Pole FL1...

Pole FL1...

Raha ya Milele Umpe ee bwana, na Mwanga wa Milele umuangazie, Apumzike kwa Amani. Amina
 
poleni wafiwa Mungu awape nguvu wakati huu mgumu sana.
 
msiba umetokea Mwanza lakini bado sijui mazishi yatakuwa wapi. Kwa kadiri nilivyosikia ni kuwa ni yule rafiki wa "kufa na kuzikana" kwa hiyo ni pigo kubwa kwake.

Nimeongea na FL1 muda si mrefu, Marehemu ni rafiki yake tangu utotoni. Tena ndiye aliyemsimamia kwenye harusi yake. Unaweza ukahisi pigo lililompata ndugu yetu huyu.
Pole sana binamu yangu FL1.
 
pole sana.....!ninakumbuka sana jumapili namna ulivyokuwa stressed wakat rafikiyo akiwa katika hali mbaya.

nakumbuka mambo mengi zaidi,MUNGU AKUTIE NGUVU MAMA
 
Habari zimenifikia kuwa dada yetu FL1 amempoteza rafiki yake wa karibu mapema leo. Naomba kutoa pole zangu kwake na kwa familia ya rafiki yake huyo kwa msiba huu. Tunamwomba Mungu awafariji familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na ailaze pema peponi, roho ya marehemu, Amina
Too Bad!
I call it a disaster!
Hakuna kipimo cha uchungu wa kupotelewa na mtu wa karibu!
Lakini acha nikupe siri..KUNA TUMAINI!...Hawa ndugu zetu wanaopotea iko siku tutawaona, usokwauso, tena katika utukufu Mwingi sana, na tena itakuwa ni milele!..Hivyo cha maana kwa sasa ni kusali na kuomba ili tumaini hilo litimilike kwako na kwake!
Pole shemeji langu!
 
Kila kilichoumbwa na uhai, hakina budi kufa. Dunia ni mapito. Weka maisha yako katika Bwana uwe na tumaini la uzima wa milele.

Pole sana FL1, tupo pamoja katika kipindi hiki cha majonzi.
 
Pole FL1 nimekufahamu muda mfupi tu kupitia post zako my dada lakini nauona ukaribu wako kwa watu ..Mungu akupe nguvu na ujasiri katika hili ..najua urafiki washinda undugu mpenzi..
Mungu awatie nguvu
EW
 
Pole mydia ni wakati mgumu, lakini sisi tukupendao tuko nawe. RIP marehemu.
 
Nashukuru sana Mwanakijiji kwa bandiko lako lakini sijui hizi habari umezipata wapi ...Ni kweli nimeondokewa na mpendwa wangu wa moyo alikuwa ni rafiki yangu wa karibu,alikuwa ni ndugu yangu alikuwa ni kila kitu kwangu lakini mwenyezi mungu kampenda sana na kumuita kwa muda aliomuhitaji yeye..Najua wote hapa duniani tu wapitaji ..ni vyema tuwe tayari kila saa na kila siku kwani hatujui siku wala saa
naona ni jinsi gani mnanipenda na kunijali..kwa sasa sitaongea kitu chochote msiba utakuwa mwanza ..sina uhakika kama itakuwa kesho ..lakini nitawafahamisha itakavyokuwa
Nawapenda wote
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe zaidi
 
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe zaidi

Dah pole sana FL1 tupo pamoja katika hiki kipindi kigumu mwenyewe nimepoteza rafiki wa mchumba angu humo humo. Lihimidiwe jina la bwana. Amina.
 
Nashukuru sana Mwanakijiji kwa bandiko lako lakini sijui hizi habari umezipata wapi !
Dunia hii kwasasa ni ndogo sana!...huh!

Kwetu wanasema.."nyumba yenye matanga haifichiki" , na habari za msiba husambaa kama moto wa nyikani!
 
Dah pole sana FL1 tupo pamoja katika hiki kipindi kigumu mwenyewe nimepoteza rafiki wa mchumba angu humo humo. Lihimidiwe jina la bwana. Amina.

hivi shem unaweza kuwa na msiba na umenyamaza hivihivi tuu?
 
Back
Top Bottom