Mcheza Karate
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 690
- 350
"Najua sisi ni marafiki kwa muda mrefu sasa, unaweza ukafahamu kwa ufupi historia yangu ktk suala zima la uhusiano/mapenzi . Samahani kama nitakuwa nimekukwaza, NAOMBA NITAFUTIE MCHUMBA WA KUNIOA. Please, naomba uwe serious". Ni ujumbe ambao nilitumiwa wiki tatu zilizopita na dada mmoja ambaye tulisoma sekondary{ a-level) kule Ndanda, zamani kidogo. Tukakutana tena chuo baada ya miaka kama sita hivi. Anaishi Mwanza kikazi. Nami niko Dar. Lakini message hiyo ya dada yangu mwanzoni niliona kama utani tu na sehemu ya utani wa marafiki mliosoma pamoja. Lakini kinachonitatiza dada yangu huyu karibu kila siku ananiuliza kama nimemtafutia huyo mchumba? Na anasisitiza huku akionesha kuwa hatanii. Binti ni mrembo kwa kweli na ana kazi nzuri tu. Sidhani kama mwenyewe hakuna vidume vinavyompiga promo. Najisikia vibaya anapoingiza hili suala lake tunapozungumza. Nikimweleza kuwa huo utani sitaki huwa anan'gang'ania kuwa mimi ndo natania yeye hatanii. Wadau nimpotezee vipi huyu mdada? Au yuko serious kweli? Wakati mwingine huwa hadi ananikasirikia ninapomwambia kuwa sijamtafutia huyo mchumba!