Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kila raisi akipata fursa kuzungumza kwenye baraza la Umoja wa mataifa husema yale yaliyojificha moyoni.Hivyo ndivyo alivyofanya raisi wa Poland Andrzej Duda jana tarehe 19 ilipofika zamu yake.
Katika hotuba yake hiyo aliendelea kutetea uamuzi wa nchi yake kutoruhusu nafaka zote za Ukraine kuingia au kupita nchini mwake kuelekea nchi nyengine.Uamuzi huo umemkasirisha sana raisi Zelensky na hata kupeleka malalamiko yake kwenye baraza la biashara la dunia.
Akiendelea kufafanua msimamo huo raisi Duda alisema kila mtu anajua hatari ya kujaribu kumuokoa mfa maji.Anaweza akakuzamisha pamoja naye mpaka chini kabisa.
Tangu vita baina ya Urusi na Ukraine vianze Poland amekuwa ni mshirika na mtetezi mkubwa wa nchi hiyo jirani mpaka katika miezi ya hivi karibuni ambapo nchi hiyo imeonekana kubadili msimamo wake pakubwa.