Poa nipoe, nisijepiga mayowe

Poa nipoe, nisijepiga mayowe

Kiranga

Platinum Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
78,790
Reaction score
128,275
Shairi hili ni la kwa wa ubani aumwaye.

Poa nipoe, kohoa nikohoe
Harija zote nitoe, ni bwage moyo Kaole
Zari na mgolole, wenye staha tuoe
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Maradhi faradhi, mimi yako faraji
Fadhaa ya kizazi, hari mwili si radhi
Kwa mtwana na kadhi, dhama isiyo hadhi
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Dhaifu si nuksani, afya kwetu hisani
Toka bwana manani, jamali iso kifani
Vipi tuikose shani, kwa mpito wa ubani?
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Wamezuriwa madhila, wetu wa kila kabila
Iskanda mwenye dira, jemadari aso bila
Mauko kumzingira, tama likatia hila
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Tambo konde la uduni, moto wa ujinga kuni
Madhila kwetu sabuni, kwa korija na makumi
Kutufulia zabuni, ya mwili kuurubuni
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Maisha kufingirisha, takilifu tunakwisha
Bora kuweza huishwa, kwa mahaba yasobisha
Na manani kumpisha, atufanyie aisha
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Kaditama nimefika, saba timilifu beti
Roho imesuuzika, chini niweze kuketi
Maneno yakikufika, uweze ree kwa cheti
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
 
Fadhila zako karima, mja nimezipokea
Fadhila kwangu ni njema, daima tazitumia
Fadhila zitasimama, muhali kuziachia


Anaepewa hidaya, Mola kamjaalia
Kuridhi na kuridhia, huwa anafurahia
Awe na uso wa haya, fadhila kuzipokea


Tathmini nimeweka, moyoni kuifungia
Kwangu nimebahatika, fadhila kunishukia
Tabu zimeniepuka, pepo nnaichezea


By Anonymous
 
Duuh
Najihisi hisi km lugha pekee nijuayo nikilugha cha kwetu tuu

Kiswahili na englishi bado majanga
 
Shairi hili ni la kwa wa ubani aumwaye.

Poa nipoe, kohoa nikohoe
Harija zote nitoe, ni bwage moyo Kaole
Zari na mgolole, wenye staha tuoe
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Maradhi faradhi, mimi yako faraji
Fadhaa ya kizazi, hari mwili si radhi
Kwa mtwana na kadhi, dhama isiyo hadhi
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Dhaifu si nuksani, afya kwetu hisani
Toka bwana manani, jamali iso kifani
Vipi tuikose shani, kwa mpito wa ubani?
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Wamezuriwa madhila, wetu wa kila kabila
Iskanda mwenye dira, jemadari aso bila
Mauko kumzingira, tama likatia hila
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Tambo konde la uduni, moto wa ujinga kuni
Madhila kwetu sabuni, kwa korija na makumi
Kutufulia zabuni, ya mwili kuurubuni
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Maisha kufingirisha, takilifu tunakwisha
Bora kuweza huishwa, kwa mahaba yasobisha
Na manani kumpisha, atufanyie aisha
Poa nipoe, nisijepiga mayowe


Kaditama nimefika, saba timilifu beti
Roho imesuuzika, chini niweze kuketi
Maneno yakikufika, uweze ree kwa cheti
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Shairi halipo sawa., kwa vina wala mizani tenzi zimechachawa mapenz tele moyoni. Mpepe hubba kidawa update raha chumbani nasema Poa nipoe nisije piga mayowe
 
Back
Top Bottom