STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,633
- 16,586
Vita vimeiharibu vibaya Ukraine, sasa Poland imeikatia mafuta ya bure.
Wakati nchi za Ulaya zikiendelea kudai kuwa ziko pamoja na Ukraine kwa hali na mali na kwamba ziko tayari kuisaidia nchi hiyo iwapo Russia itafunga bomba lake la gesi isiingie Ukraine, sasa hivi nchi jiran ya Poland imesema haina mafuta ya bure ya kuipa Ukraine.
Shirika la habari la FARS limemnukuu Waziri wa Mazingira wa Poland, Bi Anna Moskwa akitangaza hayo jana na kuongeza kuwa, nchi yake imeamua kusimamisha kuipa Ukraine mafuta ya bure, lakini mafuta ya kununua yataendelea kupelekwa Ukraine kama kawaida.
Waziri huyo wa Poland amesema, kipaumbele cha kwanza cha nchi yake ni soko la ndani ya Poland. Wananchi wa Poland ndio muhimu kuliko wa nchi nyingine, amesema. Sasa Poland itakuwa inaiuzia mafuta Ukraine kupitia shirika la PKN Orlen.
Anna Moskwa, Waziri wa Mazingira wa Poland
Waziri wa Mazingira wa Poland pia amesema, mashirika ya mafuta ya Ukraine yanapaswa yajitegemee yenyewe. Inabidi yatambue hali halisi ilivyo, hivyo yaendane na hali hiyo. Amesisitiza kwa kusema: Mafuta ya bure tuliyokuwa tukiipa Ukraine yalikuwa ni majibu ya mgogoro wa vita vya Russia na nchi hiyo, lakini hivi sasa kumefanyika mabadiliko. Ukraine inao uwezo wa kununua mafuta. Hivyo itabidi ilipie mafuta inayopewa na Poland.
Ilikuwa imejulikana tangu zamani kuwa, Poland itavunja mkataba wake na shirika la Russia la Gazprom kabla ya kufikia mwisho. Mkataba baina ya Poland na Russia unaipa Poland mita-cubic milioni 10 za gesi ya Russia kila mwaka.
Hivi sasa Poland inahitaji kujaza pengo hilo kupitia kununua gesi kutoka Marekani na nchi za Kiarabu pamoja na gesi asilia kutoka Norway. Lakini inaonekana itaendelea kuwa na upungufu wa nishati, hivyo imeiambia wazi Ukraine kwamba haina tena mafuta ya bure ya kuipa nchi hiyo.