Please...sema hata neno tu, waweza kumuokoa huyu mama!


Hebu tupe ufafanuzi kidogo hapo..atachukuliaje kama hali ya kawaida wakati umri unaenda na yeye anatamani kupata raha, amani na furaha kama watu wengine?
 

Mpevu...huyu mama ameomba kwa zaidi ya miaka 2 sasa. Ongeze miaka mingapi zaidi?
 
kwakweli matatizo kama haya wanayo watu wengi sana.
inavyoonekana huyu mama wakati wa ujauzito na baada ya kupata mtoto wa kwanza hali ilibadilika akasahau kama anandoa anayotakiwa kuihudumia(alijisahau).inaonekana mume alivumilia awali lakini baada ya mambo kuendelea kuwa tofauti baada ya mtoto wa pili,mume akajiona hana nafasi tena kwa mke wake(ndomaana tofauti ilianza baada ya miaka miwili)
ushauri.
huyu mama asiende kokote dawa anayo mwenyewe.
ajipime kufahamu tatizo katika kila nyanja ya furaha waliyokuwa nayo awali.
kama amezoea kulalamika,kumpokea mume kwa lawama na hasira,basi abadilike.
afanye nini.
1.aanze kurudisha upendo wote aliokuwa nao kwa mumewe kabla hata ya ndoa.afanye kwa vitendo na sio maneno.
2.kuanzia asubuhi hadi jioni awe na jambo zuri la mapenzi kwa mumewe.kwa mfano:-amuwekee maji ya kuoga,amuandalie chai asubuhi,aandae nguo za mumewe kazini usiku.awe naye mezani wakati wa kunywa chai huku akimpa stori kadhaa.(kwasasa asiombe penzi kabisa)
3.ajitahidi kuwepo nyumbani kabla mume hajarudi ili apate nafasi ya kumpokea.ampe pole ya kazi na asiingizejambo lolote lakukera wala kumchosha mwenzake.(atambue kuwa mumewe amechoka kwa kazi)
4.amuandalie maji ya kuoga na chakula na awe naye karibu akimpa kampani.asimuhoji kwa lolote baya au wivu katika hatua hii ya awali na aonyeshe kuwa ni mwanamke mwenye furaha(wanaume hawapendi wanawake wanaonunanuna).
5.awe msafi na avae nguo za kuvutia.kama anahela,akafanye shopping ya perfume nzuri na aweke chumba safi na kunukia.
akiyafanya haya,naamini baada ya muda mume atajishtukia na atabadilika.
N:B
kila jambo linalomuhusu mumewe afanye yeye na mume aone.katika hatua hii ya awali akubali kuteseka moyo na mwili.akiyazingatia haya utanipa matokeo mazuri
 
Mpevu...huyu mama ameomba kwa zaidi ya miaka 2 sasa. Ongeze miaka mingapi zaidi?

DC,
Je huyu mama bado anampenda mumewe na anaihitaji ndoa na kwamba ANATAFUTA NJIA ZA KUREJESHA HALI YAO YA UFAHARI WA NDOA?
Na je anahitaji muafaka wa ama aendelee...ama aepukane nae? Kwa haya nadhani naweza kuwa more clear kwa incidence yake hii..
 

Asante FL,

Nitamfikishia ujumbe wako. Ila kwa maelezo yake..yeye ndiye humsalimia na kumpokea mume akirudi home na nyumba waliyonayo ina maji ya kutosha ikiwa ni pamoja na heater. Ila mume ni mpenzi wa kuchat na simu na kuangalia movie peke yake. Hataki usumbu wa mke. Hapo ndio anapouliza, afanye nini?
 
Pole zake huyo dada

Ndugu zangu, mara nyingi matatizo ya mahusiano yanatatuliwa na wahusika wenyewe, kwani mara nyingi vyanzo vyake sio rahisi mtu akwambia kwa urahisi, bali ni matokeo ya tatizo ndio rahisi mtu kusema (kwa mfano, mme wangu analala nje, hali chakula nyumbani N.K.), sasa haya sio matatizo bali ni matokeo ya tatizo. Katika hili ndugu na wanafamilia wanaweza kutumika kuwashinikiza hawa watu wawili kukaa chini na kuyaongea yanayowasibu na si kutafuta tatizo baina yao na kulisolve.

Lazima mmoja wapo avunje ukimya
 
Mimi napenda kusema neno juu ya mkasa huo...

Huyo dada anachotakiwa kufanya ni kuzungumza na mshenga wao ili aweze kupata msaada kwani mshenga ni mtu wa karibu sana na mumewe anaweza akamsikiliza na kujua kinachomsibu mumewe...

Endapo itashindikana anatakiwa awashirikishe watu wa dini ambao ndio waliowafungisha ndoa,kwa mfano sisi wakristo mtu kama atakuwa na tatizo kama hilo akienda kwa padre,mchungaji,muinjilisti au mzee wa kanisa huwa wana utaratibu wa kuwakutanisha na kuwapa mwelekeo mzuri ili kuweza kudumisha ndoa yao....

Nina Imani kama itashindikana basi ni vema kuwashirikisha wazazi pande wa kiume ili kuokoa jahazi...mimi nina imani kuwa mambo yatakuwa mazuri tu na utakuwa na furaha tena kwenye ndoa...
 
jamani ndoa zimekuwa ndoana sasa ivi kila muhusika analia,

mie napenda kusema ivi, huyo mama kama kavumilia kwa miaka miwili na amejiotahidi kwa kila njia mwenzake anaona si kitu si lolote, abadilike sasa ajitahidi asiumie tena

kwanza asiache kumlilia Mungu kwani yeye anaweza, pili afanye zile kazi/vitu anavyopaswa kufanya kama mke, asimsumbue tena hata kwa chakula cha usiku,"sex) (ajitahidi naamini anaweza), asimuulize chochote.

awapende wanae, awe nao karibu. akiwa nyumbani kama ni mkristu aweke cd za nyimbo za dini, asome bible naamini atapata amani.

namtakia kila la heri
 
Wondering kama anaweza kuokoa ndoa isiyokuwepo....basically sioni ndoa kati ya wawili hao.....

 
Hebu tupe ufafanuzi kidogo hapo..atachukuliaje kama hali ya kawaida wakati umri unaenda na yeye anatamani kupata raha, amani na furaha kama watu wengine?

Awe calm, yaani asiwe na jazba, litampelekea yeye kuharibu kila kitu, DC kama ulishawahi kusafiri na chombo cha majini kama meli au ferry umbali mrefu unaweza kunielewa nisemapo hivi, kuwa maisha ni kama safari ya majini kwa maana hayako plain, kunawakati utafurahi na kuiona meli kama bembea inakubembeleza hadi unalala kabisa( boom stage in life) na kuna kipindi upepo unapelekea kuwepo kwa dhoruba ambayo kama mtu c ngangari ataapa kutopanda meli tena(depression side of life), kinachotakiwa ni kutambua kuwa upo ktk stage gani na nini kifanyike after all kila mutu anapenda amani na furaha maishani, ila tusisahau kuwa shida ni opposite ya raha, na maneno haya yametenganishwa na mstari mwembamba sana ukilteleza kidogo tu shida inakuvaa, ukiwa makini zaidi utaponda raha sana tu
 
Mpe pole!!Anatakiwa aanze kujiangalia yeye amebadilika vipi ndani ya hiyo miaka miwili ya mwisho! Kama alikua busy sana na watoto/kazi apunguze!Kama kajiachia sana mwili na urembo aanze kujipendezesha tena,hata mume akiona anapendeza sana atajishtukia!Ampe mume uhuru,kama anamchunguza afanye kwa siri sio anamwuliza!Akiwa anaangalia movie yake nae ajaribu kufanya kitu anachopenda hapo hapo karibu bila kumbugudhi,ila awe anajipendekeza bila kua obvious..unahitaji hiki au kile bila kuonyesha anajal
 
Ndoa zinambo hizi wajameni. Eehhh atulie tu na aendelee kusali sana
 
Ndoa zinambo hizi wajameni. Eehhh atulie tu na aendelee kusali sana

DA, mbona mama wa watu keshasali sana..aendelee hadi lini wakati mume ndo wala hana habari naye?
 
mkuu,
mi naungana na MAMA WA KWANZA KI-USHAURI!....

lakin pia,kabla ya hayo yote kuchukua kasi yao mi nilishauri wapeane LIKIZO YA MUDA
 
Wondering kama anaweza kuokoa ndoa isiyokuwepo....basically sioni ndoa kati ya wawili hao.....


Umeona mkuu? Hata mimi nimepata shida sana kuona kama bado hawa watu wana ndoa. Unawezaje kuishi na mke ambaye huna feelings naye tena halafu useme mna ndoa?
 
mkuu,
mi naungana na MAMA WA KWANZA KI-USHAURI!....

lakin pia,kabla ya hayo yote kuchukua kasi yao mi nilishauri wapeane LIKIZO YA MUDA

Ahsante sana Mkuu,

Nitawafikishia ujumbe. Ile counseling tunayoenda nayo tayari imeanza kuzaa matunda na ndiyo maana tukaweza kupata hizi taarifa zote ambazo mke hawajawahi kushea na mtu yeyote.

Ila kitu cha hatari sana ni kwamba mwanamume alimzuia kata kata mke wake asiwe na marafiki wa kike. Anasema hapendi. Hili limechangia sana kumzidishia mama wa watu upweke! Really sad in deed!
 


Babu huyo mama aanze na moja kama alivyosema kaizer ajiangalie alikua anakosea wapi na ajirekebishe na kama amefanya yote hayo bado mume ajirekebishe afanye hivi

Kwanza kuhama makanisa sio suluhisho kanisani tunachofuata ni mwongozo tu halafu mengine unafanya mwenyewe. Atafute kanisa lolote moja linatoa mafunzo mazuri hasa yahusuyo imani sio yale ya kukuambia nakuombe leo ukirudi nyumbani mambo shwari na ndio maana huyo mama anahama makanisa akifikiri muujiza huwa unakuja kama utiavyo chumvi kwenye mboga.

akae na kanisa moja atafute mtu amfundishe jinsi ya kuomba na awe na imani (hii ndio itakayookoa ndoa yake) amuombe mungu vile anavyohitaji mume wake awe na asiwe na haraka ya majibu na arelax as if hakuna kinachotokea humo ndani. Aendelee kumuomba mungu na ni vizuri akiwa anaamka saa 6 usiku kama anaweza kuomba mpaka saa 9 kama hawezi hata akiamka saa 7 mradi saa nane usiku imkute anaomba amlilie mungu kwa imani na awe anafunga hata kama si mara kwa mara hata mara moja au mbili kwa wiki nakuhakikishia kila kitu kitaenda sawa. Hakuna mungu anashindwa ila binadamu tunakosea tunakosa subira na imani (kwa hatua aliyofikia ni mungu tu anaweza okoa hiyo ndoa sisi hata tutoe ushauri gani hamna kitakachobadilisha) namtakia mafanikio mema
 
DA, mbona mama wa watu keshasali sana..aendelee hadi lini wakati mume ndo wala hana habari naye?

Kama ni hivyo aangalie tabia yake imebadilika kwa kiasi gani pengine hafanyii chochote mumewe kama zamani.
 

Maty,

Huyu dada anasema ni muumini mzuri sana na amekuwa akiomba kipindi chote cha matatizo yake. Na bado anaendelea kuomba. Kwa sasa ameamua kutulia na kuendelea kusali kanisa lake la zamani..Katoliki.

Swali ambalo binafsi linanisumbua...aendelee kusali, kuomba na kufunga hadi lini?
 

well said mama wa kwanza akishafanya yote hayo amalizie na kusali kwa imani huku akijiburudisha na nyimbo za dini kama alivyosema mwenzangu mmoja atakua amemaliza tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…