Hii ni story ya mwanamke mmoja ambaye nimekutana naye katika harakati za kupeana ushauri wa kutatua matatizo yanayotusibu katika mahusiano. Amekubali niiweke hapa ili kupata maoni ya wadau. Matatizo yake ni mengi sana ila kwa ufupi ni kama ifuatavyo:
1. Suala na unyumba katika ndoa yao yenye umri wa karibia miaka 4 wakiwa na watoto 2, limekumbwa na ukame wa ajabu. Wanashiriki tendo la ndoa kama mara 2 tu kwa mwezi na ni lazima mume atake. Mwanamke akiomba anaambiwa kuwa mume hawezi kufanya tendo la ndoa mara kwa mara. Wakati wa uchumba wao na siku za awali za ndoa yao, walikuwa wakishiriki tendo la ndoa hata zaidi ya mara 2 kwa week na wote waliliridhika na kufurahia tendo hilo. Hali ilianza kubadilika baada ya kama miaka 2 hivi. Mbaya zaidi hata kama mmoja akirudi safari baada ya kukaa kwa muda mrefu kiasi cha week nzima au zaidi, bado hakuna uhakika wa tendo la ndoa!
2. Mawasiliano ndani ya nyumba hasa hasa yale ya kimahaba nalo limekuwa tatizo. Yaani ni kama vile wanaishi maktaba. Muda mwingi mume akiwa nyumbani anacheza na simu yake akituma na kupokea sms kutoka kwa watu tofauti. Pia mume akiwa nje na jamaa wengine anakuwa mchangamfu sana, akiongea na vicheko juu.
3. Vitu vingi vya mume vimefunigiwa katika mkoba (brief case) wenye password ambayo mke hajui. Pia mume anazo account za benki ambazo mke wake hazijui kabisa. Na simu za mume zimewekewa password ingawa vitu vyote vya mke ikiwemo simu, account za bank n.k viko wazi na mume anavivinjari wakati wowote anaopenda.
4. Ni nadra kwa mume kukubali na kusifia (to appreciate) kitu alichokifanya mke. Na mara nyingi anamkatisha tamaa katika mipango yake anayomshirikisha.
Kutokana na haya matatizo na mengine mengi, huyo mama amekosa raha muda mrefu na aliwahi kufikiria kujidhuru (got closer to attempt suicide) ila kwa sasa ameamua kutafuta ushauri ama wa kuokoa ndoa au maisha yake. Amesali sana, amfeunga sana na kubadili makanisa kama nguo za mashidano ya mavazi lakini bado nazunguka pale pale. Kwa hiyo wadau nawaomba ushauri wenu ili niongeze kwenye package ya counseling ninayoendelea nayo kwa sasa.
Wasalaam, ....Babu DC
kwakweli matatizo kama haya wanayo watu wengi sana.
inavyoonekana huyu mama wakati wa ujauzito na baada ya kupata mtoto wa kwanza hali ilibadilika akasahau kama anandoa anayotakiwa kuihudumia(alijisahau).inaonekana mume alivumilia awali lakini baada ya mambo kuendelea kuwa tofauti baada ya mtoto wa pili,mume akajiona hana nafasi tena kwa mke wake(ndomaana tofauti ilianza baada ya miaka miwili)
ushauri.
huyu mama asiende kokote dawa anayo mwenyewe.
ajipime kufahamu tatizo katika kila nyanja ya furaha waliyokuwa nayo awali.
kama amezoea kulalamika,kumpokea mume kwa lawama na hasira,basi abadilike.
afanye nini.
1.aanze kurudisha upendo wote aliokuwa nao kwa mumewe kabla hata ya ndoa.afanye kwa vitendo na sio maneno.
2.kuanzia asubuhi hadi jioni awe na jambo zuri la mapenzi kwa mumewe.kwa mfano:-amuwekee maji ya kuoga,amuandalie chai asubuhi,aandae nguo za mumewe kazini usiku.awe naye mezani wakati wa kunywa chai huku akimpa stori kadhaa.(kwasasa asiombe penzi kabisa)
3.ajitahidi kuwepo nyumbani kabla mume hajarudi ili apate nafasi ya kumpokea.ampe pole ya kazi na asiingizejambo lolote lakukera wala kumchosha mwenzake.(atambue kuwa mumewe amechoka kwa kazi)
4.amuandalie maji ya kuoga na chakula na awe naye karibu akimpa kampani.asimuhoji kwa lolote baya au wivu katika hatua hii ya awali na aonyeshe kuwa ni mwanamke mwenye furaha(wanaume hawapendi wanawake wanaonunanuna).
5.awe msafi na avae nguo za kuvutia.kama anahela,akafanye shopping ya perfume nzuri na aweke chumba safi na kunukia.
akiyafanya haya,naamini baada ya muda mume atajishtukia na atabadilika.
N:B
kila jambo linalomuhusu mumewe afanye yeye na mume aone.katika hatua hii ya awali akubali kuteseka moyo na mwili.akiyazingatia haya utanipa matokeo mazuri