mimi nilisharipoti mara kadhaa kuhusu sms za habari, ratiba na matokeo ya michezo hasa EPL na LA LIGA waziondoe lakini hawanisikilizi kabisaaaaaa! Nimeshaenda kwenye karibu ofisi zao (Mlimani City, Gerezani, Nyerere Road na Habour's Tower) zote kulalamika jambo hili, wananiahidi wataziondoa, lakini hawafanyi hivyo. Kibaya zaidi wakati mwingine wananiletea matokeo ambayo tayari nayafahamu (yaani hata ya siku iliyotangulia), pia zinaweza kuingia sms 2 (yaani page 2), ila ya pil inakuwa ina neno au herufi moja tu au empty sms. Mara nyingi zinatoka kwenye namba hizi:1577150 na 15770, zaidi ya yote wananikata hadi shilingi 300 kwa sms moja! Yaani jamaa ni wezi sana!