Pole sana Rais Samia kwa kuhujumiwa

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,625
Reaction score
3,141
Ukweli ni kwamba, Mama anahujumiwa sana tena sana. Tukumbuke kuwa Mama anapohujumiwa, Nchi ndo inayohujumiwa. Nchi inapohujumiwa, Watanzania wote mmoja wanahujumiwa kwa kukosa huduma za kijamii.
Lakini ni akina nani wanakuhujumu?

Ni wale wale uliowapa nafasi katika utawala wako. Kwa mfano, kuna mradi wa Tshs. 500,000,000/=
Kitakachofanyika hapo ni kugawana hizo fedha kama ifuatavyo:

  • Mkurugenzi atapewa 20,000,000/=
  • Mhandisi 10,000,000/=
  • RC 30,000,000/=
  • DC 23,000,000/=
  • Mhasibu 10,000,000/=
  • Consultant 10,000,000/=
  • TAKUKURU 20,000,0000/=
  • Wengineo 20,000,000/=
Jumla Tshs. 143,000,000/=

Kwa hiyo 500,0000,0000/= kutoa 143,000,000/= inabaki 357,000,000/=

Matokeo ya mwisho kabisa ni Mradi kutekelezwa chini ya kiwango au kusuasua.

Mbaya zaidi ni kwamba, uozo huu wote unaendelea wakati Mbunge yupo, Madiwani wapo na Viongozi wengine wa Chama wapo na hawachukui hatua kwa sababu wanaofanya makosa hayo ni Wanachama wenzao(KULINDANA)

Anyway, ngoja iendelee kunyesha tujue panapovuja ili 2024/2025 tufanye Mapinduzi ya Kihistoria.
 
Hii kauli hii.....

"Anyway, ngoja iendelee kunyesha tujue panapovuja ili 2024/2025 tufanye Mapinduzi ya Kihistoria.

Tunachokijua:"
 
Kwamba AMIRI Jeshi mkuu mnamwita mamaenu, tatizo ndo lilianzia hapo!
 
Kwanza kabla ya hapo mkataba wa kwanza utasoma M 500,000,000 kisha utatengenezwa mkataba wa pili wa fedha M. 357,000,000 , pia ikumbukwe kuwa katika kipindi chote cha mradi unaendelea kutakuwepo na mvutano wa kimaslahi kati ya hao wengineo na Mkandarasi.
 
Na miradi hiyo ipo kibaooo, can u imagine vile wanapiga hela!
 
Huyo mamako hajitambui kabisa!

Ana kila nyenzo alafu bado anahujumiwa
 
Hajahujumiwa.

Hayo matatizo yalikuwapo kabla hajawa rais. Yeye amechaguliwa kuyamaliza.

Kama kashindwa kuyamaliza, kashindwa kufanya kazi yake.
 
Ukiwapa watu vyeo kwa lengo la kusuka mtandao wako wenye maslahi ya kisiasa badala ya watu waadilifu na wenye uwezo unategemea nini?? Ameyataka mwenyewe.

Kinachosikitisha ni kwamba anayeibiwa ni mdanganyika wa kawaida. Analipishwa kodi kibao, alafu wahuni wanazipiga tu.
 
Hao viongozi wa chama nao wanalambiswa asali wanatulia..kumbuka serikali ya ccm hakuna muadilifu wote wahuni tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mama piga kazi tumecheleweshwa mnooo kama taifa zaidi ya miaka 7.





Tunachokijua:
 
Nachukizwa sana na mtu anayesema kuwa rais anahujumiwa, wakati rais ana masikio na macho katika kila pembe ya nchi anayoongoza,yeye ndo mwenye kuajiri na ndio yeye mwenye mamlaka ya kukupiga chini. Kusema mama anahujumiwa ni unafiki kwa mleta uzi, ukweli utakuweka free sema mama ana benefit na huu ujinga wa viongozi wake aliowateua.
 
Inaumiza sana.
 
WACHA WAZIPIGE Tanganyika SHAMBA la BIBI kumbuka kusema CVM OYEE
 
Hiyo kidogo sn watu wanapiga haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…