie gari yangu ukapakize viruka njia vyako huko (alitumia neno kali kidogo) .......!

Kwa mdada kama huyu ni wazi alishaumwa na nyoka so mawazo yake yameshachakachuliwa na uhaba wa imani tena so kukupigia simu, kukumonitor kwake itakuwa ni sehemu ya maisha yake bacha.

So sometimes hizi sumbufu kama mnazoziita huwa mnazicreate nyie kwa kuweka mazingira condusive................
 
Kupiga simu siyo vibaya MJ1 ila tatizo ni kwamba saa nyingine inakuwa too much. Hebu fikiria mtu anakupigia simu kama mara kumi hivi kuanzia asubuhi hadi jioni, huo kama sio usumbufu ni nini. Halafu saa nyingine unaweza kuwa umemwambia kabisa nikitoka ofisini nitapita sehemu naweza kuchelewa lakini bado maswali kibao aaaaaaaaarrgh yaani huwa inaboa sana mkuu.
 
Aisee kumbe ulishamaliza hapa, nakuunga miguu yote mkuu, saa nyingini inakuwa kero kubwa aaaaaaaarrgh.
 
Owky Da Womanizer nina imani ujumbe huu tumeupata na tutaufanyia kazi. Hii ninaihesabu kama moja ya vitu ambavyo pengine wanawake wengi tumekuwa na mtizamo tofauti na wanaume. Na bahati mbaya sana (kwa wale tulioko ndani ya ndoa) mume anapoanza kukusema kwa ajili ya kumsumbua na simu zako huwa tunakimbilia kuquestion why ananizuia, kuna mabaya gani anafanya, mbona anajihami au kwani mi si ni mkewe nina haki ya kumpigia na kumwulize yuko wapi so asinipangie............na hapo ndipo ushindani unapoanza na kusababisha mengine.
 

Nipigie simu nikiwa baa nakunywa uniambie chakula tayari: Sawa kabisa
Nipigie kama nimechelewa kurudi toka kazini: Safi sana
Nipigie kunijulia hali kama nilikuwa na afya mgogoro: Maridadi kabisa

Umenipigia nikakuambia mamito nsharudi niko hapa KingStaa na Teamo Ti tunapata bia
Dakika tano unapiga tena......uko na Teamo kweli? Dakika tano tena......utarudi saa ngapi......dakika tano tena....mbona huji.......dakika tano tena...njoo ule......dakika tano tena........uko na malaya zako........dakika tano tena...mi nalala.......dakika tano tena.....jamani nakusubiri tule....dakika tano tena....siku hizi hunipendi....dakika tano tena.......khaaaaa!

Hata kama ni kupenda sasa hii ni kero:

SIPENDI MWANAMKE MSUMBUFU ASIYENIAMINI

Afu we mjukuu mtiifu, we umetuuliza tukuambie tunachokihitaji toka kwa mwanamke, ili mtufanyie.... Tunakuambia halafu unatuchalenji. Kwahiyo unataka tufuate unachokitaka wewe? Kwanini umetuuliza sasa, si ungetushauri unachotaka tuwafanyie?...... Mwone kwanza
 
Shikamoo babu
Hii list imetulia kweli
Lakini mmhhh
 
BE.....swali linauliza ambacho ungependa kwa galfriend/mchumba au mkeo...........sio viruka njia!!

Mjukuu mpaka mtu anaoa sometimes hata hajui ni nini kilimfanya akaoa huyo mke, kwani watu huwa na ndoto nyingi tu nataka kuoa mke alie na hivi au hivi matokeo yake anaoa ambae hana vile vitu alivyokua anataka unajua kwa nini? sababu mke anatoka kwa Bwana.

Mume anaweza kuwa na vigezo avitakavyo kwa mke lakini Mungu anajua kabisa huyu akioa huyu hawataweza dumu kwani kuna yule aliefanana nae. Mjukuu Mungu mume aliekupangia hatojali kwamba wewe ni kikojozi, wewe ni malaya, wewe hujasoma n.k watu watabaki tu wanashangaa mbona Bacha ameoa kikojozi/malaya/mbaya nk. lakini yeye hata haoni huo ukikojozi au umalaya wala ubaya wa mkewe kwani ule ni ubavu wake Mungu alimpangia na hawezi kuona mabaya unayaona wewe kwa mkewe, kwani wa kwako wewe hatokua kama wa bacha.

Ndio maana unaona wengi wakiulizwa hapa wanatoa sababu mbali mbali kwani Baba enock anaemuona ni wife material, akitokea Klorokwini atasema mwanamke gani huyu nae BE ameoa, so mi nahisi kama ndio hivyo ilivyo.
 

Hapo kwenye red....huyo mdada bado ameolewa na huyo jamaa?....Wanaume wengine si rizki!

Kwa kauli hiyo, mbele za watu, babu hana ndoa tena! Haki Ya Mungu naapa!

SIPENDI MWANAMKE MWENYE DHARAU. Eti gari yangu? ku.....ake wallah!
 

ha ha ha!
sababu ingine ya kuhamia KIBIRA
 
Marahaba kajukuu..... mi nahitaji ufafanuzi wa hapo kwenye red.... umeguna au?
Babu nimeguna sababu
waweza mpata mtu mwenye hizo namba za chini na ni vitu ambavyo tunaweza kujifunza na kuvibadilisha.. lAkini hiyo number mmoja mmhhh.. vipi kAma number moja haijakamilika???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…