Please...sema hata neno tu, waweza kumuokoa huyu mama!

Kaka angalia huyu mwanamke anakutaka, kwa nini asizungumze na mwenzake anazungumza na wewe? Na wewe kwa nini usiende kuongea na wote wawili? mademu hata kama atakuwa anaishi kwake vizuri akikurtaka atazusha mambo mengi saaana ili kukupa wewe nafasi.
 
Kaka angalia huyu mwanamke anakutaka, kwa nini asizungumze na mwenzake anazungumza na wewe? Na wewe kwa nini usiende kuongea na wote wawili? mademu hata kama atakuwa anaishi kwake vizuri akikurtaka atazusha mambo mengi saaana ili kukupa wewe nafasi.

Pretty much in line with my way of thinking..

Au huenda hamtaki lakini jamaa aki make a move anakula kilaini kama analia...

Kwa ujumla maisha ya ndoa magumu bana. Kuunganisha personalities mbili halafu kusiwe na mgogoro ni vigumu sana.
 

nakuunga mkono kwa maneno yako.jamani kwa nini mtu unganganie ndoa kiasi hicho?wanawake tunatakiwa tujiamini,kwani mtu huwezi kuishi bila mwanamume?au umgande mtu ambae hakutaki kisa watoto watapata tabu?ukiwa unajimudu kimaisha sioni kama hilo ni tatizo.mimi nimelelewa na mama na tulikuwa 4,mama yetu alitelekezwa na baba etu,na tumeishi maisha ya furaha na amani kabisa. wote tumeshakua tunamhudumia vizuri sana mama etu,na hatukuwa wanyonge wa kusema baba yupo wapi, kama kuomba huyo dada ameshaomba sana,huwezi jua pengine anaweza akaolewa na mwengine na akaishi maisha mazuri tu.maisha yenyewe mafupi jamani,ataishi maisha ya huzuni kwa muda gani?kama kujitahidi amejitahidi vya kutosha. sijui upande wa m.me kwa hii story,maana maisha katika story kuna pande mbili,lakini kama anayoyasema huyu dada ni ya kweli,aanze kuishi kwa kuwajali watoto wake tu,mwanzo ni mgumu,baadae atazoea.au kama ndio anapenda pasipopendwa aendelee kukaa hivyo hivyo
 
mamushka dia umemaliza kila kitu kaka DC mpelekee hii huyo dada na nakuambia ipo siku atakuja kutoa ushuhuda hapa yaani hata sina la kuongeza. MAMUSHKA WEWE NI NOMA
Hahaaa jamani Maty thank you dear, si unajua inatubidi tutambue hayo kabla ya kuingia ndugu yangu.
 
DC na wengineo,
Jambo la muhimu ni kuuliza ujue kama kuna mambo yaliyofanywa na mdada na kumfanya mume awe na kinyongo. Wanawake siye huwa tunasamehe sana na kuweka roho nyeupee. Wenzetu hawa kwa vinyongo usiwapimie mtu wangu! Kama kuna kinyongo itakuwa ngumu sana kuanzisha mazungumzo ua muafaka.

Njia moja niionayo ya kumsaidia ni kupima je anaweza kuishi bila huyo mume kwa sababu zozote zile ziwe za kiuchumi au kijamii. Kama anaweza basi aondoke mara moja kabla mwaka mwingine haujaisha maana unapoahirisha kuondoka basi ujue itakuwa vigumu huko mbeleni na huenda mapenzi yatakuwa yameshachuja vibaya sana. Bora aondoke sasa huenda huyo bwana akajirudi akambembeleza na wakamaliza tofauti na kuwekeana masharti ya kuishi baada ya muafaka.

Kama hawezi kuondoka kwa sababu za kiuchumi basi ajipe malengo - 3-5 years ajiimarishe kiuchumi. Kama ni kijamii ikiwemo imani za dini basi awape shinikizo familia/ viongozi wa dini kuingilia kati kupata muafaka maana mtu huwezi ishi na mwanaume tena wa ndoa maisha hayo.. anamkwaza tu hapo. Siku uzalendo utamshinda mwanadada akapata mwanaume wa pembeni, si ajabu huyo bwana akamshikia bastola na kumtoa roho!
 

Hapo ndipo na mimi napata shida kuelewa BJ, mtu unapata mateso, unanyanyaswa mpaka unaiona dunia Jehanamu, bado umeganda tuuuu,

Tatizo nini?? Watoto?? Mungu amekupa mikono, akili na neema ya Elimu hata kama ni ndogo, na labda una kazi yako, kwa nini usiondoke ukatafuta maisha na watoto wako??

Kama anataka watoto na anawapenda awape mahitaji yao wakiwa kwangu, then wkikua watajua pumba ni ipi na ngano ni ipi??

OK, unavumilia, ni majaribu Mungu atafanya njia lini?? Wakati presha inakuua?? Unakufa kabla ya siku zako kisa nini??

Kwanza ukijaribu kuangalia wakati unaingia kwene ndoa hukumshirikisha Mungu asilimia mia moja ktk maamuzi yako, lakini mambo yanapokuwa magumu Tunasema Mungu "umeniacha" kwene ndoa yangu.

Mungu si dhalimu jamani, "Hata pamoja na hilo jaribu nitafanya mlango wa kutokea"
We unaolewa by chance, simply coz ametokea wa kukuoa, na kwa sababu unataka kuolewa, baada ya miaka miwil/mitatu

jamaa anaona nilikosea njia, afu mbaya zaidi anakwambia kabisa, hivi ilikuwa je hadi nkakuoa wewe??

Hapo ukiangalia una watoto wawili au watatu, unabaki unasema kama sio hawa watoto, ningeondoka.

Mwanamke jipange sawasawa, tumia akili, nguvu na uwezo uliopewa na MUNGU, mkabidhi Mungu njia zako, ili hata ukikutana na milima na hayo mabonde kwene ndoa unakwenda kwa Mungu kwa ujasiri.

Hakuna sababu ya kuolewa kama, sitakuwa na furaha ktk hio ndoa.
Lakini pia ninayo Imani kabisa ya Kwamba MUME/MKE mwema hutoka kwa BWANA. Kwa majira na nyakati sahihi.


Mnisamehe!!!
 
Pole zake huyo Mama. Hivi ndoa ni ngumu kiasi hiki? Nitaogopa kuoa kwakweli
 


Nahisi nahitaji msaada juu ya swala zima la ndoa, kwa nn nasema hivo,
Mi najua ndoa ni makubaliano kati ya mtu A na mtu B, na kinachowaunganisha hawa watu ni UPENDO,

That means, ulimwambia mtu nakupenda ndipo mkafika huko kwene ndoa, mshenga hakuepo, mama, baba, mjomba, rafiki nakadhalika zake hawakuepo.

Wenyewe walisikia kutoka kwenu, wakawapa suport (wapambe), sasa unapofika wakati mnashindwa kumaliza matatizo yenu wenyewe mpaka hawa wapambe kwa jinsi yao waingilie kati?? Kuna upendo hapo Kweli??

Au tukishaoana tunakuwa kama CUF na CCM, so tunakaa kwene baraza tunafuta muafaka??
 
Hebu tupe ufafanuzi kidogo hapo..atachukuliaje kama hali ya kawaida wakati umri unaenda na yeye anatamani kupata raha, amani na furaha kama watu wengine?

Umeona eeh, Hivi unajua ni rahisi sana kuomba na kusubiri Mungu alete majibu ya njaa, umaskini na uponyaji (huku ukifanya kazi, ukitumia dawa), kuliko kusubiri nafsi ya mtu ibadilike iwe kama unavyotaka wewe.

Nafsi ya mwanadamu ambaye hata akiona juhudi zako, anajisemea moyoni maskini huyu anajitahidi ili nimpende lkn mbona sijisikii hivyo.
Ndo kwanza anachart, na nini tena.....Mpango mzima.

Nafsi, ambayo hata Mungu akishuka akaongea kama imeamua ni ameamua tu,
Nafsi ya mwanadamu jamaniiiiiii.
 
Ndoa zinambo hizi wajameni. Eehhh atulie tu na aendelee kusali sana

Atulie aendelee kusali sana, mpaka lini?? Kasali miaka miwili,
Amezunguka makanisa na ninavyojua atakuwa ameombea, amekunywa mafuta ya annointing sana, acha maji ya baraka,

Mapepo yamekemewa hadi basi, na nguo zake kashapeleka zikaombewe labda, lakini haoni mabadiliko.
Maji yamebadilishwa kuwa damu ya Yesu na atakuwa amenywesha tu kwa namna yake.

Ngoja niache.... but

"Soul Mate"????? Nafsi ya baba haiambatani na nafsi ya mama.
Na marafiki hawezi kwenda njia mmoja wasipopatana.
 
Wanawake sasa tupevuke na tuweze kusoma alama za nyakati.
Wanawake huwa tunaongea kwa mdomo kama hatumtaki mwanaume lakini wenzetu huonesha vitendo. Vitendo huongea zaidi. Hivi kwanini roho yako iumizwe na mtu! Men have power b'coz we (women) give them.
Huu sio wakati wa kulambana unyayo. Kwanini 2nakuwa wazito kumake decisions! Wenzetu wakiona hawatufai wanatutimua fast ila sisi tunawalea.
Mwambie huyo mama, apeleke hiyo ishu kwa wazee kama mambo inaendelea vibaya atafte ustaarabu mwingine. Awe na confidence ya maisha na wanawake wote tusiishi kwa mazoea jamani. Machozi yetu hayatokauka.
Natamani huu ujumbe umfikie kama ulivyo huyo mama bila kuchakachuliwa.
 
Mpaka pale mungu atakapojibu. Kumbuka mungu wetu ni mwaminifu hawahi wala hachelewi, ni kwa wakati wake ndipo atajibu
 

Tafadhali tafadhali usije geuka badala ya kuwa mshauri ukamega mke wa mtu kama tulivyosoma hapa juzi jamaaa kala demu wa jamaa yake wakati wa ushauri.
 

Atakuwa alimwambia baba wa watu aende chumvini na hapo baba akaona huyu mama kakosa heshima na huko saluni anakoshinda wanafundishana ujinga na ndio maana amempiga marufuku kuwa na marafiki wa kike, sasa DC sijui yeye jinsia yake mpaka wakapeana hii issue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…