greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,060
MAKALA YA 10
Karibuni tena katika MAKALA za ujenzi.Leo nataka tuangazie juu ya makosa mbalimbali yanayofanyika katika ujenzi wa majengo .1.KUNUNUA VIWANJA KATIKA MAENEO HATARISHI
Kuna watu wanataftaga majanga kabla hata ya kuanza ujenzi kwa kununua ardhi kwenye maeneo ni hatari kwa ujenzi na hawana uwezo wa kudhibiti,maeneo hayo ni kama.
- Mabonde ya mito mf.Jangwani na Kawe Makao mapya
- Ardhi yenye mfinyanzi mkali
- Mteremko mkali
- Hifadhi ya Mikoko mf Ununio na Kilongawima
- Hifadhi ya barabara za mikoa na Wilaya
- Hifadhi za nguzo za njia za umeme mkubwa,Mabomba makubwa ya maji,Gesi na Mafuta
- Hifadhi za Reli
- Maeneo ya wazi,Makaburi
- Hifadhi za Misitu na Mbuga
Utakuta mtu ana Pakua Ramani mtandaoni,ambapo
- Ramani maalum kwa mazingira ya baridi kali,
- Ramani ni ya floor ya ghorofa ila bila kujua ataitumia chino
- Ramani lazima iendane na kiwanja chako na mazingira yake.
Mtu atakuwa na Ramani,lakini hakuna mpango maalum wa matumizi katika ujenzi.
- Gharama ya Ujenzi Goba ni tofauti na Gharama za Kunduchi
- Kubaki kuuliza mitandaoni, hivi kiasi gani kinatosha,au hapa nina kiasi kadhaa.
- Kama harusi unaiandalia bajeti na kamati,basi hata ujenzi bajeti muhimu.
4.UTUMIZI WA MALIGHAFI/MATILIO MBOVU
Fundi au Mmiliki wa jengo anaweza lazima kutumia malighafi mbovu.
- Mchanga wenye chumvi
- Simenti ya kiwango duni
- Tofali za bei chee
Hapa unakuta Mmiliki au Fundi anafanya Ujenzi kwa haraka ya ajabu
- Kuta hazitokauka vizuri,mwishowe kutu
- Slab za zege kunepa
- Nguzo kulala
6.KUJENGA KIPINDI CHA MVUA
Haishauriwi mtu ujenge kipindi cha mvua kwani.
- Matofali huongezeka uzito
- Mortar ni ngumu kukauka
- Zege litakuwa na maji mengi
- Unyevu huathiri mambo mengi hata shughuli za ndani ya jengo,gypsum
Kuna Watu huweka ubahili mbele kuliko tajwa la ubora wa jengo,yani yupo radhi kutumia pesa nyingi kwenye sherehe kuliko ujenzi
- Atatumia fundi uchwala
- Atanunua matilio feki
- Atafuata ushauri wa watu wasio na taaluma
Kupanda miti karibia na jengo au uzio nalo ni suala hatarishi.
- Miti husababisha nyufa
- Miti Hupunguza mwanga kupita kwenye jengo
- Miti husababisha unyevu katika kuta
- Miti huzuia upepo
9.WATAALAM/MAFUNDI
Kwenye wataalam wa ujenzi huwa kuna makosa kadhaa nayo huwa wanafanya
- Tamaa: Mwishowe huwaibia wateja wao
- Kutojiendeleza kielimu: Wakisha maliza vyuo au miaka 10 kwenye ujenzi hudhani anamudu kila kitu
- Shirikisha mtaalam katika kila hatua,kuanzia umiliki wa kiwanja
- Tambua ujenzi ni hatua, siyo lazima ikamilike ndani ya mwaka
- Tumia mafundi bora na matilio bora
Unaweza tuma za sehemu jengo lako lenye tatizo...
Heri ya Sikukuu ya Muungano 🥳👫