greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,060
MAKALA YA 7
Karibu katika Makala yenye kukuhabarisha mambo kadhaa Juu ya Ujenzi,leo tunaangazia japo kwa ufupi juu ya "Nyufa"1. Nyufa ni mpasuko/Mipasuko inayojitokeza katika sehemu ya jengo I.e Ukuta,Nguzo,beam au msingi.
-Nyufa ni tatizo la pili kwa ukubwa linalokumba majengo ukiachana na Unyevu.
2. Kuna makundi mawili ya nyufa...
I) Nyufa zenye kuathiri mhimili wa jengo.
-huwa ni kubwa,zaidi ya mm 2.
II) Nyufa zisizo athiri mhimili wa jengo.
-upana wake hazizidi milimita 1.
*Nyufa inaweza kuwa ya imesimama wima,zimelala au zenye kuweka mchoro wa ngazi.
3. Mambo yanayopelekea Nyufa kutokea ni kama yafuatayo..
A: KIWANGO CHA UNYEVU KWENYE MATILIO
- matofali ya udongo baada ya kutoka kuchomwa, yakipata maji hutanuka.
- Kuna matilio baada ya ujenzi usinyaa
- Matilio zote za ujenzi hutanuka na kusinyaa kulingana na joto
- Kuna kokoto zina Kemikali ambazo hazitakiwi kukutana na Simenti
- Ukaribu na njia ya reli
- Mitetemo ya ardhi
- Ukaribu na barabara na uwanja wa ndege
- Mimea
- Mfinyanzi,Kichanga
- Kutuwama kwa maji.
- Jengo kuwa na urefu uliopitiliza
- Jengo kuwa na Uzito ulio pitiliza
4. Nyufa katika sehemu tofauti za Jengo....
A. Katika LINTEL/BEAM,,hapo labda
- Zege ina mchanganyiko mbovu
- Umetumia nondo chache
- Size ya Lintel ni ndogo
- Mzigo uliopo juu ni mzito
- Lintel itakuwa imseinyaa/imejivuta
- Lintel itakuwa kwenye dirisha pana kuliko, ikazidiwa uwezo.
- Mzigo mwingi upo katikati kuliko mwishoni