BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mathias Pogba kaka wa Mchezaji Paul Pogba amefichua madai mengine ya kushtua dhidi ya mdogo wake ambaye ni kiungo wa kati wa Juventus, huku mgogoro kati ya ndugu hao ukiendelea.
Lakini katika kuongezea chumvi kwenye kidonda, kaka mkubwa wa Pogba alifichua kuwa mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka wa 2018, amekuwa akitumia mamilioni ya pesa katika uchawi ili kujilinda dhidi ya kupata jeraha.
“Kutokana na hayo, njia pekee ya kujinusuru ambayo mimi [Mathias] ninayo ni kufichua uwongo wake [Paul] na udanganyifu wake," alisema kama alivyonukuliwa na Get French Football News.
“Ndiyo maana nilithibitisha uchawi wake kwa sababu cha muhimu hapa si kwamba iwapo inafanya kazi au uniamini au usiniamini, ni kwamba ina nia mbaya kwa sababu uchawi huu unategemea kufanya mambo mabaya kwa matambiko yao kwa nia ya kudhuru."
“Pia, ninauliza, je, hivi Paul hakukataa kukimbilia kwa waganga? Sasa kwa nini alifichua hilo kwa mpelelezi? Pogba alikiri kwa polisi kuwa alimlipa mganga katika msafara wake kujikinga na majeraha."
"Je, kujikinga na majeraha kunahitaji kulipa mamilioni ya euro kwa mchawi huyu kwa miaka? (hasa kwa vile haikufanya kazi)," alimaka.
Hata hivyo, Paul Pogba amekanusha vikali tuhuma za kaka yake kwamba anajihusisha na uchawi.
Jina la Kylian Mbappe pia limekuwa likitajwa mara kwa mara katika sakata hilo kati ya Paul Pogba na kaka yake Mathias alifichua kwamba Pogba amekuwa akitumia uchawi kumvuruga Mbappe.
Paul kwa majibu yake ya haraka kupitia kwa mawakili wake alidai kuwa kaka yake anashirikiana na magenge ya uhalifu yaliyopangwa kumlaghai kitita cha Pauni milioni 13.