Poleni sana mussa hussein na wasiwasi mwabulambo wa clouds fm kwa kufanya kazi na huyu "kibonde"

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
1,684
Reaction score
2,156
Habari wana JF, Nimelazimika kuwapa pole hawa vijana kwa kazi ngumu wanayoifanya na huyu Kibonde ambaye ki ukweli si kwamba ni kada tu wa MAGAMBA,bali hata kichwani hana kitu!!!!!! yaani ni empty kabisaaaa!! Leo wanaongelea matokeo ya kidato cha nne ambayo kila mtu anajua kuwa ni mabaya na kwa kiasi kikubwa matokeo haya yamechangiwa na uzembe mkubwa wa serikali na watendaji wa wizara ya elimu kwa ujumla HASA KWA DHARAU WANAYOONYESHA KWA WALIMU AMBAO NDIO WADAU WAKUBWA WA ELIMU. Huyu jamaa; KIBONDE, yaaani kila kitu anatetea serikali. Anachoongea kinatia kichefuchefu. Hawa vijana; WASIWASI NA MUSSA, kila wakijaribu kwenda kinyume nae yeye anapinga na anakuwa mkali. yaani anawadrive na lawama kibao kwa kila anayesema kuwa haya ni matokeo ya uzembe na umburula wa serikali wa kutoijali ELIMU na wadau wa Elimu hasa WALIMU kwa kutowaheshimu. HILI NI FUNDISHO KWA SERIKALI NA JAMII KWA UJUMLA KUIPA KIPAUMBELE SEKTA YA ELIMU KWA KUANZA NA KUSHINIKIZA WAZIRI KAWAMBWA AJIUZULUUUU!!!! nataman sana huyu jamaa aondoke kabisa kwenye media kwani ana boa
 
Inaelekea hizo ni Chuki binafsi zako kwa Kibonde tatizo la kufeli kwa wanafunzi si tatizo la Walimu wala Serikali bali ni kwa Wanafunzi wenye walio jiweka kizembe na kusubiri kila kitu kutoka kwa Mwalimu.
 
Inaelekea hizo ni Chuki binafsi zako kwa Kibonde tatizo la kufeli kwa wanafunzi si tatizo la Walimu wala Serikali bali ni kwa Wanafunzi wenye walio jiweka kizembe na kusubiri kila kitu kutoka kwa Mwalimu.
Teh teh teh!hoja nyepesi kwa suala zito!
 
Mdogo Kibonde ana ndoto ya hisani fulani - ikiwemo ukuu wa wilaya, hivyo harekebishiki.
 
Inaelekea hizo ni Chuki binafsi zako kwa Kibonde tatizo la kufeli kwa wanafunzi si tatizo la Walimu wala Serikali bali ni kwa Wanafunzi wenye walio jiweka kizembe na kusubiri kila kitu kutoka kwa Mwalimu.

sikatai mtazamo wako, ila kweli ndo mtu ukatae kulinganisha ufaulu wa shule za binafsi na zile za serikali?? ki ukweli si kweli kwamba wote waliofeli wamejiweka kizembe, wengine imetokea kwasababu ya mazingira magumu wanayokutana nayo kwenye shule za kata. hebu fikiri, kwanini zamani wanafunzi walifurahi kuchaguliwa shule za serikali, Ari hiyo iko wapi kwa sasa??
 
Inaelekea hizo ni Chuki binafsi zako kwa Kibonde tatizo la kufeli kwa wanafunzi si tatizo la Walimu wala Serikali bali ni kwa Wanafunzi wenye walio jiweka kizembe na kusubiri kila kitu kutoka kwa Mwalimu.
kwenye mambo serious punguzeni upuuzi,
kweli katika siku niliowahi kukasirika kwa kusikiliza jahazo ni leo. Kibonde anadiriki kusema eti mtoto anaandamana barabarani kudai walimu waingie darasani ndio sababu za kufeli?? Thhis is stupidity mussa kamuuliza si wanaandamana kudai haki yao ya kufundishwa. Anajibu eti watoto wametumwa sio wao,wametumwa na walimu. Huyu mtu ana matatizo au hana akili. Pumbavu sana samahanini wakubw nimeghafirika kweli kweli
 

zaidi ya hayo anasema eti mwanafunzi anayediriki kuandamana eti hajui na hawezi kujua umuhimu wa shule!!
 
sio kwa kibonde tu, aibu kwa clouds media nzima hususani PJ, Gerald Hando na Barbra ambao wiki iliyopita walitumia takribani wiki nzima kuunga mkono juhudi za spika kuzima hoja binafsi ya Mh Mbatia na kuhusu kutorushwa bunge live... walitumia nguvu kubwa sana, na umahiri mkubwa kuponda na kukandia wabunge eti wanajishaua.. sasa haya matokeo ni aibu gani kwa taifa? wanajisikiaje sasa kuyaona hivi wakati ni wiki iliyopita tu walikuwa wanamponda Mbatia kwa hoja binafsi na kumkebehi eti akijiuzulu wao sijui watajiua sijui nini.... loh, hii redio mbona ina vihiyo kiasi hiki???

nilidhani leo wangekuwa wakali kweli, lo, sisikii yoyote akitoa matamko tofauti na serikali... hawa ni wauaji kabisa....

 
zaidi ya hayo anasema eti mwanafunzi anayediriki kuandamana eti hajui na hawezi kujua umuhimu wa shule!!

Kwani kibonde matokeo kama haya alipataga ngapi?
samahani lakiniiiiiii......!!!!!
 
Dogo wangu alikua kasoma shule ya kata(ILALA SEC)pale Kipawa.
Alikua anakesha ingawa shule yake ilikua mbovu,matokeo yametoka kapiga 1:17!
Mie nilisoma shule moja ya day nikapanga chumba huko huko maana ilikua ni kama km 29 kwenda na kurudi na nikamaliza mwaka 1997,shule haikua nzuri maana mara ya mwisho kufaulisha vzr ni mwaka 95 kupata Dv3-1.
But mwanaume nilijipanga kisawasawa na my best friend wangu mmoja hivi ambaye kwa sasa ni marehemu,nikatoka na 1:18 huku yeye akipiga 1:9.
So mwanafunzi inabidi ajitambue kwanza kabla ya kuilalamikia serikali yake sikivu.
 
Serikali haina kosa kwa hili mimi nitaitetea.
Wanafunzi hawasomi bana na sio kuwa shule za serikali pekee ndio zimefelisha hata binafsi.
Wanafunzi ndio wa kubeba lawama na sio serikali
Kipi bora kati ya kuonesha ukweli kuwa mwanafunzi hajui au kumpatia max ili serikali ipewe sifa?
 
Well noted. Tatizo ni wanafunzi wenyewe na siyo Serikali au waalimu.
Nimemsikia kibonde, kaelezea vizur na kaelezea vizuri umuhimu wa mzazi/mlezi katika kufanikisha kufaulu kwa mtoto/mwanafunzi.

Inabidi tuache chuki binafsi kwa Kibonde! Siyo kila kitu anachosema tukipinge tu!!
 
Swala hili ni tata kigogo mimi matokeo haya nizao la kutoheshimu taluma za watu na uzembe wa wizara pamoja na serikali,jamani tukumbuke mwaka jana hawa jamaa walilazimishwa kurudi kazini kwa nguvu ya mahakama walipokuwa na mgomo kudai stahili zao leo matokeo mabaya mnashangaa nini? serikali hii kama haioni hili eti ni kwa sababu ya kukosa maabara kama alivyo sema waziri sio sahihi hivi Kiswahili ,Hesabu,maarifa ya jamii na kadhalika vya hitaji maabara? mimi nimesoma elimu mabara wala hazikuwa hivyo lakini watu walifaulu ,tusitafute mchawi tatizo ni kutothamini mchango wa walimu katika elimu ya nchii.
 

lazima serikali nitailaumu tuu na Huyu Kibonde nitampolomoshea lawama za kutotumia media vizuri kwa kuitetea serikali hata kwa mambo ya kipuuzi: Hivi mtu unae fikiri vizuri unaweza kuitetea vipi serikali iliyofuta mitihani ya kidato cha pili (na hawa ndo sample yenyewe ya waliopita tu) bila sababu ya msingi??? Serikali inayowapeleka secondary wanafunzi waliofeli darasa la saba ili tu, wote wafike secondary!! Serikali inayoamuru mtihani wa darasa la saba maswali yote yawe ya kuchagua??? serikali ambayo hadi leo inatumia sera ya elimu ya mwka1995??? serikali inayojenga shule nyingi za kata na huku ikjua kabisa shule hizo hazitakuwa na walimu wa kutosha??? Serikali ambayo imeruhusu kila mwenye kutaka kuandika kitabu kwa ajili ya wanafunzi aandike na akiingize sokoni??? serikali isiyotaka kuwapa walimu stahiki zao na wakizidai kwa nguvu tunaanaambiwa eti UALIMU NI KIMBILIO LA WALIOFELI!! Kwa upande wangu serikali haiko siriass na elimu ya watoto wetu wala si chuki binafsi kwa serikali wala huyo KIBONDE "MAJI"!! by the way anauhuru wa kutoa maoni yake lakini anatakiwa azingatie ethics za taaluma yake "kama anayo , samahani lakiniii"
 
Kibonde mwenyewe alipata four. Alishajaribu kure-seat lakini mambo yakaendelea kuwa mabaya. Sasa unategemea huyo ukimpa kipindi cha uchambuzi atatoa analysis gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…