Points 10 za ujenzi wa nyufa katika majengo

Points 10 za ujenzi wa nyufa katika majengo

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
MAKALA YA 7
Karibu katika Makala yenye kukuhabarisha mambo kadhaa Juu ya Ujenzi,leo tunaangazia japo kwa ufupi juu ya "Nyufa"

1. Nyufa ni mpasuko/Mipasuko inayojitokeza katika sehemu ya jengo I.e Ukuta,Nguzo,beam au msingi.
-Nyufa ni tatizo la pili kwa ukubwa linalokumba majengo ukiachana na Unyevu.

2. Kuna makundi mawili ya nyufa...
I) Nyufa zenye kuathiri mhimili wa jengo.
-huwa ni kubwa,zaidi ya mm 2.
II) Nyufa zisizo athiri mhimili wa jengo.
-upana wake hazizidi milimita 1.
*Nyufa inaweza kuwa ya imesimama wima,zimelala au zenye kuweka mchoro wa ngazi.

3. Mambo yanayopelekea Nyufa kutokea ni kama yafuatayo..

A: KIWANGO CHA UNYEVU KWENYE MATILIO
  • matofali ya udongo baada ya kutoka kuchomwa, yakipata maji hutanuka.​
  • Kuna matilio baada ya ujenzi usinyaa​
B. MABADILIKO YA JOTO
  • Matilio zote za ujenzi hutanuka na kusinyaa kulingana na joto
C. MCHANGANYIKO WA KEMIKALI
  • Kuna kokoto zina Kemikali ambazo hazitakiwi kukutana na Simenti
D. MAZINGIRA YA ENEO
  • Ukaribu na njia ya reli
  • Mitetemo ya ardhi
  • Ukaribu na barabara na uwanja wa ndege
  • Mimea
E: ASILI YA UDONGO
  • Mfinyanzi,Kichanga
  • Kutuwama kwa maji.
F. SANIFU MBOVU.
  • Jengo kuwa na urefu uliopitiliza
  • Jengo kuwa na Uzito ulio pitiliza

4. Nyufa katika sehemu tofauti za Jengo....
A. Katika LINTEL/BEAM,,hapo labda
  • Zege ina mchanganyiko mbovu
  • Umetumia nondo chache
  • Size ya Lintel ni ndogo
  • Mzigo uliopo juu ni mzito
B. PEMBENI YA LINTEL
  • Lintel itakuwa imseinyaa/imejivuta
  • Lintel itakuwa kwenye dirisha pana kuliko, ikazidiwa uwezo.
D. CHINI YA SLAB
  • Mzigo mwingi upo katikati kuliko mwishoni
 
4.
F.NYUFA KATIKA SAKAFU,
Hapo labda
  • Eneo lina udongo wa mfinyanzi,umetanuka na kusukuma juu sakafu
  • Eneo lina kichanga,baa ya kukauka ukashuka, na sehem ya sakafu ikashuka.
  • Sakafu kuwa ndefu kuliko
  • Sakafu kutoandaliwa vizuri.
G.NGUZO,hapo labda
  • Mchangayiko mbovu wa zege
  • Nondo chache,
  • Mzigo mzito
  • Usukaji mbovu wa Nondo
  • Kutu kwenye Nondo
5.
KATIKA KUTA
  • ukuta kuwa mrefu kupindukia
  • Utumizi wa matofali mbovu
  • Ukuta kubeba mzigo kupitiliza
  • Kuta kuchoma
  • Chumvi
  • Ujenzi mbovu
  • Mtikisiko na mitetemo
6.Hatua za Kujikinga na Nyufa (Kabla ya Ujenzi)
  • Ita mtaalam akague eneo lako kabla ya ujenzi
  • Epuka ununuzi wa maeneo korofi kama hauna kipato kikubwa
  • Ondoa miti na Mizizi yote kabla ya ujenzi.
7.Hatua za Kujikinga na Nyufa kipindi cha Ujenzi.
  • Tumia matilio zenye ubora mf. Kokoto ngumu,mchango usio na chumvi
  • Tumia mtaalam japo kwenye ushauri.
  • Tumia fundi mzuri
  • Mahitaji yazingatiwe, kwenye nondo nne ,Zikae nne
  • Usijenge kwenye msimu wa mvua
  • Epuka ujenzi wa haraka sana
  • Beam kwenye plinth na level ya lintel ni muhimu
  • Zege iandaliwe vyema, iachwe ikauke vizuri
  • Maji ya kupoza ujenzi yamwagwe kwa mda wa siku 7.
8.Unapoona Nyufa,fanya yafuatayo...
-Sikilizia kwanza kwa mda wa miezi mitatu,ili kuona imekua zaidi ama lah.
-Angalia ukubwa wa Nyufa
-Kama ni Kubwa ita mtaalam aje akague kabla marekebisho yoyote.

9.Umakini wahitajika katika utatuzi wa Nyufa,la sivyo utaishia kuweka vilaka kila msimu.

10.Kuna vyanzo vingi sana vya nyufa ,nasisitiza kama unaona zinajirudia, ita mtaalam

Nakaribisha maswali ,maoni na mapendekezo.

Mwenye kuhitaji kufanyiwa ukaguzi wa eneo au jengo lake, kuwa huru kunijuza...

EID MUBARAK
 
20240405_164754.jpg

Hapo kaweka Beam chini cha ukuta ila shida yake ni.
  • Ukuta ni mrefu sana,nilipima nikaona una mita 4.8.
  • Beam imezidiwa,uzito mwingi upo hapo kati.
  • Beam inapinda kwenda chini inaleta nyufa hapo juu
 
20240405_165146.jpg

Huyo hapo
  • Mchanganyiko wa zege ni mbovu,maji yalikuwa mengi.
  • Kwahyo zege ilivyoanza kunyauka, ikaacha nafasi/vitundu vidogo vidogo
Pia
  • Nondo zimewekwa karibu na nyuso/surface ya zege.
  • Ilipopigwa joto ikatanuka, ikaunda nyufa
  • Pia rahisi kunyonya maji na kuweka kutu na kutanuka
 
20240319_174416.jpg

Hapo wameziba nyufa kwa kuchapia...
  • Eneo lina udongo wa mfinyanzi
  • Msingi wake ni mfupi
  • Hajaweka hata mkanda wa beam wenye kusaidia kuzuia mpasuko
  • Hapo njia bora ni kudhibiti maji yasiguse udongo karibu na msingi na si kuchapia ovyo
 
Mimi kwangu paa linavuja ajabu… limefanyiwa marekebisho mara kadhaa na baadaye kuoauliwa tena lkn zote zimekuwa suluhu za muda mfupi.. Mvua ya mwaka huu ilikiwa yetu
 
Back
Top Bottom