chawa wa mama
JF-Expert Member
- Jun 8, 2020
- 292
- 1,084
Miaka ile wakati Dr. Kiiza besige akipigwa hadharani na polisi wa Uganda huku wakimweka kizuizini wakati wa kampeni na katika maisha yake ya kawaida, kwa kosa la kushiriki siasa na kugombea nafasi ya urais, niliwaona waganda ni wajinga.
Nilikuwa najiuliza inakuwaje Waganda wengi ambao ndio wanapenda chama mbadala kiingie madarakani wakubali mgombea wao apigwe hadharani? Niliwaona hamnazo sana.
Mambo yamebadilika sana, niliwakosea waganda. Niliwahi kuwakejeli kwenye mitandao yao kule kuwa ni 'wanawake dhaifu'. Leo yamenikuta mie sasa. Napata ubatizo wa moto wa jahanamu. Sijui hata hatma yangu. Nina miaka 5 home na ka degree kwangu ka mass administration.
"Aliyejipa nchi" hana mpango na wananchi wake, mtemi ile hakuna mfano, hasikii la mnadi swala. Hakika niliwakosea sana waganda wakati ule.
Lakini pia nawaona awamu hii bwana mdogo Chakulani anayopitia, msalimieni Museveni mwambie ni alikuwa Bokasa, Mobutu, Iddi Amin, Mugabe, Gadafi, lakini wote hawapo na hawana heshima tena hata makaburi yao.