Tetesi: PM, Philips, Foreign na February wamekalia kuti kavu?

Tetesi: PM, Philips, Foreign na February wamekalia kuti kavu?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Msimu wa kutumbua tumbua katika utawala wa mtukufu hautakoma kamwe. Kila baada ya muda kuna kigogo ndani ya utawala anatumbuliwa. Ndio mtindo wake, hivyo tunapaswa kuuelewa na kuuzoea tu.

Wadadisi wa mambo wameshaweza kumsoma mtukufu na kuweza kutengeneza baadhi ya tabiri ambazo mara kadhaa zimekuwa kweli kabisa. Na JF ndio imekuwa kinara wa kuweza kuzisoma Codes na kuunganisha mambo.

Ukitazama kauli kadhaa za mtukufu kuhusiana na PM wake utagundua kabisa ipo siku atatemwa tu. PM huenda ameshachokwa na bosi wake na kilichobakia ni kutengenezewa sababu nzito ya kwenda na maji. Hili la korosho ndio lilikuwa jaribio la pili, limewakumba wenzake na kumuacha salama PM, lakini kwa jicho la karibu sana, linaonekana bado bichi mnoo, hivyo PM akae kwa umakini.....

Upande wa Philips nako hali si hali, uchumi umeyumba, makusanyo ya kodi anadai yameshuka, hakuna vyanzo vipya vya mapato, mambo hayaendi, lugha zinagongana tu na bosi wake au mtoto wa bosi. Lazima mchawi atafutwe tu. Waswahili wanasema mchawi ndio alipewa alee mtoto, na mtoto ameshaangamia, kitakachofuata ni mchawi naye kuangamizwa. Philips hawezi kukwepa mtego tena. Ni suala la muda tu.....

Foreign naye huenda ameshachoka, amebanwa mnoo, hana pakusimamia, diplomasia ya Tz imepwaya mno, uwaziri kwake umegeuka kuwa shubiri, anatamani huo mzigo autue lakini anaona aibu na woga umemjaa, hana ujanja, msimamo wa bosi hauwezi kuivusha nchi kimataifa, mabalozi wamelala fofofo, hawana mbinu mbadala. Mtego uliopo mbele yake kwa sasa ni kuwa dalali wa kuuza korosho kimaitaifa. Huo ni mtihani kwake, Kitakachofuata ni kwenda na maji tu...

February yeye anajua tayari yuko kwenye blacklist, hatakiwi kuwepo kwenye baraza, anatuhumiwa kuwa ana ndimi mbili, haaminiki kabisa, anatajwa kama ndiye mjumbe mkuu wa yule adui ndani ya serikali. Kwake ni suala la muda tu, uamuzi ulishafanyika toka kitambo na mwenyewe anajua hilo. Ni

Hizo zote ni ndoto za Zanzibar-ASP.
 
Na yule wa makinikia nae ajiandae endapo tutashindwa kesi na sakata zima likafeli huki tukishindwa kulipwa chochote.

Mkulu huwa sambamba na wasaidizi wake pale wanapotekeleza alitakalo, ila likibuma, basi yeye hujinasua kwa kuwatema ili wao ndio waonekane ni chanzo/wazembe.

Msisahau yeye anapenda kuonekana ni mtu wa mafanikio siku zote na si vinginevyo na kwamba hashindwi jambo kitu ambacho si kweli na katika hali ya kawaida hakiwezekani.

To work with Mr. Successful, you need first to guarantee him success all the times, otherwise you are gone.
 
This is rubbish at best[/QUOTE
Whether it is gibberish at it best or not time will tell, let us give it a break and have benefit of doubt to the players and the game.
 
Kama atamtema PM basi atakuwa amefanya kosa kubwa sana la kiufundi. Itamgharimu zaidi ya anavyodhani.

PM ni very dedicated katika kila anachokifanya. Pia PM anajitofautisha na bosi wake katika matumizi sahihi ya kuweka mizania ya maamuzi.

PM anajua ni wakati gani awe mwanasiasa na ni wakati gani asicheke na mtu aliye mbele ya uso wake. Hao wengine haswa february, anaweza kupigwa chini muda wowote, kwa sababu keshaonyesha kejeli za zile katuni zake.
 
Kama atamtema PM basi atakuwa amefanya kosa kubwa sana la kiufundi. Itamgharimu zaidi ya anavyodhani.

PM ni very dedicated katika kila anachokifanya. Pia PM anajitofautisha na bosi wake katika matumizi sahihi ya kuweka mizania ya maamuzi.

PM anajua ni wakati gani awe mwanasiasa na ni wakati gani asicheke na mtu aliye mbele ya uso wake. Hao wengine haswa february, anaweza kupigwa chini muda wowote, kwa sababu keshaonyesha kejeli za zile katuni zake.
MKUU HAJAWAHI KOSEA WE HUNA BABA NN TOKA LINI BABA ANAKOSEA
 
Back
Top Bottom