greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,060
MAKALA YA 10
Karibuni katika Makala pendwa ambapo tunajadili mambo mbalimbali kuhusiana na ujenzi.Leo tuangazie kwenye kipengele cha Uchaguzi wa rangi(Colour) ya matilio ya kumalizia/finishing jengo Lako.
1.RANGI : ni ule ubainifu au ujuaji wa miale ya mwangaza inapoingia katika kitu fulani.
Kila matilio lazima iwe na rangi,ambazo husaidia kutifautisha matilio moja kutoka nyingine.
- Aina kuu za Rangi : Bluu,Nyekundu na Njano
- Rangi Upili: Zambarau,Machungwa,Kijani
- Rangi nyinginezo : Khaki,Kahawia,Damu ya Mzee,Samawati n.k
2. Mambo makuu ya kuzingatia katika uchaguzi wa Rangi.
A. MTINDO WA USANIFU(MUONEAKNO WA JENGO)
- Mtindo wa Kiislam (Islamic Architecture) hupendelea zaidi finishing za rangi Nyeupe,Bluu,Dhahabu au Kijani
- Mtindo wa Mediterranean hupendelea rangi ; Nyeupe ,Tan,Njano yenye udhahabu, Damu ya mzee,Machungwa na Kijani yenye uweusi
- Mtindo wa Kisasa (Modern),hupendelea rangi Nyeupe,Kijivu,Bluu,Khaki na
3.
B: MWANGA ASILI
Kiwango cha mwanga kinachopiga jengo, na upande ambao mwanga huo unatoka husaidia katika uchaguzi wa aina ya rangi...
- Upande wenye kupata mwanga kidogo,utafaa kwa rangi zenye kung'aa /kali.
- Upande wenye mwanga mwingi, uwe na rangi zilizopo.
C: MANDHARI YA JENGO
Mandhari ya jengo husaidia katika kuamua aina ya rangi katika Jengo lako
- Rangi yenye kufanya jengo lionekane zaidi kuliko mandhari
- Rangi yenye kujificha jengo
- Rangi yenye kufanya jengo liendane na mandhari
- Mandhari hizo huweza kuwa :Nyumba jirani,Miti,Miinuko,Fensi,Ardhi
5.
D: MATUMIZI YA NJENGO
Kuna mda matumizi ya Jengo husika huamua rangi zitakazo faa kutumika.
- Kanisa + Msikiti = Rangi nyeupe
- Hospital = Samawati
- Nursery = Njano,Zambarau,Machungwa
- Mahakama = Khaki, Nyeupe
- Polisi = Bluu iliyo kolea.
E: MWANGA WA TAA
Mwanga wa taa pia unaweza ukawa muamuzi wa pendekezo la rangi....
- Taa nyingi huwa za rangi ya Unjano,Bluu au mwanga mweupe
- Taa za njano hubadili rangi ya Bluu kuwa Kijani na mwekundu kuwa machungwa.
- Ndani ukiweka rangi ya Bluu,jua zikipiga Rangi nyekundu inaonekana ya Zambarau.
F: PAA
Wengi huja kufkiria rangi ya jengo, baada ya kuwa tayari ameshaweka rangi ya paa.
Hakikisha rangi ya Jengo lako ,zirandane na rangi ya paa.
- Paa la rangi jekundu, litaendana na jengo lenye rangi ;Ukijani,Orange,Pink
F : LADHA YAKO.
Lakini mwisho wa siku,rangi ya Jengo lako huweza kuamuliwa na ladha ya mmiliki,
Kama mmiliki ni mpenzi wa rangi fulani anaweza kuchagua hiyo rangi.
Mwengine hupenda rangi ya Jengo ifanane na gari yake...
9.Katika uchaguzi wa rangi
- Usifanye uchaguzi wa Rangi kwa kuangalia vikaratasi vilivyo printiwa pindi uendapo duka la vifaa vya Ujenzi.
- Jaribisha muonekano wa rangi kwa kupaka kwenye kipande kikubwa cha boksi/mbao na kuweka usawa wa ukuta
- Angalia muonekano wa rangi katika nyakati za siku.
Idadi ya rangi na muingiliano wa rangi nayo ni kitu muhimu kukiweka akilini, usije kuwa na jengo lina rangi kama Discolight
Nakaribisha Maoni na Maswali