Kuna siku utanielewa Jasusi.
Najaribu kuchangia, japo kiduchu, kujenga ka jamii fulani nchini kwetu ambako kanafanana fanana na kule tunakokimbilia. Nina uchungu mno na nchi yetu, nikisikia, kwa mfano, hayo ya nepotism, yananiuma mno.
Unaenda nchi ya watu, huna mjomba, huna Mama, huna mfadhili, huna ndugu, unaanza maisha, unatafuta kazi unapata bila ki-memo, bila ma connection, why, how? Sana sana watacheka "your name is funny, where're you from," lakini utagombania hiyo kazi kama wenyeji, utapata au kukosa kama wenyeji. How, why? Why not us?
Halafu sisi, Jasusi, ndio tunasema tuna mizizi ya Ujamaa, lakini ndo wa kwanza kubaguana, why...why... why???
By the way, nadhani foreign affairs ni moja ya wizara inayoongoza kwa nepotism.