Please...sema hata neno tu, waweza kumuokoa huyu mama!


anaomba sana lakini hana imani kaka DC mimi nishawahi kutokewa na matatizo yaliyonisumbua nikawa naomba kwa imani na kila ambacho nilimuomba mungu alifanya tena bila mimi kutarajia wakati mwingine mungu anapokaribia kufanya jambo unaona dunia yote ndio inaanguka kumbe ndio wakati ambao mungu anataka kufanya vitu vyake. Asikate tamaa najua ni ngumu sana ila ajitahidi
 
Kama ni hivyo aangalie tabia yake imebadilika kwa kiasi gani pengine hafanyii chochote mumewe kama zamani.

DA kwani ukibadilika ndiyo tiketi ya mume kuzira? Kinachoonekana kwa sasa ni kuwa mume amezira karibia kila kitu cha huyu dada. Halafu mazungumzo ndani ya hiyo nyumba kwa sasa yanaanzia kwa mama tu vinginevyo inakuwa kama shetani anapita wakati wote, ni zaidi ya library!!

Yaani mume akiingia ndani na mke akaamua kunyamaza ndo imetoka. Lazima mke amsalimie siku zote. Hii ni sawa jamani?

Halafu kinachonishangaza, kwa upande wangu mimi ndo huanzisha mazungumzo mara nyingi na hata nikiwa mbali na wife napiga simu nyingi na sms nyingi zaidi yake? Hii kitu imenitisha sana!
 

Nitaku-PM kwa maelezo zaidi. Nahitaji sana msaada zaidi ili niweze ku-update package yangu ya counselling.
 
kulingana na hii habari...mama ndo ana matatizo japo inaonekana kama mama anaonewa.......

wewe fikiria huyu jamaa hampigi....hamnyimi chakula.....mavazi nk.... kuna kitu huyo mama amemfanyia mumewe sasa mumewe akaweka level of access....yaani kama ni database mama anaruhusiwa kuona ile interphase tu.... na baba anabaki yuko kwenye schema......

sasa ili upate mwafaka wa jambo hili na wewe msuluhishi usuje onekana mbaya badae......natural justice inatakiwa....muulize mume wa huyu dada......

kuna kitu huyo dada kakuficha......yaani ni kama mwanamke anayefanya abortion halafu akienda kuungama anaungama dhambi zingine tuu... na ile moja kubwa kabisa anaiaccha......muulize vizuri nini amemfanyia mume wake
 

hizi ndoa bwana, kichomi kitupu!...alishawahi kukaa nea na kuongea nae kirafiki zaidi? coz watakapotulia na kuongea pamoja kimapenzi huyu mama ndio atapata suluhu na kujua wapi amekosea wapi arekebishe!...amshirikishe wenie kwa hili.
 
dah! acha nifungue mafaili yangu, nitarejea.
 
DC hii quote hapo kwa signature yako inamfaa sana "WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE"

Mama anatakiwa kuvunja ukimya mara moja. Abadilike otherwise gharama za kutokubadilika zitazidi za kuwa alivyo.
 

Nakubaliana na wewe JS ila suala la kuondoka mimi nalipinga kabisa asiondoke kama nyumba ni yao wote na watoto so akae alee wanae hapo hapo na inavyoonyesha huyo mwanaume familia anaitunza tatizo tu haelewani na mama, na kizuri huyo mama ana kazi nzuri mi naona kazi yake ni ndogo tu hapo uvumilivu na kumuomba mungu kwa imani na huko kuomba wala si lazima ulale kanisani kanisani unaenda tu kupata mwongozo halafu unaendelea mi namshauri asiondoke na wala asi giveup cha kufanya aanze kuchukulia hayo matatizo kama changamoto tu asiyaweke sana rohoni ingawa ni ngumu lakini ukiamua inawezekana
 
hizi ndoa bwana, kichomi kitupu!...alishawahi kukaa nea na kuongea nae kirafiki zaidi? coz watakapotulia na kuongea pamoja kimapenzi huyu mama ndio atapata suluhu na kujua wapi amekosea wapi arekebishe!...amshirikishe wenie kwa hili.

Dada Nyamayao, huyu mama anasema kila anapojaribu kuongea na mumewe anamuona kama nyau fulani tu anayemsumbua. Na mume anasisitaza kwamba yeye ndiye mume wake na kwa kuwa hajamnyima chakula au kumfukuza home atulie tu! Nadhani kuongea kimapenzi ni ngumu sana kwani mama anasema amejaribu kila njia ameshindwa.
 


Huyo mwanaume ana GUBU kisa cha kununa dume zima nini hapo bwana???
 
hizi ndoa bwana, kichomi kitupu!...alishawahi kukaa nea na kuongea nae kirafiki zaidi? coz watakapotulia na kuongea pamoja kimapenzi huyu mama ndio atapata suluhu na kujua wapi amekosea wapi arekebishe!...amshirikishe wenie kwa hili.

dearest upo umepotea mwe! karibu mwaya
 
hizi ndoa bwana, kichomi kitupu!...alishawahi kukaa nea na kuongea nae kirafiki zaidi? coz watakapotulia na kuongea pamoja kimapenzi huyu mama ndio atapata suluhu na kujua wapi amekosea wapi arekebishe!...amshirikishe wenie kwa hili.
nyamayao, kwanza hali yako sweety?
bek to yowa posti: mimi akili yangu inaniambia huyu jibaba kuna kitu anaficha na sio kwamba kuna kitu kakerwa na jimama, ningeshauri huyu mama awe spy kwa mume wake kwa muda ili aone nini kinaendelea, usishangae mume kaingia kwenye u bwabwa. kama ku spy itamuongezea presha acha akate one way tiket tu. hamna ndoa hapo. ndoa imekaa kama mchezo wa kihindi bana, mke anataka miguno mume anacheza na simu. gademu!
 
DA, mbona mama wa watu keshasali sana..aendelee hadi lini wakati mume ndo wala hana habari naye?

Asikate tamaa aendelee kusali huku akitafakari tatizo na namna ya kulitatua.
Kitu kingine hapa wadungu, akina dada wengi wa siku hizi hawajui maana halisi ya kuolewa, wanaona ukifikisha umri fulani tu lazima uolewe. Si ajabu kuona mchumba wako (wadada wa siku hizi) anadai kuolewa, unakuta anasema "Sasa dear utanioa lini maana rafiki zangu wote wameolewa halafu umri unakwenda...."

Mtu hakuoi kwa sababu ya rafiki zako wote kuolewa, wala wewe kuzeeka, ndoa ni sakrament. Dada zangu, kuolewa ni zaidi ya wewe kuhama kwenu kwenda kwa mchuchu wako, wala kulala kitanda kimoja na mme, timizeni matakwa ya ndoa, ndipo kesi nyingi zitapungua.

Mtaani kwetu kuna bint kaolewa mwezi wa sita mwaka huu (2010), Siku moja(last month) kashindwa kuelewana na bwana ake kachukua Canter kapakia vyombo vyote alivyopewa zawadi kwenye harusi karudisha nyumbani kwao. Hapa kuna mke kweli?. Na baada ya kushauriwa karudi kwa mme wake ila jamaa kampiga stop kurudisha tena vile vitu pale home, kweli ndoa itadumu hapa? (hii ni true story aminin usiamini)
 

Edson, ni vigumu sana kumpata mume kwa kuwe huyu dada tumekutana online na sina hakika kama anaweza kuwa tayari kunikutanisha na mume wake. Hata hivyo upo uwezekano wa yeye kunificha baadhi ya vitu ambavyo labda anajua kuwa alifanya na vikamkatisha tamaa mume wake. Ila hata kafanya jambo lolote, anastahili adhabu harsh kiasi hicho? Kwa nini asimpe talaka akaanza maisha yake binafsi na mume akawa huru kuoa tena?
 

hii ndoa imeingiwa na kidudu mtu kaka angu tena huyo dada ana afadhali mume anatoa matumizi wengine huwa wanakimbiwa kabisa hawapati matumizi wala watoto hawahudumiwi
 

Sawa Dc, ningeweza kushauri hiki, ajiangalie ni wapi alipoanguka mpaka ikawa hivyo, maana yawezekana kuna mahali alifungua mlango yeye mwenyewe na kuruhusu hiyo hali, mwambie ajikague anaweza kugundua tatizo lilianzia wapi na ikiwa atagundua hilo ni vizuri akarekebisha.
 

Maty,

Una maana aendelee kukaa home na waendelee kuchangia kitanda kimoja kama maiti walioko kwenye friji ya mochuari?
 

na chakula cha ucku anakipata?.....hizo ishu za kuondoka home ckubaliani nazo, y aondoke?
 
Maty,

Una maana aendelee kukaa home na waendelee kuchangia kitanda kimoja kama maiti walioko kwenye friji ya mochuari?

ishu za wamama cku hizi kukimbizana na watoto kuhama zimepitwa na wakakti, abanane hapo mpaka kieleweke...
 
Huyo mwanaume ana GUBU kisa cha kununa dume zima nini hapo bwana???

Dena Amsi, kuna wanaume wanajua kununa usiombe, kuna jamaa namfahamu kwa kununa ndo mwenyewe mpaka huwa najiuliza hivi huko nyumbani kwake inakuwaje kwa mke wake, kwa hiyo wala usimshangae huyo anaemnunia mkewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…