KERO Poa Communication tawi la Zanzibar huduma zao ni mbovu

KERO Poa Communication tawi la Zanzibar huduma zao ni mbovu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakala wa mtandao wa Yas wajulikanao Poa Communication tawi la Zanzibar enelo la Amani huduma zao ni mbovu sana.

Nilitaka kupatiwa huduma ya Uwakala wa Mixx by Yas na nikaelekezwa niende ofisini kwao kwani ni miongoni mwa kampuni zilizoteuliwa kutoa huduma hizo. Nilichokikuta najuta hata kwanini nimienda, ukifika mapokezi yao ni ya dharau sana hawajali hata wateja na muda wao wanaoutumia, nimetumia muda wa saa mbili nzima sijapata huduma ninayostahiki.

Nimeambiwa nitatumiwa namba kwenye simu nimekaa wiki nzima namba haijatumwa, ikanibidi nirudi ofisini kwao wakanielekeza nitafute fomu yangu baada ya kuitafuta hafla wananiambia kuwa fomu za wiki iliopita bado hazijaanza kufanyiwa kazi.

Kwa kweli ni changamoto kubwa sana na sijui ata kibuti hichi wanakitoa wapi
 
Back
Top Bottom