BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Poland imezungumzia tukio lililotokea usiku wa Septemba9-10, 2025 ambapo imedai Urusi ilirusha takriban Droni 20 kuingia katika anga ya Poland, baadhi zikitokea pia Belarus na kwamba tukio hilo ilikuwa operesheni iliyopangwa, iliyodumu zaidi ya saa saba, ikihusisha droni za kuvutia adui zenye uwezo wa kwenda umbali mrefu.
Poland imeeleza kuwa Jeshi lao la Anga pamoja na washirika wao wengine (Uholanzi, Ujerumani, Italia) walijibu kwa weledi, wakidhibiti tishio hilo na kuangusha baadhi ya droni zilizolengwa.
Mkuu wa Kituo cha Ubalozi wa Poland, Sergiusz Wolski akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, Septemba 25, 2025, amesema “Majibu yetu kwa uchokozi huu yalikuwa ya utulivu na ya kupimwa. Kwa ombi la Poland, NATO ilifanya mashauriano chini ya Kifungu cha 4. Vitendo vya Urusi vinatufanya kuimarisha uwezo wetu wa kujilinda na kuunga mkono sera ya NATO ya kuzuia na kujilinda.
Mkuu wa Kituo cha Ubalozi wa Poland, Sergiusz Wolski
“Tulimwita Kaimu Balozi wa Urusi katika Wizara ya Mambo ya Nje huko Warsaw na tukamkabidhi barua ya kupinga. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia lilifanya mjadala kwa ombi letu.
“Lengo la Urusi ni kuvuta nchi nyingine kuingia vitani, ikiwemo Poland. Hatutachokozwa, lakini tutaendelea kuhakikisha usalama wa anga letu na raia wetu.”
Droni zikijitokeza tena
Aidha, Poland imesema mashambulizi hayo ya Dorone hayakuwa na madhara kwa Wananchi wao lakini yalisababisha hofu na kuharibu baadhi ya vitu, na kwamba kama kutatokea vita yanaweza kutokea yale ambayo yametokea kwa majirani zao Ukraine ikiwemo uharibifu wa miundombinu na vifo vya watu wengi kutokana na vita dhidi ya Urusi.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Poland imenukuliwa hivi karibuni ikisema kuwa itazishambulia Droni zitakazojitokeza bila kuwa na taarifa au maelezo rasmi katika anga yao.
Kuhusu Vita
Aidha, Poland imeeleza kuwa Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine Mwaka 2022 bila uchokozi wowote ulikuwa mwendelezo wa mzozo ilioanzisha Mwaka 2014, ambao sasa umedumu zaidi ya Miaka 11.
Bwana Sergiusz Wolski ameeleza kuwa “Rais Julius Nyerere alisema: ‘Hakuna taifa lenye haki ya kufanya maamuzi kwa niaba ya taifa jingine; hakuna watu kwa ajili ya watu wengine. Vurugu si ya lazima na ni ya gharama kubwa. Amani ndiyo njia pekee.’ Maneno haya yanaendana vyema na vita vya uchokozi vya Urusi dhidi ya Ukraine.
Ameongeza kuwa Urusi inajaribu kulazimisha matakwa yake kwa taifa jingine huru. Vita ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Vitendo vya Urusi ni uhalifu dhidi ya amani, na majeshi yake yanaendelea kufanya uhalifu wa kivita.
“Urusi haitendi kama mshiriki mwenye kuwajibika katika jumuiya ya kimataifa. Kwa miezi mingi imekuwa ikifanya operesheni za mseto katika eneo hili, ikiwa ni pamoja na kuzuia mfumo wa GPS, kukata nyaya za chini ya bahari, kuchoma moto kwa makusudi, kampeni za upotoshaji wa taarifa, na mashambulizi ya kimtandao,” amesema Bwana Sergiusz Wolski.
Pia soma ~ Poland: Russian Attacks on Us Are Provocations Aimed at Dragging Other Countries into War