Its Tesha
Senior Member
- Oct 6, 2025
- 168
- 608
Hata kama polisi wakitoa kibali, ukweli ni kwamba Watanzania wengi hawapendi kuandamana kwa sababu wanaona maandamano yamekuwa fursa ya wizi na uporaji. cocastic Ndiyo maana niliwahi kusema kuwa waliokuwa wakiandamana wengi wao walikuwa vibaka na wezi, hasa hapa mjini Dar es Salaam, wakati wazalendo wa kweli walionekana zaidi Mbeya.
Hata Mwanza na Dar, kulifanyika wizi wa mali za watu. Kama mnaona kauli zangu si za kweli, jiulizeni: jana watu walikuwa wapi? Tukisema leo tumeruhusiwa kuandamana, unadhani watu watatoka wengi? Hapana, kwa sababu hakutakuwa na fursa ya kufanya vitendo hivyo. Lucas Mwashambwa Guys, maandamano ya Oktoba 29 yalikuwa fursa kwa baadhi ya watu, hasa vibaka.
Eleweni kuwa sibezi juhudi za wale waliotoka kuandamana kwa nia njema na uzalendo wa kweli—najua walikuwepo. Lakini pia kulikuwa na wengine walioharibu taswira yote. Mimi naungana na wote wanaotaka mabadiliko, ila tuwe wamoja. Jana tuliwasaliti wenzetu waliotangulia mbele za haki; hivyo kwa tarehe mpya tusirudie kosa hilo, bali tutubu na tujipange upya. Mungu awabariki.
its tesha here!!!