Points 10 za ujenzi: Unyevu/damp katika jengo

Kiongozi hiyo Damp proof course inauzwaje ? kwa mita au na shilingi ngapi kwa bei ya Mtanzania mnyonge?
 
Mkuu
Kwa ile ambayo ni raising damp na ndio umeshajenga, naweza kutumia tiba gani
 
Damp Proof Course,ni ile level ambayo huwa ina vidhibiti unyevu, huwa kabla au baada ya Msingi.
.Kuna aina nyingi za Damp Proof kwenye msingi.lakini ambazo zinaweza tumika.

1.Matofali maalum
-Matofali ya udongo yenye kushindiliwa vizuri na kuchomwa sana haya yanaweza tumiwa kama Damp Proof.
-Matofali ya block yaliyoandaliwa uwiano/ratio kali ,kushindiliwa vizuri na kuachwa juani mda usiopungua siku 20
-Hapa gharama ya kila tofali moja la kuchoma inaweza kuwa 250 hadi 300 na tofali la block itakuwa 2500 hadi 3000
-Angalizo:Mhandisi ujenzi : lazima ahusike kwenye uhandaaji

2.Damp Proof membrane (D.P.M)
-Hii ni sheet kubwa la Polyethylene, ambayo hulazwa kabla au baada ya mkanda wa zege wa chini...
-Ina urefu wa mita 100 hadi 120,, Upana wa mita 1 na uzito wa Kg 50,
-Linakuwa limebingilitwa,
-Huuzwa linauzwa 100,000 hadi 120,000
-Gerezani,Buguruni,Tegeta

3.Kemikali :hapa Kuna kemikali za kuchangwa kwenye Mkanda wa zege
-Bidhaa za Sika,Cyprex
-Huuzwa kuanzia 150,000 hadi 500,000 kwa ndoo ya lita 15.

ANGALIZO
-Kuna watu huwa wanaweka Nailon,hii siyo mbinu bora kwani Nailoni ni nyembamba sana na raisi kutoboka wakati wa ujenzi.
 
Asante mkuu. Kuukomoa unyevu natamani kupiga 1 na 2 zote zitumike
 
Mkuu
Kwa ile ambayo ni raising damp na ndio umeshajenga, naweza kutumia tiba gani
1.Asili ya Udongo wako ni Ipi ,Kichanga, Tifutifu, Mfinyazi
2.Sehemu iliyoathiriwa ni ipi,Ukuta wa upande Upi au Kuta zote?
3.Je eneo lako lina kawaida ya kutuwamisha maji
4.Je, Ukuta ni umelowa tu,au kuna sehemu ishaanza kuathiriwa na chumvi.
5.Eneo lina umbali gani kutoka baharini
6.Kuna kisima kwa karibu.

Majibu yako yatasaidia kukupa ushauri...
 
Asili ya udongo ni tifutifu.
Ni ukuta wa upande yaani kona moja ya nyumba kiasi cha mita 4 pande zote kutoka kwenye kona.
Eneo hili mwaka huu ndio nimeona maji yakituama baada ya ujenzi. Though naambiwa miaka ya nyuma kulikuwa na maji.
Umbali wa Bahraini unafika km 6

Hakuna kisima kwa karibu. Niliwaza kuchimba ili kupunguza hii hali.
Asante
 
Mkuu
Kwa ile ambayo ni raising damp na ndio umeshajenga, naweza kutumia tiba gani
Tiba zipo za aina nyingi...
Ila kwanza kabla haujatibu lazima udhibiti/kupunguza kasi ya Unyevu kupanda.
Kwa maana unaweza fanya marekebisho ukutani lakini maji yanapanda kama kawaida....kwahiyo tatizo linakuwepo kila mwaka.
 
Asili ya udongo ni tifutifu.
Ni ukuta wa upande yaani kona moja ya nyumba kiasi cha mita 4 pande zote kutoka kwenye kona.
Eneo hili mwaka huu ndio nimeona maji yakituama baada ya ujenzi. Though naambiwa miaka ya nyuma kulikuwa na maji.
Umbali wa Bahraini unafika km 6

Hakuna kisima kwa karibu. Niliwaza kuchimba ili kupunguza hii hali.
Asante
A..Basi hapo moja kwa moja chanzo cha tatizo kipo kwenye hayo maji...Maji yatakuwa yanatuwama hapo kwenye huo upande wa nyumba kwa chini....

B.Kudhibiti kutuwama kwa maji.
*Kama unajua maji yanapotokea weka mfumo wa Mabomba wa ku-divert njia ya maji yasiingie kwenye eneo lako.

*Kama haujui maji yanapoingilia, nenda karibu na huo upande wa ukuta, na weka mfumo wa mabomba utakao kuwa unatoa maji na kuya peleka nje.

C:TIBA
*Kwanza ,Je,uliweka Damp Proof course.?
 
Asante.Nakumbuka nyumba nyingi za Mikocheni zinabanduka plasta na rangi na kuta zinakuwa za unyevunyevu muda wote. Ungekuwa umemalizia kwa kuandika solution ingependeza. Usitoe mafundisho ya vitisho kama hawa ''manabii. wa kileo wanavyotishia waumini juu ya majini na wanga, vibwengo na vinyamkera halafu wanaambia suluhisho waende kwenye makanisa yao wanayoyaongoza.
Sababu za Unyevu Mikocheni...
Mikocheni...
-Ipo altitude ya Mita 0.5 hadi 1.5
-Mwamba wa kuzuia maji (water table) upo karibu na uso wa ardhi /surface.
/surface.
-Ipo umbali wa Km 2 hadi 4 kutoka baharini...

Na ndiyo maana Kwa Mikocheni, ukichimba shimo la Mita 1 hadi 1.5 utakuta mimaji, tena maji ya chumvi...
Ndiyo maana wana vyoo ghorofa.
 
Mwezi wa 4 naingia likizo
Kwa mwenye kuhitaji kutembelewa katika eneo lake, kukagua na kutoa ushauri juu ya tatizo lolote, kuwa huru kunijuza.

Gharama : Huduma hii ni bure
Usafiri : ndiyo pekee utagharamia.
 
Mkuu,kwanza Asante sana Kwa elimu nzuri uliyotupatia. Ingawa nilichelewa kuijua hii kabla sijajenga lakini bado sijachelewa sana.
Naomba unisaidie hili,nimejenga nyumba yangu kwenye udongo wa mfinyanzi na nililoweka ni Ile nylon nyeusi kwenye msingi kabla ya tofali,Sasa naelekea kupiga plaster. Naomba unishauri tufanye nn wakati wa kupiga plaster ili tudhibigi uwezekano wa fungus kwenye ukuta. Msaada wako ni muhimu sana kwangu.
Natumia local fundi.
Mwezi wa 4 naingia likizo
Kwa mwenye kuhitaji kutembelewa katika eneo lake, kukagua na kutoa ushauri juu ya tatizo lolote, kuwa huru kunijuza.

Gharama : Huduma hii ni bure
Usafiri : ndiyo pekee utagharamia.
 
Unyevu ni maji yaliyo kwenye kuta za jengo, na Fangasi ni viumbe vinavyokuwa kwenye huo Unyevu....(Ukijani,Weusi au Unjano)

1.Kuna ukuta ulio karibu na nyumba yako, ukuta wa jirani au fensi yako
2.Kuna Mti ulio karibu na nyumba yako.
3.Paa lako ni kujificha ama?
4.Tanki la maji lipo karibu na nyumba
5.Una slab juu ya kibaraza cha Verandah yako.?
6.Kuna njia ya maji karibu na kwako...?

Nahitaji majibu ya hayo maswali kwanza.
 
1. Sina ukuta uliona karibu na jengo langu ingawa nitakapojenga fence upande Mmoja fence itakuwa karibu na nyumba Kwa upana wa 1.5metres.
2. Hakuna mtu uli karibu.
3. Hapana.
4.Hapana.
5.hapana.
6.hapana ila aina ya udongo wake ni mfinyanzi.
 
1.Hakikisha maji ya mvua hayagusi ardhi karibu na msingi,
Yaani zungusha kibaraza.

2.Anda mfumo mzuri wa kukusanya maji ya mvua...

3.Plaster iwe na ratio nzuri ,,Isiwe tepe sana...
4.Plasta iwe na unene wa kutosha 10-15 mm
5.usioteshe miti mikubwa karibia na nyumba,miti ianzie umbali wa mita 5

6.Fensi isizidi kozi 8,,
Huo upande wa Fensi kuwa karibu na ukuta...ndiyo wa kuuangalia sana.
 
Nashukuru sana mkuu,je Kuna dawa yoyote napaswa kuchanganya na cement wakati wa kupiga plaster?kama jibu ni ndiyo,je ni dawa Gani inafaa zaidi? Maana mafundi wanatuchanganya sana.
 
Kuna Document nakutumia, Kuna mtu nilimfanyia ukaguzi...
 
Back
Top Bottom