Pluijm ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi Yanga, Lwandamina Kocha Mkuu

Pluijm ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi Yanga, Lwandamina Kocha Mkuu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa Hans Van der Pluijm amekubali kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo huku nafasi ya Kocha Mkuu ikichukuliwa na George Lwandamina kutoka Zesco ya Zambia.

Hans.jpg

Akithibitisha taarifa hizo, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga amesema uongozi wa klabu hiyo ulikuwa kwenye mazungumzo na kocha Hans ili aridhie maamuzi hayo, na hatimaye amekubali kufanya kazi na kocha George Lwandamina.

Akizungumzia nafasi ya kocha msaidizi Juma Mwambusi, Sanga amesema hatma yake bado haijafahamika kwa kuwa nafasi ya kocha msaidizi itategemea matakwa ya kocha mkuu, na kwamba mambo yote yatakapokaa sawa, uongozi utatoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kulitambulisha rasmi benchi jipya la ufundi.

Kuhusu baadhi ya wachezaji kuachwa kutokana na mapendekezo ya kocha huyo mpya, Sanga amesema kuwa hilo halijawa wazi na kwamba hadi sasa hawajapokea mapendekezo yoyote ya kuacha wachezaji na kinachosubiriwa kwanza ni ripoti ya mwalimu Hans ya mzunguko wa kwanza wa ligi.

Sanga.JPG

"Tunatarajia kupokea ripoti ya mwalimu muda wowote kuanzia leo, tutaijadili na baada ya hapo tutamkabidhi kocha mpya halafu ndiyo tutajua kama kuna wachezaji atataka kuwaacha au la" Amesema Sanga

Akifafanua sababu za mabadiliko hayo Sanga amesema kuwa uamuzi huo ni kwa ajili ya kuboresha kikosi hicho, na kwamba ni mabadiliko ya kawaida katika uendeshaji vilabu.

lwadamina.jpg

Chanzo: EATV
 
Sasa huyu mzugu ufundi wa kikwetu atauweza wapi? Anaweaza chinja kuku mweusi huyo? anaweza shikilia kibuyu au kutembea uchi usiku wa manane huyo?
 
Mkurugenzi wa ufundi wa Klabu ni mtu mhimu sana kwenye maendelea ya Klabu cha Moira wa Miguu. Huyu ndiye anayetengeneza mfumo wa Klabu, maono na maendeleo yake kwa Urefu na Mapana kwa Ujumla wake. Hivyo kitaaluma ni bosi wa Kocha ambaye anaweza kufukuzwa kwa kushindwa kutimiza malengo yaliyowekwa na Mkurugenzi wa Ufundi na Jopo lake.
Kwa hiyo Plujm ni mtu muhimu zaidi kwa sasa
 
Sasa huyu mzugu ufundi wa kikwetu atauweza wapi? Anaweaza chinja kuku mweusi huyo? anaweza shikilia kibuyu au kutembea uchi usiku wa manane huyo?
Akili zetu watu wenye ngozi nyeusi zimekwamia hapa!
 
Mgongano lazima utokee hapo,mzungu hatataka Mzambia awe na mafanikio kumpita yeye....tusubili.
 
Mkurugenzi wa ufundi wa Klabu ni mtu mhimu sana kwenye maendelea ya Klabu cha Moira wa Miguu. Huyu ndiye anayetengeneza mfumo wa Klabu, maono na maendeleo yake kwa Urefu na Mapana kwa Ujumla wake. Hivyo kitaaluma ni bosi wa Kocha ambaye anaweza kufukuzwa kwa kushindwa kutimiza malengo yaliyowekwa na Mkurugenzi wa Ufundi na Jopo lake.
Kwa hiyo Plujm ni mtu muhimu zaidi kwa sasa
Si kwa soka la Tanzania hii.
 
Back
Top Bottom