Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Shairi hili ni la kwa wa ubani aumwaye.
Poa nipoe, kohoa nikohoe
Harija zote nitoe, ni bwage moyo Kaole
Zari na mgolole, wenye staha tuoe
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Maradhi faradhi, mimi yako faraji
Fadhaa ya kizazi, hari mwili si radhi
Kwa mtwana na kadhi, dhama isiyo hadhi
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Dhaifu si nuksani, afya kwetu hisani
Toka bwana manani, jamali iso kifani
Vipi tuikose shani, kwa mpito wa ubani?
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Wamezuriwa madhila, wetu wa kila kabila
Iskanda mwenye dira, jemadari aso bila
Mauko kumzingira, tama likatia hila
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Tambo konde la uduni, moto wa ujinga kuni
Madhila kwetu sabuni, kwa korija na makumi
Kutufulia zabuni, ya mwili kuurubuni
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Maisha kufingirisha, takilifu tunakwisha
Bora kuweza huishwa, kwa mahaba yasobisha
Na manani kumpisha, atufanyie aisha
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Kaditama nimefika, saba timilifu beti
Roho imesuuzika, chini niweze kuketi
Maneno yakikufika, uweze ree kwa cheti
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Poa nipoe, kohoa nikohoe
Harija zote nitoe, ni bwage moyo Kaole
Zari na mgolole, wenye staha tuoe
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Maradhi faradhi, mimi yako faraji
Fadhaa ya kizazi, hari mwili si radhi
Kwa mtwana na kadhi, dhama isiyo hadhi
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Dhaifu si nuksani, afya kwetu hisani
Toka bwana manani, jamali iso kifani
Vipi tuikose shani, kwa mpito wa ubani?
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Wamezuriwa madhila, wetu wa kila kabila
Iskanda mwenye dira, jemadari aso bila
Mauko kumzingira, tama likatia hila
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Tambo konde la uduni, moto wa ujinga kuni
Madhila kwetu sabuni, kwa korija na makumi
Kutufulia zabuni, ya mwili kuurubuni
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Maisha kufingirisha, takilifu tunakwisha
Bora kuweza huishwa, kwa mahaba yasobisha
Na manani kumpisha, atufanyie aisha
Poa nipoe, nisijepiga mayowe
Kaditama nimefika, saba timilifu beti
Roho imesuuzika, chini niweze kuketi
Maneno yakikufika, uweze ree kwa cheti
Poa nipoe, nisijepiga mayowe