Point tatu muhimu zinazowatofautisha watu wa kanda ya ziwa Na watu wa kaskazini katika utafutaji wa pesa

Point tatu muhimu zinazowatofautisha watu wa kanda ya ziwa Na watu wa kaskazini katika utafutaji wa pesa

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Nimeishi kanda ya kaskazini miaka minne nilikuwa ninaishi Moshi mjini lakini nafanya kazi mkoa wa Arusha...Na hizi ndio point tatu muhimu Na moto wa gesi zinazowatofautisha watu wa kaskazini na watu wa kanda ya ziwa katika utafutaji wa pesa.

( 1)Ujuaji yaani kujifanya kujua Kila kitu, watu wa kaskazini hasa hata awe Na PhD nane kama bado hajajipata kimaisha au kiuchumi Huwa wana uwezo wa kujifanya mafara ili tu aweze kupata kitu flani, Na hii ni tofauti kwa ndugu zangu wa kanda ya ziwa akiwa hata Na diploma tu utamjua tu (Kiswanglish) kingi Na Huwa hawakubali kujishusha au kutafuta ujuzi zaidi wa mtaani kwa mtu aliemzidi kimaisha.

(2)Dharau, watu wa kanda ya kaskazini ni ngumu kukuonyesha moja kwa moja Dharau hata kama amekuzidi Kila kitu, mara nyingi wao Huwa wanatabia ya kumfanyia mtu wema au kumpa heshima mtu kama akiba ya baadae kwani hutambua muda wowote Alie chini kiuchumi anaweza kutoboa kimaisha Na yeye ikawa ndio point yake muhimu ya kupata zaidi au kutoboa zaidi kimaisha nadhani kwa wale ambao mmeishi uchagani mnaweza kutoa ushahidi juu ya hili.

(3)Ubinafsi, Kila mtanzania ni mbinafsi japo tunazidiana ubinafsi watu wa kaskazini anaweza kuwa mbinafsi lakini anabakiza point kidogo au nafasi kidogo akiamini muda wowote unaweza kuwa msaada kwake pale akipata shida kubwa au akikwama.hii ni tofauti kwa watu wa kanda ya ziwa akiamua kuwa mbinafsi ni moja kwa moja habakishi hata nafasi kidogo.

Mwizugukuru mgikuru Mimi mama yangu ni muhaya wa kamachumu Kagera Na baba yangu ni mchaga wa machame, Kilimanjaro kwa sadara..
 
Upo sahihi.. wachaga ni watu poa sana . Wanajua sana kuishi na watu wa aina zote

Mchaga ni rahisi sana kumchangia jirani ama rafiki yake mzaramo afanye harusi.

Ila mzaramo ni mgumu sana kumchangia mzaramo mwenzake afanye harusi.

Mchaga anajua kujishusha sana hata kama ni ana uwezo kiuchumi.

Watu wa kanda ya ziwa wanapenda kujikweza sana. Hasa akiwa na uchumi kidogo
 
Upo sahihi.. wachaga ni watu poa sana . Wanajua sana kuishi na watu wa aina zote

Mchaga ni rahisi sana kumchangia jirani ama rafiki yake mzaramo afanye harusi.

Ila mzaramo ni mgumu sana kumchangia mzaramo mwenzake afanye harusi.

Mchaga anajua kujishusha sana hata kama ni ana uwezo kiuchumi
Hapo kwenye kuishi na watu nakubaliana nawe
 
Upo sahihi.. wachaga ni watu poa sana . Wanajua sana kuishi na watu wa aina zote

Mchaga ni rahisi sana kumchangia jirani ama rafiki yake mzaramo afanye harusi.

Ila mzaramo ni mgumu sana kumchangia mzaramo mwenzake afanye harusi.

Mchaga anajua kujishusha sana hata kama ni ana uwezo kiuchumi
Wachagga sio uniform na uchaga sio kabila ni desturi fulani kwa kundi hilo, mwandishi hajakutana na wachagga jeuri, dharau na kiburi
 
Kweli wapo wachaga viburi haswa na wabinafsi
Wachagga sio uniform na uchaga sio kabila ni desturi fulani kwa kundi hilo, mwandishi hajakutana na wachagga jeuri, dharau na kiburi
Inategemea na ni mchaga wa wapi ila bado kama alivyosema mwandishi huacha akiba kidogo maana anajuwa kunakesho, ukiwa uchagani kama unywi bia pole
 
Nimeishi kanda ya kaskazini miaka minne nilikuwa ninaishi Moshi mjini lakini nafanya kazi mkoa wa arusha...Na hizi ndio point tatu muhimu Na moto wa gesi zinazowatofautisha watu wa kaskazini Na watu wa kanda ya ziwa katika utafutaji wa pesa..... ( 1) ujuaji yaani kujifanya kujua Kila kitu, watu wa kaskazini hasa hata awe Na PhD nane kama bado hajajipata kimaisha au kiuchumi Huwa wanauwezo wa kujifanya mafara ili tu aweze kupata kitu flani, Na hii ni tofauti kwa ndugu zangu wa kanda ya ziwa akiwa hata Na diploma tu utamjua tu ( kiswanglish) kingi Na Huwa hawakubali kujishusha au kutafuta ujuzi zaidi wa mtaani kwa mtu aliemzidi kimaisha. ( 3) Dharau , watu wa kanda ya kaskazini ni ngumu kukuonyesha moja kwa moja Dharau hata kama amekuzidi Kila kitu, mara nyingi wao Huwa wanatabia ya kumfanyia mtu wema au kumpa heshima mtu kama akiba ya baadae kwani hutambua muda wowote Alie chini kiuchumi anaweza kutoboa kimaisha Na yeye ikawa ndio point yake muhimu ya kupata zaidi au kutoboa zaidi kimaisha nadhani kwa wale ambao mmeishi uchagani mnaweza kutoa ushahidi juu ya hili..... (3) Ubinafsi, Kila mtanzania ni mbinafsi japo tunazidiana ubinafsi watu wa kaskazini anaweza kuwa mbinafsi lakini anabakiza point kidogo au nafasi kidogo akiamini muda wowote unaweza kuwa msaada kwake pale akipata shida kubwa au akikwama.hii ni tofauti kwa watu wa kanda ya ziwa akiamua kuwa mbinafsi ni moja kwa moja habakishi hata nafasi kidogo..... Mwizugukuru mgikuru Mimi mama yangu ni muhaya wa kamachumu Kagera Na baba yangu ni mchaga wa machame , Kilimanjaro kwa sadara..
Nilidhani Kanda ya ziwa wote.......kumbe umelenga washomiree......
 
Wachagga sio uniform na uchaga sio kabila ni desturi fulani kwa kundi hilo, mwandishi hajakutana na wachagga jeuri, dharau na kiburi
Nakubaliana na wewe mkuu , hata watu wa kagera wapo watu poa sana tu ,by the way mtoa mada ameisha wahi kutana na wabondei toka Tanga? Wenda amelinganisha makabila mawili tu ambayo amebatika ishi nayo , kuna makabila mengine yapo na mambo ya ajabu mengine cha mtoto
 
Nyongeza.
Wachagga hawana aibu kwenye kuiba fedha au mali za taasisi au kampuni. Wanapiga Cha juu, Wanaiba haswaa.
Watu wa Kanda ya ziwa wana utulivu na uaminifu zaidi.

Pia, wachagga wanapenda kusaidiana wao kwa wao ili kuinuka kiuchumi.
Kanda ya ziwa, mtu anataka yeye pekee ndiye awe wa kutukuzwa.

Tatu, wachagga ni wabahili sana. Watu ya kanda ya ziwa hawajibanibani. Wakiwa na mkwanja wanaspend kweli kweli.
 
Tusidanganyane TABIA ni hulka ya mtu siyo KABILA.

TABIA=KABILA ni vitu viwili tofauti
Kila mtu ameumbwa Kwa namna yke
Usidhani kwasababu umekutana na mchaga mwema ukadhani wachaga wote ni wema NO. au ukutane na mpare mchoyo ukadhani wapare wote wachoyo No.

Shida ya Waafrica tuna penda kujumuisha vitu ambapo kiuhalisia haitakiwi hivo.

"KABILA HALIBEBI TABIA YA MTU"
 
We jamaa labda useme wahaya ndio wana majivuno kanda ya ziwa , wasukuma kwa mikoa ya bara ndio watu poa zaidi hakuna ...Msukumu hata umdharau fresh tu ...Watu wa kaskazini ni wajivuni sana na kupenda kuweka utambulisho wao mbele hata kama sehemu sio muhimu .

Narudi tena hakuna watu wa bara wanaweza kuwafikia wasukumu kwa ukarimu ndio maana hata matajiri wa kisukumu huko migodomi ni nadra kusikia anaitwa bilionea sasa nenda kaskazini , mtu anayenunuliwa watu bi anaitwa bilionea yaani jamaa wakiingia kweny ukumbi wanataka kujulikana kwamba wana pesa , uchawa haswa wka vijana wasiojitambua .


Nimesoma nao advance na chuo mpaka leo wale wasukuma ndio rafiki zangu tutazikana inshallah , hao kaskazini kujiona wanajua sana kuna dogo nimemtema nilitaka kumuunga kweny kazi kwa kiburi cha kishmba.
 
Back
Top Bottom